Ukitaka kugombana na mtu "serikali" dai haki yako

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
Hivi ni kwa nini nchi hii na hasa za kiafrika na kiarabu mwananchi au mfanyakazi anapodai haki yake hutishiwa au hufukuzwa? kwa mfano madaktari wa Muhimbili,walimu n.k na majibu yao ni yale yale TUNASHUGHURIKIA,TUPO KATIKA UPEMBUZI YAKINIFU,TUNATARAJIA KUWALIPA....................... Hivi wanajua hao wanawatumikisha wanaishije? wanakula wapi? kubwa zaidi mwisho wa siku wanakusanya kodi toka kwake na ushetani wao zaidi wanatumia kodi hiyo hiyo. KUNA VITU TUNAVIFANYA HATA SHETANI ANATUSHANGAA
 
Tena haki yenyewe kama ni Deni ndiyo kabisaaaaaa!! Acheni jamani yaliyowahi kunikuta! Ndiyo maana kuna kuwa na despute nyingi za Interest & Rights kwa nchi nyingi za kibongo, serikali imejaa vibaka na majambazi!
 
Tena haki yenyewe kama ni Deni ndiyo kabisaaaaaa!! Acheni jamani yaliyowahi kunikuta! Ndiyo maana kuna kuwa na despute nyingi za Interest & Rights kwa nchi nyingi za kibongo, serikali imejaa vibaka na majambazi!

Na wahuni!
 
Madaktari kufukuzwa ni meseji kwa waajiriwa wengine wote wa serikali kama walimu, polisi nk kwamba UTAKAPO DAI HAKI YAKO KWA MGOMO AMA MAANDAMANO JUA KUWA UTAFUKUZWA,
Why, because Serikali ina UKATA ILE MBAYA na Chama kinachoongoza kinapoteza umaarufu at every minute.
 
Kuingiza siasa kwenye mambo nyeti kama hayo ni kuweka rehani afya za watanzania!Hao wanasiasa wakiugua kidogo tu wanakimbizwa India kwa hela inayotokana na kodi zetu!Sasa hawa wanaojitahidi kuwahudumia hawa wavuja jasho ambao ndo walipa kodi wananyanyaswa kulipwa haki yao na wanapoidai kwa nguvu wananyanyaswa kwa nguvu zaidi!
My take: kuna haja wadau wote wa afya kuwapa support hawa vijana ili kutoiruhusu serikali kuendelea kudharau taaluma na wanataaluma na kukumbatia siasa na wanasiasa!
 
Back
Top Bottom