Ukiwekwa Chini ya Ulinzi Yajue Yafuatayo

........niko mikononi mwa polisi, afande!!!!!!! maisha yangu bado ni mikosi, afande!!!! ===mtoto wa shule alikula kichapo hadi mauti==
 
Wana jf, Kumekuwa na ukamatwaji wa watu na kupelekwa kusikojulikana. Hii in kwa sababu watanzania tulio wengi,

1. Tunaheshimu Polisi na serikali.
2. Tunatii sheria bila shuruti.
3. Hatujui sheria ya kukamatwa.
Hii in kasumba ya siku nyingi tuliyonayo na ndiyo inatugharimu watu wetu.
Sasa nakuomba usikubali ukamatwa kama.,
1. Hayupo m/kiti wa mtaa au Kitongoji.
2. Mkamataji hajajitambulisha kwa kutoa kitambulisho cha kazi yake.
3. Akuoneshe kibali cha kukukamata chenye mhuri, tarehe ,kituo kilipotewa na sahihi ya Mkuu wake was Nazi.
4. Akuambie anakupeleka kituo gani.

Kama vitu hapo juu havipo, Huyo in mtekaji na mharifu sawa na Al shaabab.
Kubali kufia hapohapo ulipo maana hata ukikubali kuondoka naye kwa woga wako utaenda kufa tu.
Serikali inatengenezea watu wake kiburi cha kutotii.
 
IMEANDALIWA NA MAWAKILI.

1. Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki yako.

2. Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.

3. Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.

4. Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya kukamatwa.

5. Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.

6. Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kukri amri halali.

7. Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.

8. Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.

9. Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.

10. Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.

11. Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.

12. Ni haki yako kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.

13. Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.

14. Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.

15. Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.

16. Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.

17. Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.

18. Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.

19. Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.

20. Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.

21. Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.

22. Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.

HIZI ZOTE NI HAKI ZAKO, ZILAZIMISHE USIBEMBELEZE WALA USIZIOMBE.

SHARE UJUMBE HUU KWA WATU WOTE WANAO PENDA UTULIVU NA AMANI KATIKA KUPAMBANA NA UONEVU NA MANYANYASO YA VYOMBO VYA DOLA PALE AMBAPO UONEVU NA UKIUKAJI WA SHERIA NA HASA UBAMBIKIZAJI WA MA KESI YA UONGO....!


Source: facebook

23. Piga naye selfie ipost kabla hajakuteka



Asante baba mchungaji Gwajima kwa ushauri
 
Kama hizi sheria zipo Bongo sidhani kama askari wetu wanazijua.
 
Daa tatizo saa nyingine hivyo vyote vinavunjiliwa mbali na bado mtuhumiwa ukakosa pa kwenda, wa kukusikiliza na kukutetea.
 
Ukishapigwa tanganyika jeki unasahau yote hayo.tuambiwe na namna yaku file complaints za police malpractice tunafanyaje
 
Back
Top Bottom