Ukiombwa pesa ya soda unatoa shilingi ngapi?

Juzi nilikua zangu nmekaa sehemu nakula rost ya kitimoto na Red Wine , wakati naendelea kula pale ghafla akatokea dada mmoja ambae ni jirani yangu lakini hatuna mazoea kivile, nikamsalimia akaitika, nikamkaribisha aje kula (Kama mnavyojua wabongo unamkaribisha tuu mtu kimazoea mda mwingine hatumaanishi)

Akavuta kiti akakaa, nashangaa anamuita muhudumu "Muuudumu niletee Glass na tishuuu! "nikashangaa sana, Wine yangu nilitaka ninywe mwenyewe sasa imepata muhuni tunaipiga mande!, nikasema sio tabu, Glass ikaletwa tukawa tunakunywa huku tunapiga story.

Kiukweli Dada aliniboa sana, ananiletea story nyingi, mara aniambie "hapa kuna vyumba ujuee"

Kiukweli mimi sipendi mtu aniongeleshe sana hua nasikia kama kichwa kinauma.

Nilimaliza kula, nikapiga glass moja ya mwisho, nikanawa, nikamuita muhudumu nikalipa bili, nikamuaga yule dada nikamuacha na chupa ya wine pale anywe.

Nashangaa naondoka ananishika mkono eti anataka nimuachie hata ya soda, nikasema sio shida, kwakua nilikua na chenchi nikampa 500 ya Coin akanywe hiyo soda, alitoa macho kama kapigwa shoti, kwa mawazo yake sijui alijua nitampa shingapi.

Mambo mengine bana.
dah!haukumbuka uzi wa Riki boy mkuu?
 
Binafsi hela ya Soda inaanzia Tsh 5000. Ila kama ni mtoto wa kike na ana viwango nnavyotaka naweza mpa 15000 mpaka 30000
 
tembo wa3 tu
Kama hivi eeh??
20200519_164333.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom