Ukiambiwa upunguze jambo au uongeze jambo kwenye katiba yetu utachagua lipi?

Jun 25, 2023
10
24
Zote tunajua kuwa katiba yetu inamapungufu mengi. lakini sasa wewe kama mtanzania mzalendo ungepewa nafasi ya kuifanyia marekebisho ungetamani jambo gani jipya liwemo na lipi liondolewe ili Sisi kama Taifa tuwe na katiba nzuri kama nchi zingine.

Mimi nikipata nafasi hiyo nafuta tasisi ya kuzuia rushwa, kwa nini? Haiko fair, na inakamata walala hoi tu, mkubwa haguswi. karibuni kwa maoni!
 
Rais aweze kushitakiwa akiwa au ametoka madarakani. Kusiwe na kitu kinaitwa Kinga kwa yoyote. Kifungu hiki ndio sababu hasa ya udhaifu wa mifumo yote nchini, na wizi mkubwa wenye ulinzi wa kidola.
 
Ardhi ya eneo lote la Tanzania nairudisha kwa wananchi, Kila raia amilikishwe ardhi na apewe hati ya umiliki.
 
Zote tunajua kuwa katiba yetu inamapungufu mengi. lakini sasa wewe kama mtanzania mzalendo ungepewa nafasi ya kuifanyia marekebisho ungetamani jambo gani jipya liwemo na lipi liondolewe ili Sisi kama Taifa tuwe na katiba nzuri kama nchi zingine.

Mimi nikipata nafasi hiyo nafuta tasisi ya kuzuia rushwa, kwa nini? Haiko fair, na inakamata walala hoi tu,mkubwa haguswi. karibuni kwa maoni!
Zanzibar iwe mkoa wa Tanzania au kuwe na serikali ya Tanganyika.
 
Kuharibu uchaguzi wowote au kuharibu kura kwa namna yoyote iwe ni kosa la uhaini... maana ni sawa na kupindua uongozi halali na kuweka viongozi mamluki.

Na pia kuwe na full transparency kwenye mchakato wote wa uchaguzi, kura ya mtu tuu ndio iwe siri.
 
Hii inatakiwa iwekwe kwenye hiyo miswaada ya sasa inayopelekwa bungeni.
 
Tutengeneze namna nyingine yakuwa na bunge linalojielewa lisiloweza kuingiliwa na rais kichaa ama chama nyonyaji
 
1. Rais apunguziwe madaraka, asiteue viongozi wa mihimili mingine. Na ashitakiwe akivurunda kwenye kiti.
2. Sifa za kielimu za mgombea ubunge zirekebishwe . Lazima awe na shahada ama zaidi.
3. Viti maalumu vifutwe.
4. Ma DC waondolewee
 
Tume huru ya uchaguzi na matokeo yote ya uchaguzi kupingwa mahakani.

IGP, TISS ,CAG ,CDF , CJ ziwe nafasi za kuombwa viwekwe vigezo watu kuomba hiyo kazi na wanao omba wafanyiwe usaili na kupigiwa kura na wabunge ili kuondoa mzigo kwa Rais na kufanya kazi kwa maelekezo vyombo viwe na uhuru wa kweli lakini vigezo na masharti vizingatiwe.

Zanzibar iwe ni mmoja ya mkoa wa Tanzania na kule kusiwe na Rais bali waziri mkuu wa pili au makamo wa pili wa Rais ndio ataongoza eneo la zanzibar atapigiwa kura pamoja na Rais na hatokuwa na mamlaka kumzidi Rais hivyo zanzibar itakuwa ni mkoa ndani ya Tanzania….
 
Naunga mkono hoja
 
CCM hawakubali lolote wao wanawaza wizi milele kwa Katiba hihi mbovu na kuwapa watoto na vijukuu vyao madaraka
Hawakubali kwa sababu ni wezi wakubwa, wamepora mamlaka ya Dola na kugeuza sera za chama chao kuwa za taifa.
Sera za taifa zinatakiwa kubuniwa na wataalamu wa uongozi na uchumi, wakati vyama na sera zao zikitumika kumpata mtu atakaye simamishwa kuwa Rais.
Anayeteuliwa kugombea irais, akishinda atakwenda kusimamia utekelezaji wa sera za taifa.
sio huu uchafu wa ilani ya uchaguzi ambao unapaswa kubaki huko huko chamani...
 
Muungano uvunjwe! Hatuna cha kugawana, Tanganyika irudi kwenye nafasi yake na Zanzibar na Pemba yake wapotelee huko huko baharini. Tuingie kwenye Jumuia ya afrika Mashariki kama nchi mbili huru. Kuendelea kutatua kero za muungano ni kuendelea kulea genge la wezi na waharifu. 😡💢
 
Back
Top Bottom