Ukiwa Zanzibar Dar es Salaam ni Nchi za Nje!

eedoh05

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
632
234
Wananchi wa Zanzibar wamekuwa wakiichukua Dar es Salaam-Tanzania kuwa ni nchi ya nje. Katika mahakama mara kadha kesi uahirishwa itokeapo shahidi, mshitaki au mshitakiwa asipohudhuria mahakamani. Mahakimu wanapouliza mhusika imekuwaje hajahudhuria katika mashauri yamhusuyo? Iwapo mhusika huyo atakuwa safarini Dar es Salaam au mkoa wowote ulioko Tanzania bara; atajibiwa mhusika amesafiri nchi za nje yuko Dar es Salaam. Wewe usiyeyajua haya amini ndivyo ilivyo. Mahakimu wengi wanaohudumu katika mahakama mbalimbali huko Zanzibar watakuthibitishia.:whoo:
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Je kwenye official documents huwa wanatumia neno "nchi za nje" au ni kwenye lugha ya mazungumzo tu?
 
Kwahiyo na sie wabara tukienda Zanzibar tunaenda nje ya nchi?Waanze kutoa visa basi na kuomba za bara!
 
Kwahiyo na sie wabara tukienda Zanzibar tunaenda nje ya nchi?Waanze kutoa visa basi na kuomba za bara!
Lizzy wewe wa mwaka gani? Umesahau Zenji watu walikuwa wanaenda kwa passport/visa. Ni miaka ya 90's km sikosea hii kitu ndio iliondolewa. Ila kuja Bara ilikuwa ni free.
 
Lizzy wewe wa mwaka gani? Umesahau Zenji watu walikuwa wanaenda kwa passport/visa. Ni miaka ya 90's km sikosea hii kitu ndio iliondolewa. Ila kuja Bara ilikuwa ni free.
Mi wa zamani zaidi!Well kama ilishatolewa basi hatuwezi kuihesabia kama nchi nyingine.Wakubali tu kwamba Zanzibar ni sehemu ya Tanzania...na itaendelea kua hivyo mpaka siku upande mmoja utakapojitenga!
 
Kwa nini mnawalazimisha wenzenu, Wazanzibari hawataki Muungano jamani.

mwada-wachanwa-430x320.jpg


Zanzibar wanaamini wanajiweza kabisa bila Muungano, sisi ndio tumewang'ang'ania.

mzalendo_3-564x272.jpg

 
Zanzibara mnaringia mafuta?
mafuta yapi?zipo nchi zenye mafuta na wanayachimba na kuyauza sembuse hii zanzibar wenye mafuta ya "kufikirika"-wanachi wenyewe hawana uhakika kama mafuta yapo au hayapo-
KWA HALI ILIVYO WANA HAKI YA KUITA DSM NJE YA NCHI-NA SISI NI MUDA MUAFAKA SASA UMEFIKA WA KUWAITA FOREIGNERS
 
Nikweli ukiw Zenji, dar ni nje ya nchi kwakuwa kulikuwa na mipaka. na ndo maana hata ukinunua kitu huko na ukakilipia ushuru mfano Gari, ukitaka kukileta Dar utakilipia upya.
 
Back
Top Bottom