LiverpoolFC
JF-Expert Member
- Apr 12, 2011
- 11,348
- 3,219
R.I.P Wapendwa wetu!
Kazi kweli kweli!
Kazi kweli kweli!
Inalilah wainalilah lajuun!!
Ni lini watanzania tunakabiliana na ajari za kizembe zinazo sababisha vifo visivyo tarajiwa?
Hii ni ajari imetokea maeneo ya ubungo kama unavyo ona dereva na mteja wa boda boda walilambwa na gari.
Je swala la usalama barabarani linaitaji kuwa swala la mtambuka?
Je Trafic polisi wameshindwa kazi za kusimamia usalama barabarani?
Kuna haja kuwepo na usalama shirikikishi barabarani pindi dereva anapo vunja sheria za barabarani raia wamkamate na kumfikisha sehemu husika badala ya kusubili Trafic ndo amkamate?
Taifa linapoteza nguvu kazi, vijana wanakufa vifo vya kizembe sana barabarani.
....Ni huzuni sana! Hata hivyo, nani alaumiwe?! Je, ni Wachina waliyetengeneza TOYO, SUNLG na pikipiki nyingine? Au, tuseme hizi ndio "ajira" kwa vijana wa Tanzania ambao hawatayarishwi kwa mafunzo maalumu ya matumizi ya vifaa vya moto (motor bikes) na sheria, kanuni na taratibu za matumizi ya barabara (kwa usalama wao na vyombo wanavyotumia)? Nadhani tuna wajibu wa kuchunguza kwamba ajali nyingi zinazotokea barabarabi zinazowahusisha madereva (vijana) wa BODABODA (PIKIPIKI) zinasababishwa na ukosefu wa weledi (maarifa + ujuzi (ustadi) + maadili) ya matumizi ya vyombo vya moto na matumizi ya barabara. Tuna wajibu kama taifa kuhakikisha kwamba vijana wanapojiajiri kwenye sekta ya uchukuzi wanaandlaiwa kabla ya kuingia kwenye kazi hiyo.
Hii picha sio ya Ubungo na ajali hii haijatokea Tanzania. Mleta thread athibitishe
Ni lini watanzania tunakabiliana na ajari za kizembe zinazo sababisha vifo visivyo tarajiwa?
Hii ni ajari imetokea maeneo ya ubungo kama unavyo ona dereva na mteja wa boda boda walilambwa na gari.
Je swala la usalama barabarani linaitaji kuwa swala la mtambuka?
Je Trafic polisi wameshindwa kazi za kusimamia usalama barabarani?
Kuna haja kuwepo na usalama shirikikishi barabarani pindi dereva anapo vunja sheria za barabarani raia wamkamate na kumfikisha sehemu husika badala ya kusubili Trafic ndo amkamate?
Taifa linapoteza nguvu kazi, vijana wanakufa vifo vya kizembe sana barabarani.
Ajali ni ajali tu...ndio maana ikaitwa ajali!
du binadamu wa maana ukiwa hai.!!
lakini andhani madereva wa bodaboda ni notorious zaidi. Ukiangalia vituko wanavyofanya barabarani, ni vya hatari sana. Nawashangaa sana wanapokuwa kwenye trafic lights jinsi wanavyoshindana na magari!
Ajali ni ajali tu...ndio maana ikaitwa ajali!