Ukiwa na moyo dhaifu usifungue ni ajari mbaya boda boda

TIQO

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
13,787
2,078
529058_328682440512117_100001110916827_789575_1404827954_n.jpg

Ni lini watanzania tunakabiliana na ajari za kizembe zinazo sababisha vifo visivyo tarajiwa?
Hii ni ajari imetokea maeneo ya ubungo kama unavyo ona dereva na mteja wa boda boda walilambwa na gari.
Je swala la usalama barabarani linaitaji kuwa swala la mtambuka?
Je Trafic polisi wameshindwa kazi za kusimamia usalama barabarani?
Kuna haja kuwepo na usalama shirikikishi barabarani pindi dereva anapo vunja sheria za barabarani raia wamkamate na kumfikisha sehemu husika badala ya kusubili Trafic ndo amkamate?
Taifa linapoteza nguvu kazi, vijana wanakufa vifo vya kizembe sana barabarani.
 
Hakuna ajali ya bahati mbaya..kila ajali inaipukika kama mtu binasfi akijali USALAMA WAKE
Safety first/Usalama kwanza... tukishaligundua hili ajali zitapungua au zitakwisha
 
529058_328682440512117_100001110916827_789575_1404827954_n.jpg

Ni lini watanzania tunakabiliana na ajari za kizembe zinazo sababisha vifo visivyo tarajiwa?
Hii ni ajari imetokea maeneo ya ubungo kama unavyo ona dereva na mteja wa boda boda walilambwa na gari.
Je swala la usalama barabarani linaitaji kuwa swala la mtambuka?
Je Trafic polisi wameshindwa kazi za kusimamia usalama barabarani?
Kuna haja kuwepo na usalama shirikikishi barabarani pindi dereva anapo vunja sheria za barabarani raia wamkamate na kumfikisha sehemu husika badala ya kusubili Trafic ndo amkamate?
Taifa linapoteza nguvu kazi, vijana wanakufa vifo vya kizembe sana barabarani.

kaka kweli ni tatizo,makosa yapo hapa. madereva wa magari wanawadharau sana hawa jamaa wa bodaboda,pili madereva wa bodaboda wengi hawajui sheria za barabarani na wanaharaka sana,tatu sisi abiria huwa tunachekelea tu hata kama dereva wa bodaboda anafanya ujinga akiwa kakubeba. issue ni abiria kuwa wakali na pia wao wazijue sheria za barabarani kwa usalama wao maan kama unajua utaratib utamwongoza dereva wako. nawakilisha
 
mmmh,

kwakweli kama ndio hivyo sitopande tena Boda boda

Pamoja na kwamba wenye makosa wengi ni dereva wa bodaboda lakini pia madereva wengi wa magari humu barabarani hasa hapa Dar es Salaam wanadharau sana kwa boda boda, unaweza kuta mahala ambapo anatakiwa kupunguza mwendo ampishe mtu wa pikipiki apite yeye hajali akijua hata ikitokea ajali hato pata madhara kwani yuko ndani ya gari,

kweli inasikitisha sana tena sana na sana lakini wote tunapaswa kuheshimu sheria za barabarani hata kama unaendesha loli unapaswa kumuheshimu mwendesha baisikeli na pikipiki

mungu awalaze pema peponi hao wahanga wa ajali hiyo. amina
 
Inasikitisha Sana!!!!!!!!!!

Hizi ndizo ajira 2000 alizotuahidi ............. katika kampeni mwaka 2005.

MIZAMBWA
INANUIMA SANA!!!
 
Ni balaa, tumekuwa taifa tusiojielewa, usalama barabarani ni jambo la mtu mwenyewe kwanza kisha jamii kwa ujumla, hata sheria iwe kali vipi, kama mtu hajali usalama wake ni kazi bure. Kama mwenye gari hamjali mwenda kwa miguu/baiskeli au pikipiki basi jamii imepotoka.Turudi nyuma tufundishane kujaliana, na kuheshimu haki ya mwingine kutumia barabara,ndipo tukazie sheria. Tatizo ni kubwa zaidi ya sheria, ni kutokujaliana.
 
Tatizo la bodaboda yaani huwa hawana muda kabisa wa kufuata sheria za barabarani. For example wanaambiwa wawashe taa zao za pikipiki but ni very rare kuona hicho kitu. Na zaidi sana kwenye makutano ya barabara, yaani mataa huwa hawa bwana wanakatiza tu bila kujali trafic anaita magari ya kwenda wapi au imewaka taa ya wapi? sasa kama mtu ametoka speed huko si anawabeba tu jamani. Nafikiri inahitajika elimu ya kutosha kwa hawa jamaa, or else trafic wanatakiwa wawe serious sana na hii mijamaa ambao wengi wao hawana hata lesseni.
 
Nani aliruhusu pikipiki zitumike kusafirisha abiria?? Ujinga mtupu!! Inashangaza sana ukilinganisha miaka ya 70s na 80s na wakati huu, usafiri dar ulikuwa wa heshima mabasi makubwa yenye kufuata ratiba inayoeleweka abilia wanaingia kwa mstari mabasi yenye mlango wa kuingilia na kutokea hakuna mpiga debe au konda mpanga watu kama magunia ya mkaa!!!! Sokoinne aliporuhusu dadala pia aliweka vigezo vya gari litakalo ruhusiwa kusafirisha watanzania. Vituko vilianza wakati wa mzee ruksa vikaja vipanya mara chai maharage na hali imezidi kuwa ovyo sasa hivi tuna bodaboda na kubebana migongoni( wakati wa mvua). Nataka mtu anieleze ni kwa nini badala ya kuendeleza kile kilicho chema sisi tuna boronga???? Mbona mwl pamoja na mapungufu yake kama binadamu aliweza kutuwekea mifumo inayoeleweka kwenye sekta zote??? tena hapakuwepo na technologia wala wasomi wengi Kama sasa?? Tatizo tumekosa watu wenye vision, wanaoweka maendeleo ya nchi mbele na bila watu kama hao hatuwezi kuwa na mfumo wa kimaendeleo kwenye sekta yoyote
 
Waziri wa ajira alikuwa ana zungumzia ajira hizi za boda boda zimeongezeka mara dufu.
 
529058_328682440512117_100001110916827_789575_1404827954_n.jpg

Ni lini watanzania tunakabiliana na ajari za kizembe zinazo sababisha vifo visivyo tarajiwa?
Hii ni ajari imetokea maeneo ya ubungo kama unavyo ona dereva na mteja wa boda boda walilambwa na gari.
Je swala la usalama barabarani linaitaji kuwa swala la mtambuka?
Je Trafic polisi wameshindwa kazi za kusimamia usalama barabarani?
Kuna haja kuwepo na usalama shirikikishi barabarani pindi dereva anapo vunja sheria za barabarani raia wamkamate na kumfikisha sehemu husika badala ya kusubili Trafic ndo amkamate?
Taifa linapoteza nguvu kazi, vijana wanakufa vifo vya kizembe sana barabarani.

Mie nadhani hawa madereva wa boda boda wao wana sheria zao za barabarani, maana wanajiendeshea wanavyojua wao wenyewe na hata abiria muda mwingine wako kimya tu
 
its inhuman, even to see them,so sypathy.My the living Lord rest their soul in peace.

Hope we shall also repy=AMEN
 
kaka kweli ni tatizo,makosa yapo hapa. madereva wa magari wanawadharau sana hawa jamaa wa bodaboda,pili madereva wa bodaboda wengi hawajui sheria za barabarani na wanaharaka sana,tatu sisi abiria huwa tunachekelea tu hata kama dereva wa bodaboda anafanya ujinga akiwa kakubeba. issue ni abiria kuwa wakali na pia wao wazijue sheria za barabarani kwa usalama wao maan kama unajua utaratib utamwongoza dereva wako. nawakilisha
lakini andhani madereva wa bodaboda ni notorious zaidi. Ukiangalia vituko wanavyofanya barabarani, ni vya hatari sana. Nawashangaa sana wanapokuwa kwenye trafic lights jinsi wanavyoshindana na magari!
 
Back
Top Bottom