Ukioa mke asiyetaka kwenda kwenu

I AM WHO I AM

Member
Oct 18, 2012
49
35
Helo wandugu. Ninaomba ushauri.
Nimeoa na mke wangu ni wa Pwani. Tumepata mtoto ila huyu mwanamke hataki nimpeleke mwanangu kwetu.
Niko Mkoa mwingine kikazi. Huko kwetu nimejenga na nina nyumba yangu. Mama anahitaji walau akae na mjukuu wake siku 3.
Mke hataki. Wala hawazi nikifa Leo nitapelekwa kwangu.
Infact hana mawasiliano mazuri hata kumjulia mama yangu hali.
Hii imenifanya nikate mawasiliano na kwao. Kwani alikua ikipita wiki anadai mama yake analalamika simsalimii.
Mama yangu Mimi kwake ni mtoto pekee. Alitumai kupata mwali atakae mpenda. Sasa analalamika tu.
Kuna haja ya kua na mke wa kikijini na mjini?
 
Wewe ni mwanaume au mtoto wa kiume?

Naomba unijibu hili swali kwanza....
 
Huyo ni mkeo au mke wa mwingine?!
BE A MAN, mambo mengine sio lazima ushauliwe,unajiongeza tu!
 
Kaka mtihani unao ila tumia wanaume wako hakuna faida ya kukaa na mtu asie penda kuona ndugu zako mtoto wako ni damu yako. Mama yako anahaki ya kumuona mwanao kama hataki angalia usiwe umeuziwa mbuzi kwenye gunia cha msingi mlazimishe kama mwanaume mpaka akubali kama hataki kata kata chukua maamuzi magumu. Matatizo kama haya hutokea sana mara nyingi unapo oa mkoani mara nyingi huwa hawataki hata kwenda kasalimia wazazi wako ikitokea amekukalia kichwani unaweza kufa wanao hawa wafahamu ndugu zako
 
Msingi unapokuwa mbovu kumbuka nyumba itakaposimama lazima iporomoke
 
Kosea kujenga lakini sio kuoa.

Vijana ambao bado hamjaoa Ombeni Mungu sana Mpate wake Wema wasikua na makuu.

Ndugu mleta hoja unaweza kumuweka kikao na msimamizi/wasimamizi wa ndoa ili kuinusuru ndoa yenu.Maana ukisema umpe talaka unaweza kupata mjeuri zaidi ya huyo.

Zungumza na Mwenzako.
 
Kuna jamaa yangu unamsema humu kiaina..!
Hadi namhurumia wakati mwingine..!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom