Ukiugua malaria utumie dawa gani?

MJINI CHAI

JF-Expert Member
Dec 12, 2010
2,198
1,226
Wana JF naomba kujuzwa Dawa ya Malaria kwa sasa ni ipi? maana kila dawa inaonekana haina nguvu, je tutumie Kwinini ambayo inaonekana inatibu Malaria? wasiwasi wangu naona kana ni dawa ya mwisho pale zinaposhindikanika dawa zingine, sasa tufanyeje? naomba Msaada wana JF
 
Onana na madaktari kwenye zahanati ama vituo vya afya! Watakushauri dawa sahihi ya kutumia.
 
huko kuna oroda na Mseto sijui wa nini?... dawa zimechakachuliwa na unatakiwa ulipie hata na vipimo mi nachanganyikiwa sijui nianze kunywa MWAROBAINI tatizo cjui Dozi yake maana ni chungu kweli...
 
Dawa Mseto (Artemisinin based combination therapies) ndo dawa zinazoshauliwa kutumika hata na wizara ya afya. Kama wewe hutaki basi nakushauri tafuta tiba za kichina. Jizoeze tabia ya kufuata ushauri wa wataalamu.
 
sawa mkuu......wataalamu katika zahanati zetu hizi wana yodo sanaaa nitawasikilizaga tu nipone
 
Dawa Mseto (Artemisinin based combination therapies) ndo dawa zinazoshauliwa kutumika hata na wizara ya afya. Kama wewe hutaki basi nakushauri tafuta tiba za kichina. Jizoezi tabia ya kufuata ushauri wa wataalamu.

Hili ni tatizo kubwa sana katika nchi yetu maana kila mtu anajua kila kitu.watu hatuheshimu utaalamu hata kidogo au sijui ni kwa sababu umechakachuliwa na wanasiasa.Tabu kweli kweli.
 
Jamaa analeta mauza uza hata kwenye afya yake! ni kazi sana kuelewesha mtu wa aina hii
 
mkuu c kwamba siwezi elewa ila naangalia na Mtu mwenyewe anetoa ushauri hasa akiwa amelewa pombe muda wote teh..teh..tehhhhhh
 
Mkuu sisi walevi huwa tuko makini sana kwenye fani zetu! Nadhani ulikuwa mdogo hebu fatilia habari za Prof Shaba wa Muhimbili. Alikuwa kama mimi full time yuko juu ila kazi ni balaaa! Unakunywa kinywaji gani? Beer, wine, rum ama whiskeys?
 
mkuu yule anayeshindaga pale Makumbusho ni Prof Shaba au Prof Fupi? na aliyekufa ni nani kati yao? na kuhusu swala la nakunywa kinywaji gani? mimi ni Non Alcoholic ila mnatulazimishaga nyinyi Madactor na madawa yenu mnayoweka pombe
 
Tumia mwarobaini!

wewe safi sanaaaaa, sasa Mkuu Dose yake ikoje? si unajua uchungu wake? nisije onekana nawanunia watu ninamopita kwa kukunja uso huku midomo imechongoka muda wote kwa uchungu wake
 
Dawa Mseto (Artemisinin based combination therapies) ndo dawa zinazoshauliwa kutumika hata na wizara ya afya. Kama wewe hutaki basi nakushauri tafuta tiba za kichina. Jizoeze tabia ya kufuata ushauri wa wataalamu.
Mkuu, Rev Masanilo,dawa si tatizo, tatizo lipo kwa wapimaji na wapimwaji pia. Wapimaji wengi wa nyakati hizi either hawamjui malaria parasite anaonekanaje(morphology) au hawamjui kabisa na hata parasitemia count hawajui pia. Mtu anapima anambiwa ana malaria 2, au 3 unampa dawa,tena second line treatment,this is ridiculous!

Unakula dawa, tena hiyo ya mseto na unamaliza dozi,ukipima, malaria ipo palepale na hapo kuna wengine walishatumia Artisunate lakini ukipima unaambiwa ipo.

Mpimwaji yeye kwake kila homa ni malaria tu,hajui kuwa kunaweza kuwepo tatizo jingine mbali ya malaria ndo maana watu wanakula dawa za malaria ovyo sababu ya kuamini kila homa ni malaria. Itatuchukua muda mrefu sana kuamini kuwa malaria imepungua sana kwa sasa sababu ya jitihada zilizofanyika kudhibiti.
 
Thanks mkuu NG'OTIMBEBEDZU for your good elaboration
 
Mtu unahitaji moyo wa ziada kuwaamini WATAALAMU wa Kitanzania. Wengi wao wamekaa kifisadi sana
 
Ni kweli Mkuu hasa vifaa vyao wanavyovitumia kucheck, nakumbuka zile Microscopy za shule ya Msingi miaka ile ya 1970 nazionaga kwenye hizi Laboratories sasa kweli huwa zinafanyiwa Calibrations hizi? au ndio bora liendeee
 
Wana JF naomba kujuzwa Dawa ya Malaria kwa sasa ni ipi? maana kila dawa inaonekana haina nguvu, je tutumie Kwinini ambayo inaonekana inatibu Malaria? wasiwasi wangu naona kana ni dawa ya mwisho pale zinaposhindikanika dawa zingine, sasa tufanyeje? naomba Msaada wana JF

kama unaumwa hapa utaongeza ugonjwa wazo tu kila mtu ATAKUJA NA YAKEBINAFSI NTAKWAMBIA KUNYWA MAJI YA ALOVERA UPO...SIJUI WA MSETOMCHANGANYIKO/METADIDY NA WENGINEO...POLE SANA WE KUNYWA UNAYOAMINI KUPONA NI IMANI TU KULE VIJIJINI AWAJUI MAMBO YENUYA METAKEVIN/DUKOTEXYIN NA NYINGINE WANAKUNYWA MTI MMOJA WANACEHEMSHA MAJANI NTAKUJULISHA JION STAY TUNED NAJARIBU KUUPANDA UNAKAUKA NATUMAINI UKIKUA NTAANZISHA HERBALIST YANGU
 
mkuu, rev masanilo,dawa si tatizo, tatizo lipo kwa wapimaji na wapimwaji pia. Wapimaji wengi wa nyakati hizi either hawamjui malaria parasite anaonekanaje(morphology) au hawamjui kabisa na hata parasitemia count hawajui pia. Mtu anapima anambiwa ana malaria 2, au 3 unampa dawa,tena second line treatment,this is ridiculous!

Unakula dawa, tena hiyo ya mseto na unamaliza dozi,ukipima, malaria ipo palepale na hapo kuna wengine walishatumia artisunate lakini ukipima unaambiwa ipo.

Mpimwaji yeye kwake kila homa ni malaria tu,hajui kuwa kunaweza kuwepo tatizo jingine mbali ya malaria ndo maana watu wanakula dawa za malaria ovyo sababu ya kuamini kila homa ni malaria. Itatuchukua muda mrefu sana kuamini kuwa malaria imepungua sana kwa sasa sababu ya jitihada zilizofanyika kudhibiti.

akikupima ukimwi huyu si takwambia una ukimwi loh m ndio maana nasema kupima uchochoroni loh..mmh
 
Back
Top Bottom