Ukusanyaji mapato mradi wa Mwendokasi: UDART yamaliza mkataba na MaxMalipo, kusaini mkataba mpya na TTCL..

Dar es Salaam. Kampuni ya Usafirisha wa mabasi yaendayo Haraka(Udart), imemaliza mkataba na Max Malipo Africa katika ukataji wa tiketi na sasa huduma hiyo itafanywa na Kampuni ya Simu(TTCL).

Hayo yamesemwa leo Aprili 13, na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano wa kampuni hiyo, Deus Bugaywa alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mabadiliko hayo.

Amesema mabadiliko hayo ni moja ya njia ya kuboresha huduma zao ambapo TTCL kutokana na kuwa na mkongo wa taifa wanaamini wateja wao watapata huduma iliyo bora.

Kuhusu wafanyakazi waliokuwa wakikatisha tiketi, amesema wataendelea na ajira zao kwani hata awali walikuwa wanaripoti kwa Max Malipo lakini masuala ya mshahara walikuwa wakipewa na Udart.

"Katika mabadiliko hayo sasa wakata tiketi hawa wataripoti TTCL na mshahara kuendelea kupewa na Udart,"amesema Bugaywa.

Chanzo: Mwananchi

My Take
Hongera kwa TTCL kwa kupata tender hii sasa kazi ni kwenu kuonesha utofauti katika huduma.
Uzembe na umangimeza ndio kinafata TTCL wameshinda kusambaza hata network yao hata hapa Dar tu.
 
Tender hii ilitangazwa lini ? , Sheria ya manunuzi na Mauzo ya PPRA Zinasema haswa kuhusu miradi hii inayosimamiwa na private firm's ?
 
Tender hii ilitangazwa lini ? , Sheria ya manunuzi na Mauzo ya PPRA Zinasema haswa kuhusu miradi hii inayosimamiwa na private firm's ?

Hakuna tender yoyote..Si unajua Chattle hajui kitu kinaitwa PPRA...yeye anashusha manunuzi tu....

Ulishaona serikali hii inafuata sheria lini mkuu?
 
Kila kitu ni mipango mkuu hata USA ilikuwa imefunikwa na Ujerumani enzi za Hitler lakin wakati wa vita kuu mbili za dunia zinapiganwa USA alijiongeza akatengeneza silaha za kijeshi,uchumi wake ukakua na leo ni world superpower. Hayo yote yaliwezekana sababu ya mipango mkuu. kwa hiyo hata TTCL wakijipanga vizuri wanaweza kufanya kweli.
Acha kufananisha US na nchi kama Tanzania ww. Tupo tofauti kwa kila kitu, ndo mana kuna watu huwa wana argue kuwa ukiwatoa waTz woote uwapeleke US na uwatoe waUS uwalete hapa bongo, after years bongo itakuwa km US na US itakuwa kama Bongo (na si kwamba tunajidharau no, ila tunadharau prerequisites for Dvt km tulilolifanya sasa).
Kama hujui mradi wa mwendo kasi una under perfom vibaya mno. Jaribu tu ku google uone magari ambayo ilibidi yawe yanaoperate na sasa ni magapi yanaoperate achilia mbali madereva wao ambao hawapo trained (they have zero innovative ideas), vitu vingine vingi tu. Halafu unaleta mtoto mwingine(TTCL) Aje akulie kwenye mazingira ya inefficiencies and unataka kufananisha US na TZ kweli?!!watch out
 
Wabongo wengi tuna mihemko, hatuna logical reasoning na ndio maana maendeleo yetu ni duni, every challenge can be an opportunity, Sasa hapo ndio pagumu, tunaishia kulalamika tu.
Elezea hoja yako hata kwa vivid examples. Unaweza kufikiri wenzako wana mihemko kumbe wewe akili yako ndo imelala km wengine wanavyotaka TTCL Ikulie kwenye molono wa mwendokasi(dart)
 
Hongereni sana ttcl na tuna taraji makubwa na yenye tija kwa hicho ulichotunukiwa (sbb hakukuwa na competitive bidding)
Angalizo sioni namna ya kuboreka kwa kuuza tiketi ikiwa ulishindwa kuboreka kwenye kuuza data pamoja na kumiliki mkongo .Hukushiba kwenye sinia huwezi shiba cha kuokoteza kwenye mkeka
 
Umezaliwa lini...?
Umewahi kutumia simu za kupiga kwa opereta ili akuunganishe..?

Kampuni zote za simu unazoziona leo zimeikuta na kuipita TTCL kwa ufanisi....jiulize walikosea wapi...achana na habari ya kujipanga vizuri...
japo sijazaliwa zamani sana lkn nimewahi kutumia.
Ukweli wangu nadhani utabaki palepale, Siku hao jamaa watakapoamua kubadilika hakuna Mtandao Tanzania Utawafikia.
nimewahi kupitapita kwenye mitandao inayofanya vizuri na ya zamani kidogo hasa kwenye technical department. Kwa miundombinu tu ya TTCL ambay o coverege ilikuwa kubwa sana kwa wakati huo. Wakiweka mikakati Vizuri naamini wanaweza kufanya vizuri sana.
 
Elezea hoja yako hata kwa vivid examples. Unaweza kufikiri wenzako wana mihemko kumbe wewe akili yako ndo imelala km wengine wanavyotaka TTCL Ikulie kwenye molono wa mwendokasi(dart)
Endelea kuwa mtabiri wa mitandaoni mkuu wewe mwenyewe mbona hujatoa vivid example zaidi ya porojo tu?
 
Endelea kuwa mtabiri wa mitandaoni mkuu wewe mwenyewe mbona hujatoa vivid example zaidi ya porojo tu?
Fuatilia comments zangu hapo juu. Halafu sio kila uzi lazima ucomment mzee!! Zingine ziwe sehemu ya wewe kujifunza. Shida ya mbongo anajifanya anajua kila kitu. Ukifuatilia vizuri huu uzi utaona watu wanaojua yahusuyo private sector wameshusha nondo zao. Sasa km hujui kuhusu private sector si ukae ujifunze? By the way ni mara chache sana Gvt inaweza kufanya biashara na ikafanikiwa. Nadhani TBA wamekuwa mfano mzuri ktk hili. Karibi kila halmashauri, wakala waliowapa TBA tender wanalalama tu.
 
Sababu ya kuwa na mkongo wa taifa hainifanyi kuamini kwamba TTCL watatoa hiyo service kwa ufanisi mkubwa kuliko hao waliomaliza muda wao. Ngoja tusubiri tuone sisi akina Thomas
Na waliandaliwa/walijiandaa kwa hili? Acha matomaso tuongezeke..
 
Max malipo ni akina nani?
Naona mikataba yote na taasisi za serikali zinasitishwa baada ya mkataba kwisha.
Kwa ttcl sidhani kama wataweza hii kazi, kwani hata ile ya mawasiliano tu imewashinda.
Tutarajie mikwamo ya kila siku.
Poleni sana Max malipo.
 
Kumbe UDART mnadaiwa na maxmalipo hela ya service ya kukusanya nauli, hamna jinsi hapa! Mlipe tu maana pesa mnakusanya nyingi tu.

Hii ya kuyokusainiana nao mkataba mpya kumbe ni janja ya nyani tu.
 
Back
Top Bottom