Ukitaka kuwa bilionea, kaa na mabilionea

mimiamadiwenani

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
5,411
7,016
Nakumbuka nilipotoka na nilipo, namshukuru Mungu sana kwa kunikutanisha na jamii tajiri na sahihi.

Achana na kichwa cha uzi, nimetumia neno bilionea kama mfano tu wa hoja yangu, haimaanishi mimi ni bilionea.

Sehemu yenye mchango mkubwa wa kukufanikisha au kukudumaza ni mkusanyiko wako wa ibada. Ni watu unaokusanyika nao kushiriki ibada.

Ukiona kanisani pako au msikitini pamejaa masikini tu wa hali moja kama wewe. Hapo una -20% za kufanikiwa. Hakutokuwa na wa kumuinua mwenzake kwani wote mna hali moja.

Kuna makanisa/misikiti unakuta kuna matajiri wanasali na wapo watu wa kawaida. Hapa una +60% za kufanikiwa, kwa sababu una access na mabilionea. Pia ni rahisi kufanikiwa kwa sababu unachangamana na mabilionea, wapo kwenye cycle yako. Ni faida na bahati kwako.

Binafsi ndipo nilipo mimi kwa sasa. Nashiriki ibada na mchanganyiko wa watu wa kila rangi unaowafahamu wewe duniani.

Ibada ni moja dunia nzima, utaratibu ni mmoja, mawaidha ya ibada ni mamoja, sare za ibada ni moja duniani kote. Ni kama jamii ya siri kwa 98%, kwa sababu huwezi kujileta tu from nowhere, ni lazima uwe directed na mwanachama.

Na unapoletwa kwenye jamii hii, HUTOJUA kama ndiyo unaingizwa, utakuja kujua mbeleni sana. Hii imewekwa kwa sababu maalumu. Hata mimi sikujua, ila nilipoingia na kugundua kuwa hii ndiyo ileee jamii, aisee nilijiona nina bahati sana.

Nikamuuliza director wangu kwa nini ulinificha? Akasema ilikuwa ni LAZIMA iwe hivyo.

Ya ndani yanabaki kuwa ni siri baina ya walio ndani TU, hayatakiwi kutoka nje. Maudhui ya ibada hayatakiwi kuonekana na yeyote wa NJE ambaye HAHUSIKI. NI MWIKO!!!

Binafsi nakutana na wenzangu wengi waliofanikiwa kama mimi, na wengine wanasaidiwa. Kwa kuwa kuna watu wengi wenye hadhi zao humu, I wish mbeleni nitafanikiwa zaidi na zaidi kwa sababu na deal na ku engage na watu mabilionea, watu wenye pesa kunizidi mimi.

Mambo ni mengi, naomba tu nihitimishe kwa kusema kuwa. Tafuta jamii na cycle yenye tija, ji attach nayo. Mafanikio yako yamebebwa na Mungu kupitia mikononi mwa watu.

Hujifunzi kuwa wengi wenye mafanikio wana cycles/jamii/mitandao yao? Huwezi kufanikiwa ukiwa huna mtandao, huna cycle upo upo tu. Never on earth.

Diamond, Alikiba, Mr Blue na wengine wote wenye mafanikio kwa Bongo Flava, wana cycles/mitandao yenye watu wenye tija iliyowafikisha hapo. Hujifunzi tu?

Jiulize sasa usiku huu, upo kwenye cycle yenye watu wa namna ipi? Unachangamana na watu gani kwenye ibada? Una mtandao gani?

Mungu anakupa utajiri/mafanikio baada ya wewe kuwa kwenye duara la watu sahihi. Hakupi tu from nowhere.
Rejea Daudi na wote uwajuao. Wote tayari walikuwa kwenye duara/mitandao sahihi.

Daudi alikuwa kwenye mtandao wa kifalme wa Sauli, Yonathani na wengine wengi. Hiyo tayari ilikuwa faida kubwa kwake.

Brotherhood! Brotherhood! Brotherhood!

Where are you attached?
 
Unatuaminisha kwa kutaja mara 3 brotherhood,mbona kama wewe ni mshetani mwenye vinasaba vya utapeli,umetega chambi uopoe vyura au samaki? Humpati mtu humu,this is the home of great thinkers.
 
Unatuaminisha kwa kutaja mara 3 brotherhood,mbona kama wewe ni mshetani mwenye vinasaba vya utapeli,umetega chambi uopoe vyura au samaki? Humpati mtu humu,this is the home of great thinkers.
Hapana ndugu, silo lengo langu kabisa. Sijawahi na sitowahi kufanya utapeli. Nimeongea kwa wale wanaojiweka peke yao peke yao halafu wanataka mafanikio makubwa, it's so hard.

Unaitafsiri vibaya maana ya brotherhood!
 
Nakumbuka nilipotoka na nilipo, namshukuru Mungu sana kwa kunikutanisha na jamii tajiri na sahihi.

Achana na kichwa cha uzi, nimetumia neno bilionea kama mfano tu wa hoja yangu, haimaanishi mimi ni bilionea.


Where are you attached?
Weka picha mkuu
 
Nakumbuka nilipotoka na nilipo, namshukuru Mungu sana kwa kunikutanisha na jamii tajiri na sahihi.

Achana na kichwa cha uzi, nimetumia neno bilionea kama mfano tu wa hoja yangu, haimaanishi mimi ni bilionea.

Niingizemo namm humo bas kaka
 
Haha
Screenshot_2024-02-08-19-02-53-821_com.mxtech.videoplayer.pro.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom