Ukosefu wa uvumilivu unavyowanyonya watu haswa vijana

ANTDOTE

JF-Expert Member
Oct 14, 2023
217
605
Kuna dogo Jirani kanunua simu toka mahala Fulani, aina ya SAMSUNG A04s kwa utaratibu wa kulipa shs 90,000/= mara Moja na kisha kuendelea kulipa shs 1500/= Kila siku kwa mwaka mzima.

Kimahesabu itakuwa ni shs 90,000+ (1500 x 365) = 637,500/=

Simu hii kwa bei ya Sasa unaweza kuipata kwa shs 279,000/= Hadi 340,000/=. Ndio kusema Hadi dogo amalize deni atakuwa amelipa fedha ya karibia au sawa na Simu 2.

WAGALATIA 3:1
Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga?,
 
Utakuta kijana wa miaka 23 anamiliki macho ma 3
Alafu anakuja anakuambia Brother naomba uniwezeshe mtaji nifanye biashara ya nguo

Namuangalia alafu nawaza Huyu Dogo mkononi Hiyo simu aliyoshika ni ya Mil 2, alafu ameinunua kwa Cash siyo mkopo, Alishindwa nini kuvumilia na kununua simu ya kawaida ya 200k alafu iliyobaki uwe ndyo mtaji?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom