Ukimya wa Lowassa kuzungumzia rushwa katika chaguzi za CCM -- kulikoni?

Jamani hii haikai sawa hasa kwa huyu mjamaa (EL) ambaye anadaiwa kuutaka urais kwa udi na uvumba, na anayeripotiwa yuko katika mkakakti kabambe wa kupanga safu yake katika chama chake kujihakikishia uteuzi wa kugombea kwenda Ikulu mwaka 2015.

Rushwa katika chaguzi zinazoendelea katika CCM si suala la siri tena -- liko nje nje kabisa. Takriban vyombo vyote vya habari hususan magazeti vimekuwa vikiripoti rushwa ikitembea katika chaguzui hizo, tena mara nyingine waziwazi.

Isitoshe hata mwenyekiti wa chama hicho (JK) amelizungumzia suala hilo kwa masikitiko makubwa.

Lakini kwa nini huyu mgombea mtarajiwa (EL) hata siku moja hatujamsikia akizungumzia rushwa kama ni kitu kinachomkera? kulikoni?

Naomba majibu jamani, na msianze kuzungusha zungusha (spinning) katika swali hili ambalo ni simpo kabisa,

Nawasilisha.

........... Hakuna cha ajabu kujipanga ni kujipanga tu.... Mh. EL anajipanga kama kuna anayeweza ajaribu kupangua..... si muda bado upo!
 
Lowassa aongee nini wakati karibu rushwa yote inatoka kwake? Ulitegemea kweli nguruwe ausifie uturi wakati yake kinyaa? Lowassa haoni kama kilichofanyika ni jinai na rushwa kwa vile yeye na genge lake ndiyo wanufaika. Ahongea hao CCM wenzake lakini hatahonga watanzania wote. Hata akifanya hivyo akiingia kwenye kinyang'anyiro kama mgombea wa CCM nitapenda sana.Hii itakukwa ni fursa ya aina yake kwa upinzani kuchukua nchi kirahisi ingawa nasikia wana mpango wa kumuengua kwa kuchagua mwanamke. Tuombe Lowassa aendelee kampeni zake ili tummwange mambo kwenye uchaguzi.
 
"(EL) ambaye anadaiwa kuutaka urais kwa udi na uvumba," Atazungumziaje, wakati mwenye umekiri kwamba anautaka kwa udi na uvumba?

Uwanja ni wa CCM kama kuingia ikulu ni kwa manemane, udi na uvumba.

Mungu atusaidie...si akagombee urais wa TFF tuu.
 
........... Hakuna cha ajabu kujipanga ni kujipanga tu.... Mh. EL anajipanga kama kuna anayeweza ajaribu kupangua..... si muda bado upo!

last week kwenye kipindi cha hamza kasongo hrs alikuwepo mkama moja ya maneno aliosema ni hatari sana kujionesha mapema kwamba unataka kugombea nafasi kubwa kwani unawapa maadui nafasi kubwa ya kukupinga
 
Humu ndani kuna watu wanatutafutia BAN yaani wanamshika Kondoo mkia wake na kutuuliza hivi huyu Kondoo anany... wapi mbona tundu lake halionekani? mmemsingizia kabisa Kondoo kuwa na mkia mkubwa ni kumuonea wivu
Hata mtoto mdogo wa miaka 14 leo anajua nani ni fisadi na ifikapo 2015 atapiga kura wapi?
BORA KULIPIGIA JIWE KURA YANGU maana naona hata Baba & Mama Mwanaasha na Ritz 1 wameshamnywea kawavuruga kuanzia UWT UVCCM sijui km atawaacha ktk Wazazi na wakifanya mchezo hata kwenye Kiti cha mwisho atawang'oa
Du hapa jamaa yangu achague moja agangamale kiume au kimfie mkonono EL hana mchezo
 
hivi mnajua hata issue ya ajira kwa vijana AMEIPORA KUTOKA KWA SUMAYE??? kwa wale wenye kumbukumbu wanajua hili sio mashabiki
 
Umeuliza swali ambalo jibu lake linafahamika directly! EL ana ukwasi mkubwa sana! ni Expert wa mbinu chafu hasa rushwa! ndiye aliyemuweka JK madarakani.
 
Jamani hii haikai sawa hasa kwa huyu mjamaa (EL) ambaye anadaiwa kuutaka urais kwa udi na uvumba, na anayeripotiwa yuko katika mkakakti kabambe wa kupanga safu yake katika chama chake kujihakikishia uteuzi wa kugombea kwenda Ikulu mwaka 2015.

Rushwa katika chaguzi zinazoendelea katika CCM si suala la siri tena -- liko nje nje kabisa. Takriban vyombo vyote vya habari hususan magazeti vimekuwa vikiripoti rushwa ikitembea katika chaguzui hizo, tena mara nyingine waziwazi.

Isitoshe hata mwenyekiti wa chama hicho (JK) amelizungumzia suala hilo kwa masikitiko makubwa.

Lakini kwa nini huyu mgombea mtarajiwa (EL) hata siku moja hatujamsikia akizungumzia rushwa kama ni kitu kinachomkera? kulikoni?kama ni simple jibumwenyewe sisi tunajibu maswali magumu na kufanya maamuzi magumu.

Naomba majibu jamani, na msianze kuzungusha zungusha (spinning) katika swali hili ambalo ni simpo kabisa,

Nawasilisha.

kama ni simple jibu mwenyewe sisi tunajibu maswali magumu na kufanya maamuzi magumu.
 
kwanini mtu atake uraisi kwa nguvu nyingi ivo...tena mpaka kotoa takrima kwa kiasi kikubwa na kuweka rekodi mpya ya utoaji rushwa...hyu mtu sidhani kama ana nia ya kuwatumikia wananchi, bali ana ajenda za siri na hatari sana hyu mtu...
 
Umeuliza swali ambalo jibu lake linafahamika directly! EL ana ukwasi mkubwa sana! ni Expert wa mbinu chafu hasa rushwa! ndiye aliyemuweka JK madarakani.

Ni sahihi kwa EL kukaa kimya maana hana uhalali wowote wa kukemea rushwa. Yeye ndo kinara wa ruhwa ndani ya Chama Cha Magamba.
 
Msifanye mchezo na biashara ya mafuta na gesi. Mnawajua wanaomchangia gizani na anaopanga nao mikakati? Mnamjua yule jamaa wa Buzwagi, unamjua yule jamaa wa igunga, unamjua jamaa wa bariadi. Hao ndio wanaocheza picha hii kwa ushirikiano. Pinda alisema watu hawa ni hatari na mkiwaendea ovyo wanaweza kuyumbisha uchumi wa nchi. Mlidhani anatania! Tushukuru uwepo wa Dr. Slaa. Najua anacheka na kufurahi akiona washindani anaoletewa anawajua nje ndani. Nadhani dr anazidi kuomba wala rushwa wapite ccm ili awababue jukwaani. WATAAIBIKA
 
Tatizo la wana JF wengi ni kuandika mambo mengi kwa kuongozwa na hisia, chuki binafsi na unafiki badala ya kufanya utafiti na kuwa na ushahidi hasa linapokuja suala linalomhusu Lowassa. Hivi kama mna ushahidi na tuhuma za Lowassa kuwa ni fisadi na mtoa rushwa mkubwa je ni kipi hasa kilichosababisha msiupeleke huo ushahidi wenu mahakamani?. Je hakuna vyombo vya kupambana na rushwa na ufisadi nchini vya kumkamata na kumhoji?. Kama hayo yote hayawezekani basi Lowassa ni "mtakatifu" na anastahili kuingia ikulu 2015. No research no right to speak.

we umezaliwa na umekulia nchi gani? eti mahakama na vyombo vya kisheria...kama hautoki kwenye ukoo wa lowassa basi una matatizo ya kufikiri sawa swa bila uvivu.
 
Lowassa aongee nini wakati karibu rushwa yote inatoka kwake? Ulitegemea kweli nguruwe ausifie uturi wakati yake kinyaa? Lowassa haoni kama kilichofanyika ni jinai na rushwa kwa vile yeye na genge lake ndiyo wanufaika. Ahongea hao CCM wenzake lakini hatahonga watanzania wote. Hata akifanya hivyo akiingia kwenye kinyang'anyiro kama mgombea wa CCM nitapenda sana.Hii itakukwa ni fursa ya aina yake kwa upinzani kuchukua nchi kirahisi ingawa nasikia wana mpango wa kumuengua kwa kuchagua mwanamke. Tuombe Lowassa aendelee kampeni zake ili tummwange mambo kwenye uchaguzi.

Huyu jamaa ni political and business mafia amehonga hadi CDM )umeshasikia Mbowe au SLaa anamsema?) ZZk ni kijana wake mtiifu. akipita ccm hamna wa kumzuia sana sana atawapa uwaziri akina zzk, mbowe na slaa kama ishara ya utaifa
 
:A S soccer:Hakuna cha kushangaza kwanini lowasa kakaa kimya ni kwa sasababu hicho chama nikawaida tu kutumia rushwa kwenye cha guzi zake nijambo la kawaida kabisa yupo sawa tu kukaa kimya.
 
Anahusika vipi? Mbona yeye tulikuwa naye hapa mnazi mmoja kwenye vikoba, rushwa imetolewa huko Dom. Where is connection between suspects and EL?
 
Jamani hii haikai sawa hasa kwa huyu mjamaa (EL) ambaye anadaiwa kuutaka urais kwa udi na uvumba, na anayeripotiwa yuko katika mkakakti kabambe wa kupanga safu yake katika chama chake kujihakikishia uteuzi wa kugombea kwenda Ikulu mwaka 2015.

Rushwa katika chaguzi zinazoendelea katika CCM si suala la siri tena -- liko nje nje kabisa. Takriban vyombo vyote vya habari hususan magazeti vimekuwa vikiripoti rushwa ikitembea katika chaguzui hizo, tena mara nyingine waziwazi.

Isitoshe hata mwenyekiti wa chama hicho (JK) amelizungumzia suala hilo kwa masikitiko makubwa.

Lakini kwa nini huyu mgombea mtarajiwa (EL) hata siku moja hatujamsikia akizungumzia rushwa kama ni kitu kinachomkera? kulikoni?

Naomba majibu jamani, na msianze kuzungusha zungusha (spinning) katika swali hili ambalo ni simpo kabisa,

Nawasilisha.

Nakala: -PASCO,
SLP 2015,

-RITZ
 
Back
Top Bottom