Uko kwenye kundi gani kati ya haya? Kwa wewe mwenye ndoa

Latifaa

JF-Expert Member
Jan 18, 2012
501
257
kwenye ndoa kuna makundi kama 5:
1. Walioolewa
2. Waliooana
3. Wanaolazimisha ndoa
4. Waliooa wanaume
5. Wanaotumikia ndoa
haya makundi ni ya wanawake ila wanaume pia
mmeguswa.

Hawa watu hawafanani hata kidogo japo wote ni wanandoa.
1. Walioolewa: hawa wana wanaume wanaojielewa wako wapi na wanafanya nini na wanaelewa nafasi yao
kwenye familia na wamesimamia nafasi zao bíla kutetereka na hawasaidiwi nje, nyumba zao zina msimamo na hawayumbi.
Kwamfn. Mwanaume anafanya majukumu yake bila kutega, kama kulisha familia, kutoa adaya shule, kulipa bili
zote, hela ya saluni ya mama, zawadi kwa mama na watoto, mafanikio yakitokea anajenga nyumba anafungua
miradi nk. Hapelekwipelekwi na mkewe na siku mkewe akimletea zakuleta anarudi sha kwao.
2. Waliooana: hapa ngoma droo, wife akiwa na hela anafanya maendeleo sawa na baba, unakuta baba ana biashara yake na mama ana yake kila mtu anajijua alipopata hela, muda wa kurudi home kila mtu anarudi anavyotaka na haulizwi, hapa mfumo dume hakuna chochote mnachonunua mnachanga
sauti kati ya baba na mama zimelingana kila mtu na jeuri yake, swala la mapenzi ni makubaliano, kuzaa makubaliano , mwanamke hafukuzwi hapa ataakikosa wala0kunyanyaswa labda
mtengane kabisa, ubabe kwakila mtu sio jambo la ajabu, ukiona hiyo hali jua hujaoa wala kuolewa hapo bali mmeoana

hayo yaliyobaki nitamalizia kesho namba 3-5.

Usingizi wakuu
 
Kundi langu halipo hapo,hebu ongezea kundi la sita la kulelewa(ndio mm)
 
Sawa tunasubiri makundi ya kesho, ila usisahau kuweka na lile kundi alilohalalisha obama
 
Kumbe na wewe umeolewa/oana (whatever)? Mi kundi langu halipo hapo. Si unajua makundi hayawezi kuwa universal
 
Kuna classification za ndoa pia? Kha!
Na za wachumba ndo zipi, tafadhali ndugu mwandishi..
 
Back
Top Bottom