Ukijiungana na TTCL tegemea kero hizi

EvilSpirit

JF-Expert Member
Jun 15, 2017
8,558
12,683
1. Customer care kuchelewa kupokea simu ya yako au kutokupokea kabisa.

2. Meseji kutofika kwa wakati au kutofika kabisa au kutoenda na hata ikifika ulipoituma usipate delivery report au meseji unaweza ukatuma muda huu ikifika baada ya masaa kadhaa au hata kesho yake.

3. Customer care kuwa waongo na wababaishaji.

4. Ukikwangua vocha vibaya ukafuta namba za vocha usitegemee utapata msaada ndio inakuwa imetoka hiyo wakati kuna mitandao ukifanya kosa hili ukiwasomea tu serial number wanaretrieve namba za vocha faster.

5. Ukiuliza salio sasa majibu unaweza kuyapata muda huo huo au baada ya masaa kadhaa hata kama ni zaidi ya siku.

6. Kwenye T-pesa huko ndio usithubutu kuweka au kumtumia hela kwenye hiyo huduma unaweza ukalia.

7. Vocha za TTCL kuzikuta ni mtihani unaweza kuzunguka mji/kitongoji kizima kuzitafuta.

Kwa kero hizi huwa najiuliza hivi hili shirika linajua hata nini linafanya? Ni shirika linaloongoza kwa huduma mbovu sana na sioni hata lipo kwa ajili ya nini sasa kama hata huduma haliwezi kutoa huduma za uhakikia
 
Tunajivunia maprofesa makini hapo TTCL. Wana uhakika wa mishahara ya nn wajitese?
Hiyo mishahara wanapewa tu pasipo kuingiza chochote mkuu.Sijui kwanini huduma za public ni za hovyo hovyo angalia hospitali zao,angalia shule,angalia tanesco
 
Nilitoka kwenye huo upuuzi baada ya kuona napata stress za bure ,hamia halotel mkuu utasahau hizo shida.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Halotel ni walewale tu kuna location nilihamia network ikawa slow kila siku nawapigia hamna cha maana wanachonisaidia.Miezi kama miwili iliyopita nilipoteza laini yao nikashukuru sana
 
''Dear customer, your balance has been used up. Please, dial *148*30# for more services!''

Hii message ya kifala inaingia mfululizo wakati ndo kwanza nimejiunga bundle gb 1.2 na dk 10 zinaisha wiki ijayo!

Acheni ujinga!
 
Heti hili shirika ndio serikali ya mwendazake ilikuwa inapanga litumiwe nchi nzima kama zile bombardiers mbovumbovu za ATCL
 
Ufala unaendelea!
IMG_0765.png

Yaani hapo nina madakika na mb kibao!

Halafu zinaingia kwa fujo, dk 1 msg 10!
 
Kwenye kupata internet,yani utasanda!
Na msg utatuma wee mpaka vidole vikatike ila haiendi,nilijua ni kwangu tu kumbe tuko wengi!
Ni kuhama tu hakuna namna!
 
1. Customer care kuchelewa kupokea simu ya yako au kutokupokea kabisa.

2. Meseji kutofika kwa wakati au kutofika kabisa au kutoenda na hata ikifika ulipoituma usipate delivery report au meseji unaweza ukatuma muda huu ikifika baada ya masaa kadhaa au hata kesho yake.

3. Customer care kuwa waongo na wababaishaji.

4. Ukikwangua vocha vibaya ukafuta namba za vocha usitegemee utapata msaada ndio inakuwa imetoka hiyo wakati kuna mitandao ukifanya kosa hili ukiwasomea tu serial number wanaretrieve namba za vocha faster.

5. Ukiuliza salio sasa majibu unaweza kuyapata muda huo huo au baada ya masaa kadhaa hata kama ni zaidi ya siku.

6. Kwenye T-pesa huko ndio usithubutu kuweka au kumtumia hela kwenye hiyo huduma unaweza ukalia.

7. Vocha za TTCL kuzikuta ni mtihani unaweza kuzunguka mji/kitongoji kizima kuzitafuta.

Kwa kero hizi huwa najiuliza hivi hili shirika linajua hata nini linafanya? Ni shirika linaloongoza kwa huduma mbovu sana na sioni hata lipo kwa ajili ya nini sasa kama hata huduma haliwezi kutoa huduma za uhakikia
CCM wanaua nchi.
 
Back
Top Bottom