Ukipewa namba na mwanamke wa JF kuwa makini sana, ukizubaa unaliwa

Kwema wana Jf.

Leo sina maneno mengi ila nipo hapa kuwahasa mabaharia wenzangu kuwa wanawake wengi wa Jf ni butu sana na wanapiga mizinga vibaya mno.

Ndugu ukitongoza mwanamke wa Jf anakuvuta taratibu na akiona kama umeshaiva mithili ya nyama choma utasikia nashida ya shilingi 3000, 5000, 7000 au shilingi 10000 umsaidie anakurudishia muda siyo mrefu.

Ewe mwanaume ukijichanganya hakuna rangi utaacha kuona na hakuna mziki utapigwa uache kuucheza.

Tahadhari wale penda penda kama mimi na wale baharia wenzangu tusiochagua mahali pakuogelea nawaombeni sana muwe makini mno.

Wanawake wa Jf hizi salamu pia ziwafikie na muache kutuona wajinga na PM hatutaacha kuja ila mjue wazi kabisa tuna akili na sasa hivi hakuna mwanaume mjinga mjinga wote tumekua wajanja sana.

Hiyo mbinu yenu ya kujifanya mnatupenda na kutujali tumeijua .
Yamekukuta nini 😆
 
Inategemea na wewe mtumiaji wa huu mtandao. Kama unaitumia JF kutafuta wanawake lazima ukutane na hao matapeli, maana wengi ndio wamejazana humu kwa kukosa shughuli za kufanya hivo wengi wao wana maisha magumu.

Sidhani kama kuna mtu humu jf ambaye hana muda na kujadili mambo ya wanawake na kutongoza hovyo akasumbuliwa kwenye pm yake unless labda huyo mwanamke wakuja pm awe na shida au msaada wa mawazo ama ushauri na sio kuomba pesa
 
Back
Top Bottom