Ukiwa huna maono ya kisiasa utabeza hata viongozi wa Dini

njundelekajo

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
310
227
UKIWA HUNA MAONO YA KISIASA UTABEZA HATA VIONGOZI WA DINI

Chama cha siasa ni muungano wa watu wanaotafuta mamlaka katika dola na hasa serikali kwa kusudi la kutekeleza shabaha za kisiasa au za kifalsafa pamoja na faida kwa ajili ya vikundi flani au zao binafsi.

Ili kufikia lengo hilo la kusaka dola chama cha siasa ni lazima kijenge imani kwa jamii yake kupitia maono(vision) ambayo ndani yake huzaa vitu vingi ikiwemo sera na ilani za chama katika chaguzi.

Lakini pia hata viongozi na wanachama wa chama husika wana uwezo wa kuathiri mwelekeo wa chama kama hawatoshiba muono wa chama ama kutojua wajibu wao katika chama cha siasa..

Maono ingawa linaonekana ni neno linalopatikana sana kwenye mizania ya kidini na imani,lakini maana yake ni fikra za kinjozi ama uwezo wa kuona mbali.Maono katika maisha ya kawaida husadia kujua unataka kufanya nini na kwa wakati gani.

Maono yanataka kufanana na ndoto lakini tofauti ndoto hupatikana usingizini ilihali maono huja binadamu akiwa hana hata lepe la usingizi.

Chama cha siasa chenye maono huondokana na hali ya kudumaa na kushindwa.Chama cha siasa kipo kutekeleza mambo kwa mkondo maalumu.Ugunduzi wa mkondo huo ndio huitwa maono.

Maono ya chama cha siasa ni kuiona kesho yake kutoka leo.Ni mwisho maalumu wa chama hapo baadae kwa ajili ya kushika dola.Ni hatma ya kisiasa ya chama juu ya vile kinavyotaka kuwa baadae.

Kuna masuala chama cha siasa kinapaswa kuyaepuka kwa gharama yoyote ile.Moja wapo ni kukosa maono.Kosa hili linagharimu chama kwa kuwa na machaguo mengi ya masuala yanayokuja kukiweka chama kwenye nyakati ngumu hivyo kukosa kuaminika na inaweza pia kupunguza umaarufu wa chama.

Si kila jambo chama cha siasa kinapaswa kuweka mkono wake kama kipo nje ya malengo yake.Kinapotaka kujiingiza kwenye mjadala wowote lazima kipime uhusiano wa nguvu yake ya ushawishi katika suala husika lakini pia uhusiano kati ya suala lenyewe na lengo la chama.

Hivyo muono huzaa agenda mujarabu ambazo chama huunga au kuzipinga pamoja na kuziibua kwa ajili ya maisha ya baadae ya chama husika.

Husaidia pia kutambua mipaka ya kisiasa ya chama namna ya kujiingiza kwenye mijadala.Si kila mjadala una afya katika uhai wa kesho wa chama cha siasa.Ipo mijadala chama kinapaswa kunyamaza na mingine kujitokeza na kujibu.

Maono huweza kufanya chama kuondolewa au kuongezewa hadhi(stripped or deduction of honour and dignity) .Maono ni barabara kupitia inayoonesha wapi unataka kwenda.Pasi maono huenda kukawa hakuna mafanikio.

Vyama vya upinzani haivionekani kuielewa dhana hii kwa upana wake.Vimekua vikijitokeza ama rasmi au kupitia wanachama na wabunge wake mmoja kushiriki kwenye kila suala.Bahati mbaya katika upande waliopo utamaduni unawataka kupinga kila agenda inayoonekana kuifurahisha serikali ama chama cha mapinduzi.

Ndani ya chama cha siasa kuna kazi mbili za kufanywa.Kuna kazi za chama na kazi za siasa.Kazi za chama hufanywa na watendaji maalumu na kisha hubebwa na upande mwingine wa wanofanya kazi ya siasa kulifikisha kwa jamii/wanachama

Kazi ya chama inatokana na itikadi ya chama ni kazi ya kujenga chama.Kazi hii hupewa mtu anayekijua chama na aliyetayari kukifia chama.

Katika muundo wa Chadema kazi hii ilipaswa kufanywa na katibu mkuu wa Chadema Vicent Mashinji.Kwakua amepwaya kwenye nafasi hiyo watu wanaopaswa kufanya kazi ya siasa wanaifanya kazi ya kujenga chama katika njia isiyo jali maono .

Kundi la wanachama na wabunge wa chama hiko wanaowashambulia viongozi wa dini waliokutana na rais Magufuli si watu sahihi wa kufanya kazi hiyo ambao hawafahamu kama Chadema huko mbele itawahitaji zaidi viongozi wa dini kuliko viongozi wa dini wanatakavyohitaji Chadema.

Kosa kama hili la kuwaachia watu wasiofahamu maono ya chama kisiasa kufanya kazi ya kukijenga chama limewahi kuwaathiri Chadema katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2015.

Kwenye uchaguzi huo chama hiko kwenye kampeni zake kilitumia nguvu kubwa kumnadi mgombea ambaye wanachama na wabunge walimchafua kwa zaidi ya miaka 10.

Hivyo kulazimika kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja,kumsafisha Edward Lowassa na baadae kumuombea kura.Kama maono yangetumika ni wazi mashambulizi ya Chadema kwa Lowassa yangekua na mipaka.

Haitoshi wakati fulani pia katika namna ya kujenga chama hiko pasipo kua na maono,Chadema imewahi kumshambulia rais wa awamu ya nne Mrisho Jakaya Kikwete kua ni dhaifu na anayependa "kucheka cheka hovyo"

Katika hilo la udhaifu aliyekua Mbunge wa jimbo la Ubungo kupitia chama hiko,John Mnyika alisimama bungeni kueleza udhaifu wa Kikwete . Kauli hiyo inatafsirika pia ilisababishwa na kiongozi huyo kuwaachia wakosoaji wake wazungumze pasi na mipaka.

Leo Chadema ni wa kwanza kumlilia Kikwete.Inawezekana kabisa rais huyo mstaafu anakumbukwa zaidi na Chadema waliomuita dhaifu pengine zaidi anavyokumbukwa na wanachama wa chama chake cha ccm.

Machi mwaka 2015 Chadema ilimvua uanachama Zitto Zubery Kabwe ambaye kwa wakati huo alikua mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini kupitia chama hiko.

Labda zilikuwepo sababu sahihi kutosha kumvua unachama Zitto ,lakini ni dhahiri mbinu zilizotumika kumuondoa zilikua dhaifu na zilikosa maono ya kumwangalia Zitto baada ya mwaka 2015.

Kudhihirisha hilo leo Chadema inamtumia Zitto wa ACT kuliko hata inavyowatumia wabunge wake kama Lema na Mnyika kusukuma mbele agenda za kisiasa za chama hiko.

Kama wangeiona jana faida ya leo wanayoipata kwa Zitto basi bila shaka kumuacha Zitto anayeutaka uenyekiti ndani ya Chadema wakati ule lingekua jambo la maana sana kuliko kuramba matapishi ya kumtumia akiwa si mwanachama wala mbunge wa chama hiko.

Chaka cha mapinduzi kimefanikiwa sana kwenye eneo hili la maono.InawezekanaMiaka ukongwe wake wa miaka 42 dhidi ya mpaka 26 ya vyama vya upinzani unachangia.

Miaka kadhaa nyuma chama hiko kiliwahi kufanya mpango kama wa Chadema kwa Zitto kwa kuondoa wanachama na viongozi walionekana kukidhoofisha chama hiko.

Katika zoezi hilo lilipewa jina la Operesheni vua gamba inadaiwa ilikusudiwa kuwaondoa aliyekua mbunge wa jimbo la Igunda Tabora,Rostam Abdulrasul Aziz,Edward Ngoyai Lowassa na Endrew John Chenge.

Kwakua CCM ilikua na maono ya kisiasa haikutumia mbinu ya kuwanyang'anya kadi za uanachama .Hii ilitokana na ukweli kwamba majina hayo matatu ni makubwa kwenye siasa za Tanzania.

Walichofanya ni kuzunguka nchi nzima Nape Nauye aliyekua katibu wa itikadi na uenezi wa chama hiko na katibu mkuu wake Mzee Kinana kudhoofisha nguvu ya utatu huo mtakatifu uliokua ukitajwa lakini pia kukitenganisha chama na wao.

Zoezi hilo lilizaa matunda kwa Rostam kutangaza kujiuzuru ubunge,kupunguza nguvu za Chenge aliyetaka kujijenga kupitia nafasi ya spika wa bunge lakini pia kuliongeza"aibu" kwa Lowassa kuacha kuvitumia vyombo vya habari kwa uwoga wa kuulizwa maswali takribani miaka 8,hivyo kukaa kimya kuliko changia sana kupunguza nguvu yake kisiasa.

Hata Endrew Chenge mwenye miaka 61 sasa alipojaribu kujitutumua kugombea nafasi ya uspika mwaka 2005 CCM haikupata tabu kulikata jina lake kwa hoja ya "sasa ni zamu ya mwanamke" pasipo kuacha mpasuko ndani ya chama.Endrew Chenge alikwisha kamuliwa sumu yake yote na operesheni vua gamba.

Katika maono hayo hayo ya CCM dhidi ya Endrew Chenge chama hiko bado kinanufaika na uwepo wake ndani ya chama kwa maana ya kuongeza ya wabunge wa chama hiko lakini pia Chenge ni mwenyekiti wa kamati ya bunge.Ni vigumu kumuondoa Chenge katika siasa za Bariadi kwa miaka 10 iliyopita

Chadema wangekua na maono hata robo ingewasaidia kuifahamu nguvu ya Zitto ndani ya Kigoma kwa miaka 10 iliyopita leo ingejivunia uwepo wa Zitto kama mbunge lakini pia idadi ya wabunge wa chama hiko ingeongezeka kwa sababu hata kushindwa kwa David Kafulila katika uchaguzi kulichangiwa na kiongozi huyo wa sasa wa ACT Wazalendo.

Maono si kwa chama kama taaisisi hata wanasiasa mmoja wanapaswa kuwa nayo..Marehemu Julius Kambarage Nyerere alifanikiwa sana kuwa na maono ya kisiasa.

Maono hayo yalimpa misimamo sahihi iliyokuja kubadilika na kutengeneza imani.Imani ya watu kwa mwalimu iliisadia ccm kama chama.

Ingawa maono yale mara nyingine yalimuungiza kwenye migogoro lakini hayakupunguza hadhi wala imani ya watanzania kwake.

Mathalani, mwalimu aliwahi kutofautiana na mzee Ali Hassan Mwinyi kwa namna alivyokua akiongoza nchi katika baadhi ya maeneo ya msingi.

Aidha mwaka 1958 alitofautiana na wenzake ndani ya TANU. Tofauti hiyo iliyoleta mgawanyiko wa kifikra ndani ya TANU ilisababishwa na uchaguzi ulioitishwa na serikali ya kikoloni Tanganyika mwaka 1958.

Katika mkutano wa Tabora wa 1958 TANU iliamua kushiriki kwenye uchaguzi huo.Baadhi ya wanachama TANU wakiongozwa na Zuberi Mtemvu walitaka chama hiko kisishiriki uchaguzi huo.Kundi hilo baadae lilijitoa brain ya TANU na kuunda chama cha African National Congress(ANC).

Tofauti za mwalimu dhidi ya Kolimba,Malecela na Mwinyi inadaiwa ndizo zilizosababisha Mwalimu kuandika kitabu cha "Uongozi wetu na hatma ya Tanzania"

Kwa hivyo si kweli kuwa na maono ya kisiasa kunamfanya mwanasiasa asitofautiane kimtazamo,fikra na mawazo dhidi ya watu wengine.Kazi ya siasa katika ujumla wake ni pamoja na migogoro ya fikra.

Kuwa na maono kwa mwalimu kulisababisha aaminike mno na Miami hii ya liwasaidia wengi nje ya yeye mwenyewe akiwepo Benjamini Mkapa mwaka 1995 aliposhinda urais uliokua na upinzani mkali toka kwa Augustino Lyatonga Mrema wa NCCR Mageuzi.

Upinzani hasa Chadema unapaswa kujua mafanikio ya chama cha siasa sio kushinda kila uchaguzi na kila agenda au mjadala bali pia ni pamoja na kufanikiwa kuongeza thamani ya taswira ya chama cha siasa.Wasiwe watumwa wa mijadala na mambo yenye kuifurahisha ccm.Wasimame kwenye maono yao kama yapo.

Ili kufanikiwa katika hili ni kuchagua kunyamaza bila chama kujihusisha kwenye masuala yasiyo na mbadala zaidi ya kusifia.

Sina hakika kama yupo anayeweza kufanikiwa kuwaaminisha watanzanzania kwamba viongozi wote wa dini wanatumiwa na serikali.

Ni hawa hawa waliosifiwa wakati ule walipotoa waraka maalumu ulioioksoa serikali.Ni hawa viongozi wa dini ambao Chadema alifuata ushauri wao wa kuhairisha operesheni UKUTA mwaka 2016.

Leo wamesimama kwenye kweli isiyowapendeza upinzani wanadhihakiwa,kuangwa,,kuzodolewa kama walivyozodolewa Jakaya Kikwete,Zitto Kabwe na Edward Lowassa ambao sasa ni vipenzi vya upinzani.

Kesho ya upinzani bila maono ni mbaya sana.Hii ni sababu iliyowafanya Lazaro Nyarando alipohamia Chadema kuonekana shujaa lakini Mwita Waitara alipohamia ccm ni msaliti.Ni sababu ya Lowassa wa ccm kuonekana shetani lakini Lowassa wa Chadema ni malaika.

Noel Nguzo.R.
27/1/2019
 
Kudhihirisha hilo leo Chadema inamtumia Zitto wa ACT kuliko hata inavyowatumia wabunge wake kama Lema na Mnyika kusukuma mbele agenda za kisiasa za chama hiko
imemtumiaje ndg au na wewe umekumbwa na ile hali ya ya kushikiwa akili na chakubanga
 
Mwandiko wako umekaa kisiasa, naona umetuwekea na jina umesahau namba ya simu kwa ajili ya uteuzi
 
Anayetakiwa kujua kuwa si kila uchaguzi lazima ushinde si Chadema ni CCM, ni kweli Mkapa alimshinda Mrema? Kama ni hivyo kwanini matokeo ya awali yalifutwa kisha baada ya hapo uchaguzi ukaendelea kufanyika kwa wiki nzima kwenye maeneo tofauti? Mwaka 2001 kulitokea nini Zanzibar, CUF walipora ushindi? Huko Zanzibar uchaguzi uliopita matokeo yalifutwa eti kwa sababu baadhi ya wajumbe walivua mashati ukumbini!
Unapoamua kutetea kundi moja lazima ufikirie hoja za msingi za kundi lingine.
 
Back
Top Bottom