Uchoyo kwenye Ndoa, Mkeo na watoto wamekondeana alafu wewe umenawiri

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
UCHOYO KWENYE NDOA, MKEO NA WATOTO WAMEKONDEANA ALAFU WEWE UMENAWIRI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Wakati nakua Wazee wangu walitupiga marufuku kula bingo. Bingo ñi chakula ambacho vijana wanachanga pesa kisha wanaenda kukipika, inaweza kuwa Nguna(ugali) na samaki au nyama yenye kachumbari.
Pia walitupiga marufuku kula kwa mama ntilie. Hata kama tunahela zetu binafsi.

Nilipojaribu kuwauliza, walijipanga ufafanuzi kuwa, tabia hiyo ya kula bingo na vijana, kula kwenye magenge ni moja ya tabia zinazoweza kumfanya kijana baadaye aje kuwa mchoyo ndani ya familia yake.

Kama unachakula au unahamu ya chakula fulani na unapesa, basi nunua hicho chakula leta nyumbani Watu wale wote kwa pamoja.

Uchoyo ndani ya ndoa unatokana na sababu nyingi. Zipo sababu za kiasili, lakini nyingi za sababu zinatokana na makuzi, malezi pamoja na mazingira.

Unakuta mwanaume yupo Bar anakula nyama na pombe ilhali nyumbani kwa mkewe na watoto hajaacha kitu. Au ameacha unga na maharagwe. Huo ni uchoyo, ubinafsi na tabia mbaya sana.
Kama unajijua unatabia za namna hii ambazo kimsingi ni tabia za hovyo ni akheri usiwe na familia.

Uchoyo ni pamoja na kutaka kula vizuri pekeako.
Unang"'ang'ania kuwekewa mapaja pekeako, mkeo na watoto unawatelekeza. Hiyo ni roho chafu ya uchoyo.

Kile kizuri unachokitaka basi wape familia yako. Au gawana nao,au wekeni zamu ili kila mmoja apate hicho kizuri.

Umaskini au kipato kidogo haijawahi kuwa sababu ya kushindwa kuihudumia familia yako. Kuijali na kuipenda. Ubinafsi na roho mbaya ndio chanzo kikuu cha mateso na kushindwa kuitunza familia yako.

Ili familia yako iwe na nguvu, umoja,upendo na mshikamano ni lazima mjitahidi sana ninyi Mke na mume kuondoa ubinafsi na roho mbaya. Kila mmoja amtangulize mwenzake.

Haipendezi Mwanaume kuwa mchoyo tena kwa mkewe na watoto.

Jitahidi kuwianisha ndugu zako na familia yako. Upo ule uchoyo mwingine wa sisi wanaume unakuta unawajali ndugu zako kuliko kumjali mkeo. Huo ni uchoyo wa kiwango cha juu kabisa. Na bahati nzuri Watu wa aina hiyo wanatabia ya hapo juu ambayo ni kujipenda wenyewe kuliko familia yake.

Watibeli hatuishi hivyo. Tunajua nafasi ya kila mmoja wetu katika maisha yetu. Kila mtu ananafasi katika maisha yetu iwe ni nafasi ndogo au kubwa lakini itaheshimiwa na kulindwa.
Mke atabaki kuwa sehemu kuu ya familia yetu, watoto watakuwa sehemu ya mzunguko wa pili katika familia yetu. Wazazi,ndugu, jamaa na marafiki.

Tusiwafundishe wanawake ubinafsi.
Kiasili wanawake ni wabinafsi kwa sababu wanataka kupendwa na kupendelewa zaidi . Lakini wanawake hujifunza upendo na ukarimu kutoka kwetu.

Mwanamke ataku- treat the way unavyomchukulia na unavyomtendea.

Wanaume wengi wamekosa pesa na msaada wa wanawake kwa sababu wanashindwa mambo madogo wanapokuwa mbele ya Wanawake.

Wanawake ni Watu wa visasi. Weka akilini hiyo. Ukimfanyia wema naye atakufanyia Wema. Ndio maana wanaume wenye akili hawaruhusu Wake zao kupewa zawadi au kupewa Wema na wanaume wengine kwa sababu wanawake ni Watu wa kulipa iwe hisani au kisasi.

Pia wanawake ukiwafanyia Baya hasa linalogusa hisia zao. Hesabu unadeni ambalo utalilipia tuu ikiwa hautakuwa Makini.
Ukimfanyia uchoyo mkeo lazima atakulipa iwe nyakati za uzee au vyovyote vile.

Kuna ile tendency ya wanaume kuwachukulia wanawake kama sio Watu na wakati mwingine kama watoto. Unamfanyia Mwanamke jambo fulani zuri labda kumsomesha, au kumpa jambo fulani kubwa. Basi kila mara unatumia jambo hilo kama fimbo. Hiyo tabia inajenga uchungu na hasira kwa wanawake wengi.
Ni kama manyanyaso. Ni kiashiria cha kutokuwa na mapenzi na huyo Mwanamke.

Wanawake hujisikia hali ya hatia na kulipa hisani pale unapomfanyia jambo alafu hausubiri shukrani na wala huhesabu, ni kama umelisahau. Hukuona kama mwanaume ambaye anastahili kupewa heshima na malipo ambayo yeye hawezi.

Tuache uchoyo.
Ujumbe huu ni kwa wote lakini mara hii nimeuelekeza zaidi kwetu sisi wanaume.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Wanaume wanaojipenda sana kuanzia chakula mavazi mpaka manukato, wengi wao wana tabia ulizozianisha hapo juu. Yaani unakuta mtoto ananunuliwaa nguo sikukuu mpaka sikukuu lkn baba kila siku anajifanyia shopping. Hii ni tabia ya hovyo sana, Mungu atuepushe nayo
 
Upo sahihi ni tabia chafu sana mkuu ila kama kina mama wanaweza kuvumilia mume mchepukaji au mlevi nadhani hata hili wanaweza.

Mama na watoto watakondeana na kupauka iwapo baba ndio chanzo pekee cha kipato cha mama ila wife akiwa ile aina ya wanawake unaowafagiliaga kitakachotokea ni baba akienda huko kujificha kula kitimoto akirudi home anakuta mama na wanae wanakula vizuri tu na watoto hawatavaa matambara
 
Wengine Wana tabia za ajabu huwezi kuamini:-
-Anaweka saini kwenye unga ili akirudi na saini imefutika balaa huzuka.
-Anatiboa sufuria katikati ili maji ya ugali yakiwekwa yasivuke kipimo.Yakizidi yatavuja tu na kusumbua uwakaji wa moto.
-Kukatakata nyama na kuhesabu vipande.Vitaliwa kwa idadi anayotaka na muda autakao.
-Mlo mmoja wa wasiwasi usio kamili ndani ya masaa 24.
-Uvunjwaji wa hayo yaliyopo juu ni kipigo kwa mkiukaji hadi avunjike,kuvimba na/au kuvuja damu.
😂😂😂😂😂
 
Safari ya mafanikio itakuwa ndefu mno kwa huyu mtu
 
Wanaume wanaojipenda sana kuanzia chakula mavazi mpaka manukato, wengi wao wana tabia ulizozianisha hapo juu. Yaani unakuta mtoto ananunuliwaa nguo sikukuu mpaka sikukuu lkn baba kila siku anajifanyia shopping. Hii ni tabia ya hovyo sana, Mungu atuepushe nayo
Mimi nguo nawanunulia Sana kabla shule haijawakolea ,ikikolea wasahau labda wanikumbushe

Bwenini nguo za Nini ,kuonana maratatu au mbili kwamwaka
 
Wengine Wana tabia za ajabu huwezi kuamini:-
-Anaweka saini kwenye unga ili akirudi na saini imefutika balaa huzuka.
-Anatiboa sufuria katikati ili maji ya ugali yakiwekwa yasivuke kipimo.Yakizidi yatavuja tu na kusumbua uwakaji wa moto.
-Kukatakata nyama na kuhesabu vipande.Vitaliwa kwa idadi anayotaka na muda autakao.
-Mlo mmoja wa wasiwasi usio kamili ndani ya masaa 24.
-Uvunjwaji wa hayo yaliyopo juu ni kipigo kwa mkiukaji hadi avunjike,kuvimba na/au kuvuja damu.
😂😂😂😂😂

😂😂😂
Umeniharibia ratiba yangu mkuu.
Ratiba yangu inaonyesha leo ningecheka kuanzia 08:23 usiku mpaka saa 09:11 usiku
 
Ni tabia mbaya sana, japo siku hizi hata dada zetu wameanza haka katabia, anatoka kazini anapitia bar na kupiga vitu vya maana, then anaingia home mkavu....

😀😀😀
Hiyo tabia ya uchoyo inaweza kudhibitiwa na sisi wanaume.
Wanaume tukiamua hii dunia iwe sawa inakuwa. Sema hatutaki hilo litokee ili kujinufaisha(baadhi)
 
Upo sahihi ni tabia chafu sana mkuu ila kama kina mama wanaweza kuvumilia mume mchepukaji au mlevi nadhani hata hili wanaweza.

Mama na watoto watakondeana na kupauka iwapo baba ndio chanzo pekee cha kipato cha mama ila wife akiwa ile aina ya wanawake unaowafagiliaga kitakachotokea ni baba akienda huko kujificha kula kitimoto akirudi home anakuta mama na wanae wanakula vizuri tu na watoto hawatavaa matambara

Ni kweli kabisa.
Lakini hata kama Baba ndiye chanzo kikuu cha kipato kama upendo ndio unatawala huwezi sikia wala kuona tabia za kichoyo
 
Back
Top Bottom