Ukistaajabu ya Escrow utaona ya Mwakyembe

Tina

JF-Expert Member
Jul 9, 2007
572
579
Ama kweli, ukistaajabu ya Musa, utaona ya Mwakyembe, haya hapa!Harrison Mwakyembe kwa kipindi cha miaka miwili na ushee hivi alikuwa Waziri wa Uchukuzi ambayo kwa hali yoyote ile ni sekta nyeti na muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa Taifa letu.

Katika kipindi hiki kifupi ambacho kwa wachambuzi wa masuala ya usafirishaji ilikuwa kama zaidi ya muongo mmoja,Mwakyembe alijidhihirisha rangi yake kamili kuwa ni mpiga porojo na fisadi mkubwa sana.

Hitimisho hili halitokani hata kidogo na chuki binafsi wala matarajio yoyote yale bali linatokana na matendo yake katika kipindi hiki ambacho alikitumia kufanikisha matakwa yake ya kifisadi kama mifano hai kwenye makala haya inavyodhihirisha.

Kama waziri wa uchukuzi, Mwakyembe alihakikisha anaweka wandani wake kusimamia mashirika yaliyoko chini ya Wizara ya Uchukuzi. Aliweka mtandao wake kuanzia bodi za wakurugenzi, menejimenti, viongozi wa wafanyakazi na hata wafanyakazi wa ngazi zote wakiwemo ndugu, rafiki na jamaa zake. Mwakyembe alikubuu kubuni miradi ya kisadi kila uchao. Heko wadau makini kwenye sekta ya usafirishaji kwa kutibua mipango yake mingi ya kifisadi.

Madudu ya Mwakyembe Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) hayakuwa na ukomo.-Mwakyembe alibuni mpango wake kamambe wa ufisadi TPA kwa kuvunja bodi ya Mzee Raphael Mollel na kuteua "vijana wa kazi" chini ya Joseph Msambichaka kama ambavyo alitamba mwanzoni.

Kwa kuamini matamshi ya Mwakyembe, baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo walioongozwa na John Ulanga walijizatiti kusimamia menejimenti ya TPA ipasavyo.

Azma ya kina Ulanga na wenzake ndani ya bodi iliwafanya kuchukua hatua stahiki dhidi ya Madeni Kipande ambaye Mwakyembe amemfanya Kaimu Mtendaji Mkuu TPA milele, kwa kumsimamisha kazi mnamo mwezi Agosti 2013.

Hata hivyo, uamuzi huu ulimfanya Mwakyembe apate kiwewe kwa kuwa Kipande alikuwa ni mshirika wake mkubwa katika pilikapilika zake za kuchota fedha bandarini, aidha moja kwa moja au kupitia miradi lukuki aliyokuwa akiibua kila uchao. Kwa hivyo Mwakyembe aliivunja bodi ya kina Ulanga na kuwandoa wajumbe wote wenye "kiherehere"na kumbakisha Msambichaka ambaye anamtetemekea Kipande.

Uvunjaji wa bodi ya "vijana wa Mwakyembe" ya TPA ilikuwa ni matumizi mabaya ya madaraka na ukosefu wa misingi ya utawala bora na haki. Bodi hii ya TPA Mwakyembealiiunda yeye mwenyewe, kwa kutoa sifa zisizohesabika kwa wajumbe hao, ambao baada ya muda mfupi tu, walifichua udhaifu wa mteule make, Madeni Kipande na kuamua kumg'oa, lakini Mwakyembe aliwabadilishia kibao, na kuwafukuza wajumbe wa bodi hiyo ambao walikuwa mstari wa mbele kupiga vita maovu ndani ya TPA.

Kwenye sekta ya usafirishaji, Mwakyembe alijulikana kama "Mwanasheria anayebaka sheria". Kwa mshangao wa wengi alidiriki hata kumteua mfanyakazi wa ngazi ya chini ambaye kazi yake ni mtunza mazingira (mfagia choo) Edmund Njowoka kama mjumbe wa bodi ya wakurugenzi TPA eti kwa kuwa alikuwa kiongozi wa DOWUTA, kwa lengo la kuwarubuni viongozi wa DOWUTA (chama cha wafanyakazi bandarini) wakae kimya.

Achilia mbali shule ya ngumbaru, sembuse Mwakyembe na PhD yake ya sheria, uteuzi huu ulikinzana na sheria iliyoanzisha TPA ya mwaka 2004 ambayo inakataza wajumbe wa bodi kuwa na "conflict of interest", lakini yeye Mwakyembe kwa kuwa anabaka sheria aliivunja sheria hii kwa makusudi ili kujinufaisha yeye binafsi.

Mwakyembe aliamua kutia pamba masikioni mwake na kufumbia macho UOZO wa kila aina uliofanywa pasipo kificho na Kaimu Mtendaji Mkuu TPA (Madeni Kipande) ambaye alimsimika hapo ili kulinda maslahi yake binafsi, kwa mkwara wake kwamba Kipande angekaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu TPA kwa wiki mbili tu, ambazo ziligeuzwa kuwa kukaimu nafasi hiyo milele. Mwakyembe aliamua kipindi chote cha uongozi wake kumlinda Kipande kwa kuwa alikuwa ni mshirika wake, katika ufisadi na uonevu wa kila aina.

UOZO wa kutisha ulifanywa na Kipande chini ya usimamizi wa karibu wa Mwakyembe ambaye aliufahamu kwa kina kwa kuwa ulikuwa ukiibuliwa na kufichuliwa na wakereketwa mbali mbali wa sekta ya bandari katika vyombo vingi vya habari, kwa kupitia majadiliano miongoni mwa wadau na yeye mwenyewe, malalamiko ya wateja na hata mitandaoni.

Ukiukwaji wa haki za kibinadamu na misingi ya utawala bora kutokana na matumizi mabaya ya madaraka na Kaimu Mtendaji Mkuu TPA-kwa kuuvuruga kwa makusudi na kinyemela muundo wa utumishi wa TPAna pia kutofuata kanuni za utumishi ili kuwapandisha vyeo wapiga debe wao bila kufuata seniority ni uozo uliofanyika ndani ya TPA. Uhamisho holela wa wafanyakazi mbali mbali, kutoka au kwenda Makao Makuu, bandari za mwambao na zile za maziwa bila kufuata muundo wa utumishi ulioidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi ulikithiri.

Lengo la uhamisho huu holela na ukiukaji wa muundo wa utumishi TPA ilikuwa ni kuwatilisha adabu na vile vile kuwakomoa wafanyakazi wasio na hatia kutokana na hisia potofu walizokuwa nazo Mwakyembe na Kipande kuwa baadhi ya wafanyakazi walikuwa wanampiga vita Kipande ili anyang'anywe nafasi hiyo, ambayo Mwakyembe kamfanya kukaimu milele (indefinitely). Pia wafanyakazi wengine walituhumiwa kuendelea kulinda maslahi ya Ephraim Mgawe, ambaye alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, kabla ya kuondolewa na Mwakyembe mnamo mwezi Agosti 2012, kwa tuhuma mbali mbali ikijumuisha kushindwa kuisimamia vyema TPA.

Mwakyembe aliwashangaza na kuwakasirisha wadau wa sekta ya usafirishaji ambao walishuhudia tuhuma dhidi ya menejimenti ya TPA iliyofukuzwa, kadri siku zilivyopita, ndivyo ilionekana kuwa ilionewa.--Miradi yote iliyobuniwa na menejimenti ya TPA iliyofukuzwa ndio hiyo hiyo Mwakyembe aliyejifanya CEO wa TPA na kibaraka wake Kipande walihangaika nayo bila kuweka mikakati mahsusi ya kiutekelezaji na hivyo kuishia kwenye karatasi. Mradi pekee uliokwenda vizuri ni mradi wa Jengo la Bandari ambao Mwakyembe na Kipande awali waliunyooshea kidole utawala uliopita kuwa ulitumia pesa za TPA vibaya kwa kuwekeza kwenye jengo.

Baada ya kubaini kuwa miradi ya utawala wa TPA uliopita ilikuwa na tija, Mwakyembe na Kipande waligeuka nyuzi 360̊ na kuona mradi wa jengo la bandari kama mkombozi katika "cargo clearance" kwa kuwa jengo hilo litatumika kama Kituo cha wadau wote, na hivyo kurahisisha na kuharakisha utoaji wa mizigo bandarini. Haya yalikuwa ni maono ya menejimenti ya TPA iliyofukuzwa na Mwakyembe. Lakini maono ya Mwakyembe na Kipande ilikuwa ni kujenga nyumba ya wageni ufukwe wa Matema, Kyela kwa maslahi binafsi ya Mwakyembe.

Watanzania wote tunakumbuka mradi wa bandari ya Bagamoyo ambayo hadi leo Mwakyembe hajafanya kitu. Na sio huo tu, bali hata uboreshaji wa usafiri wa treni nchini kote umeishia kuwa porojo na gumzo la vijiweni.

Treni ya mwendo wa kasi mwezi wa Desemba 2014 iko wapi?

Zipo taarifa, tena kwa maandishi kuhusuKipande kuwanyanyasa wafanyakazi wa ngazi zote, bila kukemewa na mtu yeyote. Kipande pia ni shujaa wamatumizi ya matusi ya nguoni kwa wateja, wadau na wafanyakazi bila simile, na tabia hii chafu iliwakera sana watu wengi, lakini Kipande alipeta tu, kwa vile Mwakyembe aliamua kumlinda.Dhuluma ya Kipande na Mwakyembe kwa wafanyakazi wa TPA ilisababisha vifo vya baadhi ya wafanyakazi.

Mwakyembe alihusika na ubadhirifu wa fedha za umma kwa kutumia rasilimali za TPA kwa manufaa yake binafsi na kuigeuza TPA shamba la bibi. Chini ya Mwakyembe tulishuhudia ubadhirifu wa kutisha kutokana na uibuaji wa miradi isiyo na tija kwa Taifa.

Taifa lilishuhudia kusuasua kwa mradi wa ujenzi wa gati 13 &14 ambayo mchakato wake kwa kutumia kampuni moja ya kichina uliwekwa rehani na Mwakyembe, baada yeye mwenyewe (Mwakyembe) na Kipande kuanza majadiliano ya kuhamisha mradi huu kinyemela kwenda kwa kampuni moja ya uhifadhi na uwakala wa mizigo yenye mizizi yake mjini Kinshasa. Mradi mwingine wa kifisadi ulikuwa ni wamfumo wa kukusanya taarifa za mizigo (ECTN)ambazo hata hivyo tayari zilikuwa zinapatikana bila hata malipo yoyote. Mfumo huu ambao ulipigwa marufuku na SUMATRA kwa jitihada za wadau wazalendo ili kulinda bandari ya Dar es Salaam, ulipigiwa debe sana na Mwakyembe ambaye aliweka shinikizo la kuweka mfumo huu batili bila mafanikio.

Lengo la Mwakyembe na Kipande ilikuwa watimize ndoto yao ya kujipatia mamilioni ya fedha kiulaini kupitia ECTN, zaidi ya dola za kimarekani milioni mia moja kwa mwaka. Hongera wadau wazalendo kwa kusimama kidete kuzuia ufisadi huu ambao ungelikuwa ni zaidi ya ESCROW!

Mwakembe-bila hata soni, walipanga na Kipande kupeleka mradi wa kituo cha mizigo kwenye kiwanja cha SUKITAambao ulipangiwa kutumia shilingi bilioni 10.0 huku ikifahamika wazi kuwa mradi huu usingelikuwa na manufaa yoyote kwa TPA.

Mwakyembe aliamuru mradi huu utekelezwe kwa maslahi binafsi ya Kipande na yeye mwenyewe kwa kisingizio kwamba ulikuwa ni mradi wa chama tawala, na walitumia sababu hiyo kuthibitisha uhalali wa mradi huu. Bila hata woga wowote, Mwakyembe na Kipande waliamrishaujenzi wa nyumba ya wagenijimboni kwa Mwakyembe, ufuko wa Matema kwa bajeti ya Sh. 500 milioni za TPA.

Mwakyembe pia alikuja na mkakati wa kifisadikugawana kiasi cha sh 800 milioni kama fidia ya mapatano nje ya mahakama-kati ya TPA na mkandarasi ambaye alishindwa kutimiza wajibu wake wa kujenga nyumba ya Meneja wa Bandari Tanga. Mkakati huu ulikuwa nikielelezo halisi cha ubadhirifu wa Mwakyembe wa fedha za umma kwa kutumia rasilimali za TPA kwa manufaa binafsi na kuigeuza TPA shamba la bibi.

Mwakyembe alikuwa kinara wa kutumia fedha za TPA kinyume cha sheria ili kugharamia matumizi ya Wizara ya Uchukuzi ikiwemo posho za safari, posho za vikao, takrima na kulipia tafrija binafsi za Mwakyembe nyumbani kwake na hotelini, n.k. Ukaguzi wa CAG uliibua hoja hii iliyowekwa kwenye ripoti yao.

Ni pigo kwa Mwakyembe kuondoka wizara ya uchukuzi kabla ya kukamilisha ukodishaji wa eneo lake kwa TPA lililopo Bahari Beach kwa kiasi cha dola za kimarekani elfu hamsini kwa mwezi ili litumike kama kituo cha wasafiri watakaotumia boti kati ya Dar na Bagamoyo.

Uozo mwingine ilikuwa ni ajira za upendeleo bila kujali muundo uliopokwa kuajiri familia, jamaa na marafiki wa Mwakyembe na Kipande pamoja na washirika wao pasipo kificho, hata kwa nafasi za kazi ngazi za juu.Dhamira ya Mwakyembe kujaza nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA kwa uswahiba bila kufuata taratibu za ushindani ilifahamika baada ya Mwakyembe kusitisha usaili wa nafasi hiyo iliyotangazwa kwenye magazeti ili ijazwe kiushindani.

Maoni ya Mhariri wa Gazeti la Majira tarehe-5 Januari 2014 kwa kutoa wito kwa Serikali kuingilia kati kituko cha ajira za wapambe wa Mwakyembe hasa Kipande kama ilivyoidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya TPA na kutangazwa kwenye vyombo vya habari kuwa usaili wa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu TPA ulisitishwa kwa mwaka mmoja, ili Mwakyembe na mwandani wake Kipande waendelee kufanya madudu kadri watakavyo, ilikuwa na dhamira ya kuendeleza UOZO, ambao Serikali haikupashwa kufumbia macho hadi tarehe24 Januari, 2015, hasa katika Taasisi ya ummakubwa na muhimu kwa maendeleo ya Taifa kama TPA.

Umma wa Watanzania ulishuhudia Mwakyembe akiukingia kifua utendaji mbovu na uongozi dhaifu wa Kipande ambao ulijitokeza katika kipindi chote tangu aliposimikwa hadi leo hii. Ajabu na kweli, kigezo pekee kilichomwezesha Kipande kuendelea kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA imekuwa ni uswahiba wake na Mwakyembe.

Umma wa Watanzania umechoshwa na UOZO huu na ni vyema wananchi wenye sifa ambao walioomba nafasi ya Mkurugenzi Mkuu TPA wakatahiniwa na Tume ya Ajira au chombo chochote huru kwa kutumia vigezo mahsusi, ili kumpata kiongozi mahiri wa kuitoa TPA hapo ilipo na kwenda mbele zaidi. Mwakyembe alichakachua hadi taarifa za mapato ya TPA kwa kuwatangazia uongo wananchi kuwa TPA tangu alipoteuliwa uwaziri ilianza kukusanya mapato ya shilingi bilioni 50 kwa mwezi, huku Mwakyembe alifahamu fika kuwa kiwango hiki hakikuwahi kufikiwa na TPA.

Ili kutimiza ufisadi wake ndani ya TPA, Mwakyembe alishabikia marupurupu yasiyo na mipaka wala tija kulipwa kwa viongozi wa DOWUTA ambacho ni chama cha wafanyakazi Bandarini kama njia ya kutafuta uungwaji mkono na wafanyakazi hao na pia kuwafunga midomo viongozi wa DOWUTA ili wasiseme ukweli kuhusu UOZO huu waliokuwa wakifanya yeye Mwakyembe na Kipande.

Marupurupu hayo ilikuwa ni pamoja na posho za kujikimu kutokana na ziara katika bandari kadri DOWUTA walivyotaka, posho za kujikimu na za vikao kwa kufanya mikutano mbali mbali ali mradi DOWUTA wanataka kukutana popote pale na pia uteuzi wa mjumbe wa DOWUTA kwenye Bodi kwa kuvunja sheria iliyoanzisha TPA.

Mwakyembe alijigeuza kuwa Mtendaji Mkuu (CEO) wa mashirika ya umma yaliyokuwa chini yake. Ili kumlinda Kipande na kuficha UOZO kibao ambao umeota mizizi ndani ya TPA kwa ajili yake, Mwakyembe alijigeuza na kufanya kazi kama Mtendaji Mkuu wa TPA, na dhana hii haikuwa sahihi.

Mwakyembe badala ya kusimamia sera katika Wizara ya Uchukuzi alijigeuza kuwa Mtendaji Mkuu (Chief Executive Officer) wa TPA kwa kusimamia kazi za kila siku ndani ya TPA hasa bandari ya DSM. Mwakyembe alikubuu kwa kutoa maagizo moja kwa moja bila kupitia kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, na vile vile bila hata ya kushauriana na Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi. Mwakyembe alikiuka misingi hii iliyowekwa kwa ajili ya utawala bora na uwazi kwa sababu moja tu, ambayo ni kuhakikisha kuwa analinda maslahi yake binafsi huku akijificha kwa kutumia dhana ya"waziri jembe". Ukweli Mwakyembe aligeuka na kuwa "waziri pembe" na kutumia pembe zake hizo kuchoma na kuumiza watu, tena kwa hisia tu, kwamba labda walikuwa wanaingilia kati maslahi yake binafsi na kuyachelewesha au kuyatibua.

Mwakyembe wakati wote, alishinikiza maamuzi ya utata na utekelezaji wa miradi ya kifisadi kwa kutumia menejimenti na Bodi za Wakurugenzi, hususan bodi ya TPA na Kipande ambaye alimpachika kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu TPA milele, ili wajichotee fedha za TPA na kuigeuza shamba la bibi, na hatimaye wale hadi wavimbiwe.

Watu makini walishauri kinagaubaga kuwa bora kubaki na "mawaziri mizigo" kwa kuwa kama watendaji chini yao wanafanya kazi vizuri, mambo yatakwenda tu, kuliko mawaziri wala rushwa wanaokiuka misingi ya haki za binadamu na utawala bora ili kujineemesha kama Mwakyembe alivyo.

Mwakyembe aliwahi kumtaka Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Edward Lowasa apime kuhusu sakata la Richmond, ambayo kwa Watanzania wengi ni bora hiyo Richmond kwa kuwa mitambo ya umeme ilionekana, kuliko ufisadi huu wa Mwakyembe ambaye alishinikiza kuwafukuza Wachina ili wasijenge gati 13 & 14, na badala yake kuileta kampuni ya kibelgiji iliyojiimarisha Kinshasa katika nyanja ya uhifadhi na uwakala wa mizigo, kwa lengo la kupora ardhi ya TPA kinyemela hapo Gerezani Creek, ili apate sio tu kitu kidogo, bali mkato wa kudumu na kumwezesha kupata URAIS! Iwapo Wachina wangelishindwa kujenga gati hizi, basi zabuni ingelibidi kutangazwa ili kupata thamani ya pesa za walipa kodi wa nchi hii, na sio kuchagua kampuni ya wabelgiji kwa maslahi binafsi ya Mwakyembe.

Mwakyembe alichafua "hali ya hewa" ndani ya Wizara ya Uchukuzi ambayo kwa muda mrefu haikuwa shwari. Ilibainika kuwa kutokana na ufisadi wa Mwakyembe, hali ndani ya Wizara ya Uchukuzi haikuwa shwari kwa kuwa mahusiano ya kazi kati ya Waziri Mwakyembe na Naibu wake Mh. Dkt. Charles Tizeba, na pia kati yake na Katibu Mkuu wa Wizara ya hiyo, Dkt Shaaban Mwinjaka hayakuwa mazuri. Viongozi hawa wa juu wa Wizara ya Uchukuzi walimshutukia Mwakyembe kwa kuwa aliwaweka kando, na kujifanya Mtendaji Mkuu (CEO) wa mashirika kama vile TPA, TAA, n.k, kwa kuwa taasisi hizi zinao uwezo wa kifedha na pia aliweka maswahiba wake kuziongoza ili kumwezesha kufanya atakalo kwa maslahi yake binafsi.
 
Na mie nataka kujua kwanini leo? au ulinyimwa mgawo? ukadhani hatakuwa waziri tena akiachishwa alipokuwepo?

au ulishindwa kuiba au wa karibu yako hakukupa vya wizi now huyooooooo.
 
SIYO TPA tu mkuu ambako Mwakyembe amekuwa akifanya ufisadi. Mwakyembe amekuwa akiwatumia ndugu na jamaa zake kuchota pesa sehemu nyingi za taasisi zilizo chini ya wizara ya uchukuzi. Kuna ndugu yake pale Wizarani anaitwa Tumpe Mwaijande, Huyu mama ni Director wa Maritime safety and security.

Mwakyembe amekuwa akimtumia huyu mama kukamilisha ufisadi wake. Huyu Mama ni mpuuzi tu. Miaka ya 2003, huyu mama alikuwa na scandal ya kuuza vyeti vya mabaharia pale wizarani. Lakini Baada ya Mwakyembe kuingia pale alimpandisha cheo huyu mama fisadi kwa sababu tu wanatoka sehemu moja. Hiyo ya hali ya hewa kuchafuka pale wizari ni kweli kabisa mkuu, Huyu MWAKYMBE alikuwa hashirikiana na watendaji waaandamizi wenzake.

Alijifanya yeye anajua sana, kumbe ilikuwa ni mbinu yake ya kuficha ufisadi wake. Kuna tetesi kuwa Naibu waziri wa Uchukuzi alitembelea moja ya taasisi za wizara hiyo, baada ya kuambiwa kero na changamoto zilizokuwa zikiwakabiri wafanyakazi wa taasisi hiyo ya umma, Dk. Tizeba aliahidi kuzitafutia kero ufumbuzi kero hizo. Lakini cha kushangaza mwakyembe aliivyopata taarifa ya ziara ya Tizeba kwenye taasisi hiyo, Mwakymbe alitoa maneno ya Kejeli kwa Dk. Tizeba akisema yeye ndo waziri, Dk. Tizeba hana uwezo wa kuwatatulia wafanyakazi kero zao. "Hayo aliyoahidi alikuwa akifurahisha nafsi yake". Na kweli hakuna chochote kilichofanyika kwenye taasisi hiyo.

Mwakyembe Fisadi tu. Ila alikuwa akitumia media ili aonekane anafanyakazi, Lakini ukweli uliopo ni kwamba TPA, TAA, SUMATRA amekuwa akijichotea pesa. Alioondosha uongozi wa taasisi hizi na kuweka watu wake ili kufanikisha ufisadi wake: Huyu nifisadi anayepaswa kuchunguzwa.
 
HAKUNA KITU HAPA, NI POROJO, CHUKI, INDA, HADITHI ZA KUSADIKIKA ZA MAMLUKI WANAOLIPWA NA MAFISADI ALIOWATIMUA MWAKYEMBE. NILIISHAUSOMA UJINGA HUU KWENYE GAZETI LA BALILE ANAYETETEA BULA AIBU WAHAYA WENZAKE WAWILI WALIOWEKWA PEMBENI NA UONGOZI WA TPA.

MAPUNGUFU YA FACTS NI KIBAO:
- Mradi wa Bandari na EPZ Bagamoyo uko chini ya usimamizi wa PMO, siyo Mwakyembe!
- Mwakyembe alizuia mradi wa Gati na 13&14 kutokana na gharama kubwa za kifisadi za ujenzi (dola milioni 523 badala ya dola 200 au 250 tu!)
- Mradi wa nyumba ya wageni jimboni kwa Mwakyembe ni hadithi/porojo za Balile & Haya Co. Ltd
- hakuna taarifa yoyote ya CAG kuhusu Mwakyembe. Kama zipo mpelekeni Mahakamani
- chini ya KIPANDE TPA imefikia malengo ya ufanisi na kupata HATI SAFI kila mwaka!
- Mwakyembe ni Waziri wa kwanza wa Uchukuzi kupewa tuzo na heshima ya HONORARY INTERNATIONAL AMBASSADOR wa CHARTERED INSTITUTE OF LOGISTICS & TRANSPORT ya Uingereza mwaka 2013 kwa uchapakazi sekta ya Uchukuzi. Mwakyembe ni Balozi wa Nne kuteuliwa duniani.

Mwenye wivu, nongwa ajinyonge tu but facts will remain facts!
 
Yani nime soomaweeeeeeee, hadi nilipo choka na kushindwa kumaliza kuisoma taarifayako sijaona point hata moja, nitasoma comments za wengine labda watanisaidia kuelewa kitu.


Mi naona Mwakyembe Mwakyembe tu mwanzo mwisho, si ungeyasema siku zote km yalikukaba...
Wengi wamelichoka hili chama
 
Asante Ijabu kwa ufafanuzi, maana mkeka huu ulivyoandikwa ni msururu wa lawama tu zisizo na ushahidi. Ndo maana wengine tumepunguza sana interest hapa kitokana na porojo za kisiasa na uchimvi tu. Mwakyembe kafanyakazi Bwana! Amefufua sekta iloyokuwa ICU! Amekomesha wizi bandarini! Semeni na hayo basi!
 
Tina mission yake kuu yeye ilikuwa ni mwakyembe. yaaan alikuwa hali halali ana deal na mwakyembe huyu dada yangu. mwakyembe alimshika pabaya sana kwa kweli, sasa mama utapumua nasi tutapumua. Maana ilikuwa shida.

Kila siku ni kuhusu mwakyembe, ukiwa sebulen unamwaza mwakyembe, ukiwa msalani mwakyembe, ukiwa room mwakyembe, ukiwa kitandani mwakyembe. ndo maana mpaka umepungua sana uzito.

Pole mama ndo maisha. Sasa amekuja sitta huyu ni mshkaji tu so wala usiwe na shaka.sasa watu mtapiga pesa na kusafirisha madawa kwa sana maana mwakyembe naye alikuwa anajifanya kukaza kiaina. Sasa dada relax tu. Sawa? Tumeshasoma sana about Mwakyembe, hebu mfanyie kazi mwingine sasa. Unaonaje ukimchagua mtu kama Wassira au Anne Kilango ukamfanyia thesis?
 
Last edited by a moderator:
Acheni chuki za kijinga nyie! hakuna mtanzania asiyejua uchapakazi wa mwakyembe, inaonyesha mleta hoja una chuki binafsi

Mwizi! Mijizi yote ya bandari iliyofukuzwa au kuondolewa kwenye vitengo nyeti inaweweseka!
Wameiba mno TPA hasa idara ya uhasibu mpk mfagizi ana gorofa!
 
Back
Top Bottom