Ukienda Mjini kutafuta Maisha hakikisha unafanya haya

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,892
UKIENDA MJINI KUTAFUTA MAISHA HAKIKISHA UNAFANYA HAYA

Anaandika, Robert Heriel

Leo sina mengi ya kusema, najua Maisha hayana Formula Ila zipo Formula katika Maisha. Ukitaka chukua usipotaka Acha.

Ooh! Mimi ni kijana, nina miaka 25, sina hili wala lile. Sijui nikatafutie wapi Maisha. Mimi ningekujibu nenda Dar. Lakini kama huko mazingira hayakuruhusu basi nenda mji wowote mkubwa. Ukifika huko basi nisikilize,

Ukija mjini hakikisha haya yanatokea unayafanya

1. Uwe na ujuzi wowote iwe ni ujuzi wa ukinyozi, ufundi nguo, udereva, n.k

2. Uwe tayari kufanya kazi yoyote ya nguvu na Akili

Akili na nguvu vitatumika Kwa pamoja au kuna Wakati utatumia kimoja zaidi ya kingine.

3. Uwe MTU mwenye Bajeti Kali na msoma ramani, kisomi tunakuita Street- surveyor
Tumia Kanuni ya resources management ya Aidha Reuse au recycling Kwa vitu ambavyo unaona vinafaa kutumika zaidi ya mara moja. Usile kama upo Nyumbani kula kama mwanajeshi aliyepo vitani. Ukilakila Akili itakuwa inalewalewa na utakuwa unawaza kunyakunya au kuwaza ngono. Angalau Kula mara mbili Kwa siku Kwa interval ya masaa 5:30 mpaka masaa sita. (Kula itategemea unafanya kazi ipi, kama ni kazi za nguvu itakupasa ule haswa)

4. Uwe mtu wa kufuata mambo yako
Usiwe conservative, mambo ya kusema Dunia imeharibika sijui kule kwetu kupo hivi uwapo huku usiyatumie Sana. Tumia kilichopo Kupata ambacho hauna. Usitumie ulichonacho kukipoteza unachomiliki.

5. Kabla hujafanya maamuzi fanya utafiti Kwanza
Sio unanunua Nunua vitu bila kufanya uchunguzi. Utajikuta unapata hasara.

6. Usitafute Mchumba au mpenzi
Mapenzi hayakai pamoja na Shida nyakati za mwanzoni. Kibongobongo mapenzi ni liability, utapata hasara kubwa ewe kijana. Ikiwa utaona umetingwa Sana Draft Bajeti ambayo itaeleza mara ngapi Kwa mwezi utanunua Huduma za mapenzi. Usije leta mambo ya dhambi, hiyo Kanuni haitafanya kazi Huko mjini. Alafu elewa kuwa dhambi sio hiyo moja tuu, na NI ngumu kupitisha siku bila kutenda dhambi labda ulale siku hiyo. Na sio ajabu kulala kwenye bila sababu ikawa ni dhambi.

7. Zima location yako (turnoff your GPS)😂😂

Nimeona nikuchanganyie kakingereza kidogo ili unione mtaalamu😊. Kivyovyote iwavyo unapoanza Maisha lazima utakuwa dhoofu hali, utakuwa dhalili. Zima data, Zima location, hakikisha Watu wako wa karibu hawajui unaishi wapi na unafanya shughuli gani. Kanuni hiyo ni muhimu sana. Hata hivyo watu wengi watajitahidi kukuchimba na kukuchimbua ili wajue upo wapi, unakaa wapi na unajishughulisha na nini. Watatoa visingizio ati unaweza kupatwa na Baya hivyo ni muhimu wanajua ulipo. Usiwasikilize😊😊. Jichimbie hukohuko kwenye handaki. Mpaka utakapopata ahueni ya Maisha.

Kuna faida nyingi kivita endapo utaficha location yako na shughuli zako unazozifanya kuliko kuziweka wazi
Usimwambie yeyote Yule hata kama ni Mama au Baba yako. Watajifanya hawatasema Ila kimsingi watasema, na nduguzo na jamii yako wayajifanya hawajui ulipo na unachofanya kumbe wanajua.

8. Usisaidie wala usijipe wajibu wa kusaidia mtu ukiwa katika hatua za awali
Kuna Wakati WA kupanda na wakati wa kuvuna. Uliona wapi MTU akienda kuvuna kwenye mti usio na matunda? Wewe bado hujajimudu, ni kama mti unaochipusha majani kisha utoe maua alafu MTU aje atake matunda Wakati hata mti haujatoa matunda.

Ndio maana nikakuambia ficha location, ficha unachokifanya. Watu wengi hupenda kujua ulipo na unachokifanya sio Kwa sababu wanataka kukusaidia au kukusapoti Bali ni kwaajili ya kujipatia faida Kutoka Kwako.Sisemi nakufundisha uchoyo, Ila nakueleza uhalisia wa mambo yalivyo. Mtu akibisha abishe.

9. Hakikisha majirani hawakujui vizuri
Kuwa muugizaji, kuwa bingwa wa drama. Uhakika ni kuwa kwa kipato chako kwa vile bado ni Duni, utapanga kwenye nyumba yenye wapangaji watakaotaka kukujua wewe ni Nani, asili yako ni ipi, na unajishughulisha na nini. Usipende wakujue na hakikisha wasikujue vizuri na wakikujua basi wakujue kwa taarifa nyingi za uongouongo. Zikubali hizo taarifa wanazokujua nazo.

Elewa kuwa Watu wanatafuta kukujua ili wakudharau au wakuheshimu. Na mara nyingi Watu wakikujua hukudharau na heshima inapungua. Elewa kuwa Watu na hapa nazungumzia majirani watakuhukumu Kwa vile wanavyokujua, mfano watasema, ninyi wagogo ndivyo mlivyo, au ninyi Wachaga ndivyo hivi mlivyo. Mara zote watakuweka kwenye upande negative/upande wa mabaya.

10. Epuka magenge au kukaa vijiweni
Labda kijiwe kiwe kazini mfano Garage, au fundi nguo, au karakana la seremala n.k. Hakikisha unapokaa hapo kijiweni ambapo ni ofisi ya MTU ujifunze Dani hiyo hata kama ni juujuu. Mfano kama kijiwe kipo kwenye Gereji ya bodaboda, jipe muda kisha Anza kujifunza ufundi bodaboda na udereva bodaboda. Unapata muda wa kupiga umbea alafu hapohapo unapata ujuzi Bure.

11. Epuka kuingiza marafiki ghetto lako au kwenda Ghetto la marafiki zako
Urafiki wa mjini haundeshwi hivyo. Tumekutana mjini tutaishia mjini kwenye vijiwe, au migahawa au hoteli au fukwe.

12. Epuka kujiingiza kwenye migogoro isiyo na maana Kwa kuonyesha kuwa unahitaji Heshima
Taikon ninatumia Kanuni isemayo, sio lazima Kupata heshima ya kila MTU. Kudharauliwa hakuna nguvu endapo utakuwa na mtazamo wa kuwaweka Watu kwenye makundi Yao. Mbwa hawezi kukubwekea alafu nawe ukabweka. Huwezi tafuta heshima Kwa Mbwa au kunguru labda nawe uwe kunguru au Mbwa. Elewa kuwa migogoro mingi ni matokeo ya Makosa ya kuwaweka Watu kwenye makundi yasiyoyao. Ukaribu na mazoea yaliyopitiliza ndio huzalisha migogoro mingi.

13. Ishi vizuri na watu uwapo mjini maana haohao ndio Wateja na watakaotumia bidhaa au Huduma yako
Sio Mama yako au Baba yako au Ndugu yako au marafiki zako watakaokuunga katika biashara yako utakayoianzisha, asilimia 99% watakaokusapoti ni wale usiowajua hasa katika hatua ngumu za Maisha.

14. Usipende kukaa ndani ikiwa shughuli zako sio za kutumia akili
Kama shughuli zako asilimia kubwa zinahitaji nguvu penda kutembea tembea kutafuta riziki

15. Epuka MTU anayelazimisha kuingia kwenye circle yako bila kumfanyia vetting ya kutosha.

16. Starehe ni muhimu lakini usiiendekeze.

17. Usipende kueleza matatizo au shida zako kwa watu
Mfano, hata kama umesoma na hauna Ajira. Usipende kujitangaza tangaza umesoma lakini hauna Ajira ukadhani ATI Watu watakuonea huruma na watakupa Ajira. Sio kweli. Hautaonewa huruma isipokuwa utakuwa Case study hapo mtaani kuwa umesoma lakini hauna Ajira na watu vijiweni watajenga hoja zao Kuwa Elimu sio Jambo lolote wakitumia hoja Madhubuti na dhahiri kupitia wewe. Elewa kuwa matatizo hatatangazwi Ila yanajitangaza yenyewe, kuyatangaza matatizo nu kuongeza tatizo jingine.

18. Weka Malengo, mipango na mikakati yako

Andika, Mwaka 2023 nitanunua kitanda Tsh 200,000/= , hapo tayari unagodoro, Sabufa Tsh 150,000/= Mashuka, mapazia, Jiko la Gesi(hapo unatumia Jiko la mkaa) jumla ya Pesa labda ni Tsh 1,000,000/= milioni moja ya Kitanzania. Ndio Bajeti ya malengo yako Kwa Mwaka huu. Tembelea humohumo. Usitoke.

19. Usipende mashindano

Mara nyingi wivu ndio huchochea mashindano. Ukiona jirani kanunua kitu nawe unataka kununua. Nop! Mambo hayaendi hivyo. Tayari unamalengo na mipango yako. Hiyo ndio ramani yako Kwa Mwaka huu. Kwanini mwenzako akinunua Luninga Roho ikuruke? Mashindano yatakuondoa kwenye mchezo, utapoteza Focus (shabaha) Kwa sababu za kijinga. Ukishapanga malengo yako hakikisha yanatimia pasipo Excuse yoyote.

20. Epuka kuwa mzigo kwa mtu

Weka Bajeti zako vizuri zikutosheleze. Usisumbue sumbue Watu. Kila MTU anamsalaba wake. Umakini ni muhimu katika kuhakikisha hauwi mzigo Kwa MTU. Kuwa Mzigo Kwa MTU huleta uhasama, majungu na kudharaulika.
Labda litokee tatizo nje ya uwezo wako mfano, Umepata ajali, umeumwa n.k Lakini sio unakosa Pesa ya kula unaanza kusumbua Watu. Ukikosa Pesa ya kula nenda kakope Unga na Mafuta Kwa Mangi au kwenye Duka unaponunuaga bidhaa. Wewe si mteja wao. Kushindwa kukopa au kukopeshwa mjini tafsiri yake hauaminiki na sio muwajibikaji. Hivyo Watu wanaona hautawalipa.

21. Ishi sehemu ya watu mlio daraja awa kuepusha migogoro
Sio unaenda kuchukua chumba cha laki moja Wakati uwezo wako ni Chumba cha elfu 50. ATI ili nawe uonekane matawi ya juu. Utakwama. Elewa kuwa Duniani hakuna Maisha magumu isipokuwa Watu hutafuta ugumu Kwa kuingia kwenye nafasi na matabaka au majukumu yasiyoyao. Unapochukua chumba cha laki na wapangaji wenzako hadhi na Daraja Lao ni laki. Jua hata vitu wanavyotumia vinaendana na hadhi Yao. Elewa kuwa umeme sio ajabu ukaambiwa utoe elfu 30 Kwa mwezi, maji elfu 10-25 Kwa mwezi. Mwisho utaanza kulalamika kuwa wewe hautumii umeme mwingi Kutokana na hauna vifaa vinavyotumia umeme. Watakuambia haujakatazwa kununua. Mwisho inakuwa mtihani kwako.

Nipumzike Kwanza, kisha tutaendelea.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom