Ukiweza ku 'survive' Arusha, basi wewe mikoa yote utaweza kuishi

Lupamba's grandson

JF-Expert Member
Jan 9, 2015
1,232
1,192
Habari ya saa hii wanajamvi,

Nimeona nilete uzi huu baada ya kukaa na kutafakari jambo hili. Mimi nimmoja wa watu wanaojivunia kuimaliza mikoa yote Tanzania kuizunguka sambamba na kuishi huko kwa miaka kadhaa na miezi isipokuwa Ruvuma na sehemu nyingine sijafika kiukweli ni Zanzibar na nina mpango huu mwaka Mungu akijalia nitafika niwe nimemaliza asilimia zote 100%.Katika kuzunguka na kuishi mikoa hii nimejifunza kitu ambacho uenda kwa asilimia 80% - 99% kuna ukweli mkubwa na kama kutakuwa na uongo basi watu watatoa hoja zao hapa.

**Swala liko hivi mtu akitokea ameenda Arusha kafika stand tuseme hana chochote, wala ndugu, wala rafiki wala pakulala, wala chakufanya then akaanza maisha kuanzia hapo from the scratch na akaweza kuishi na kuja kutoboa na kufika walipofika wengine nakuja kuonekana basi huyo mtu hata umpeleke mkoa gani hapa Tanzania ni rahisi sana kutoboa kwa hiyo basi nakamilisha kwakusema kama kichwa cha habari ni hivi;

MTU AKIWEZA KU 'SURVIVE' ARUSHA ANAKUWEZA KU HANDLE CHANGAMOTO ZOTE NA MAHITAJI YOTE HAKUNA MKOA ATASHINDWA KUISHI

Kama siko sahii pinga kwa hoja na sio matusi.
 
Ungetoa hoja zako kama vile gharama za maisha, fursa na nk ili tuweze kulinganisha kutoboa sometime inategemea na opportunity mfano mimi nimeishi kilimanjaro, Arusha, Dsm, Tanga na ZNZ kila sehemu kuna changamoto zake na unafuu wake kutegemea na kile unachofanya unaweza kufeli chuga ukatoboa Tunduma so ni mentality plus support sehem husika pamoja na lifestyle yko maana wanavyoishi chuga ni tofauti na tanga, zenji au sehemu yyte
 
Kutoboa ni akili yako na attitude yako juu fursa zilizkuzunguka popote ulipo na uwezo wako kupima mambo haijalishi unaish wapi mbona wapo walitoka arusha na bado wanasota tu kwenye mikoa mingine!
 
Aisee hili jambo linahitaji ufafanuzi zaidi. Nitaonge tofauti kidogo na mada yako. Kiasi fulani nakubaliana na wewe Arusha ni mkoa tofauti na mikoa mingi hapa Tz na utofauti huu ni rahisi kugundua kama umeishi hapa Arusha. Unajua sehemu mtu anapoishi (mkoa, wilaya) inaweza ikaathiri namana unavyoyawazia maisha. Kwa mfano Archuga na Moshi attitude inayotawala watu wengi ni kufanikiwa maisha materially na si vinginevyo.

Sasa hapa ukichunguza kuanzia conversations watu wanazungumza sana kuhusu miradi, wapi kuna dili nikajaribu, na kweli vijana wengi hapa wamefanikiwa. Kamwe usimdharau mtu hapa Arusha na wilaya zake Karatu, Ngorongoro, Monduli......unaweza kukutana na kijana ukadhani si lolote lakini wengi wanamiliki ardhi, wanalima na mishe mishe za tourism zinasaidia kuongeza kipato.

Kuna wakati nilikuwa na Wakenya wanaofanyia Segal Family Foundation tupo Karatu kufanya utafiti fulani....waliona wazi wazi wakazi wamejitahidi sana kimaisha.

Nimesimulia hayo yote kuonyesha hapa Arusha kuna attitude fulani watu wanajitahidi wafanikiwe materially na hii ndio inamfanya kila mtu aone.....aaah kwanini na mimi nisijaribu? Yes ukijaribu utakosea lakini utapata kujifunza na utafanikiwa. Do not quit.
 
Exactly 100%.

Nimeishi Ngaramtoni kule. Kuishi Arusha inahitaji uwe kichwa hasa kama hauna ndugu na wala huna pa kuanzia.

Itoshe tu kusema , Life ya Arusha ni National Examination ya kuhustle maisha hapa bongo.

Gharama za maisha Kule zipo juu.
Machalii mda wore ukiwazingua unakula kisu.
Full Baridi, Kama una ngiri au unaumwa kisukari lazima update mushkeli.

Changamoto halisi za maisha ya Tanzania zinapatikana Arusha.
 
Back
Top Bottom