Ukikutana na abiria anachungulia unachofanya kwenye simu yako bila ridhaa yako unafanyaje?

Je ukipigiwa Simu Kwenye daladala utafanyaje ili watu wasisikie unachoongea?
Macho hayana pazia haiwezekani ufanye kitu Kwenye public halafu watu wakikiangalia ukasirike
Yaani mfano we mdada anatembea barabarani uchochoroni abanwe na mkojo aamue kukojoa sehemu ya wazi niangalie pembeni wakati anakojoa nisimuangalie, namuangalia vizuri sana
 
Dah! Hii ilinikuta juzi aisee... Nimepanda basi natoka Tabora nipo na Tablet naperuz zangu Twitter huko. Kumbe jamaa anashuka na post zangu moja baada ya nyingine uzalendo ukamshinda kwenye post ya kikosi cha Simba akaniambia emh rudisha hapo sijamaliza
 
Naweka camera ya mbele tuonane vizuri
Umenikumbusha kituko kimoja niko kwenye basi Kilimanjaro nikiwa natoka Arusha pembeni yangu alikaa mdada ambaye alipandia Mianzini. Ni mweupe sura anayo sana sema shape amenyimwa. Muda mwingi wa safari nilikuwa na chatt huyo mdada alikuwa kama spy kwangu akiona tu ninachatt anaanza kuchungulia. Baadaye nikaona kama ananibore vile. Sijui nilipata wapi wazo la kumpiga picha. Ikawa kila akichungulia anakutana na camera inamchukua picha... Baadaye alisonya na hakurudia tena kuchungulia.
 
Huu Uzi ukipata watu wa kushare visa vyao vya hasara na faida za kujianika wakati ukijua upo katika hadhara ya wazi utatembea mpaka mwisho wa Dunia na bado Uzi utabaki ukiendelea
 
Baadhi ya abiria wamekuwa na tabia hii ya kuchungulia kinachoendelea kwenye simu za majirani zao wanapokuwa kwenye usafiri wa umma bila kujali hawapaswi kufanya hivyo.

Ukikutana na abiria kama huyu akiwa anachungulia unachofanya kwenye simu yako bila ridhaa yako unafanyaje?
Unamchoma moto kama lile basi la sai baba
 
Dah! Hii ilinikuta juzi aisee... Nimepanda basi natoka Tabora nipo na Tablet naperuz zangu Twitter huko. Kumbe jamaa anashuka na post zangu moja baada ya nyingine uzalendo ukamshinda kwenye post ya kikosi cha Simba akaniambia emh rudisha hapo sijamaliza
🤣 🤣 🤣
 
Unaanza kuangalia video chafu za X tu, mwenyewe ataacha kuangalia, au unaanza kupiga naye selfie tu.
 
Nchi zilizoendelea ni mara chache sana utakuta mtu anadokolea macho kwenye simu yako. Kwa Tanzania ni jambo la kawaida sana. Na kuna jingine: kudokolea mtu macho kama panya aliyedakwa shingo. Hili Bongo wanalo sana wanaume hasa Dar.
Watu hawako busy sana
 
Baadhi ya abiria wamekuwa na tabia hii ya kuchungulia kinachoendelea kwenye simu za majirani zao wanapokuwa kwenye usafiri wa umma bila kujali hawapaswi kufanya hivyo.

Ukikutana na abiria kama huyu akiwa anachungulia unachofanya kwenye simu yako bila ridhaa yako unafanyaje?
Shida ya simu za laki na nusu ndio hiyo, simu za maana mtu wa pembeni akipiga chabo anaona dark tu.
 
Wagonjwa wa akili mnashauriana ujinga. Kama mnapenda faragha kuna namna lukuki za kuipata na simu yako. Ukitumia sehemu ya wazi utatizamwa tu.
 
Mi sioni kama wanafatilia simu ila kwa mbanano ule wa daladala unatoaje simu na kuanza kufanya mambo ya faragha.
 
Back
Top Bottom