Ukiambiwa uchague kimoja kati ya hizi project za Kilimo utachagua ipi? na why?

Kwa maziwa na nyama now ni karibia nchi nzima, Majanga ya asili hasa Ukame yanateketeza sana mifugo hasa Ng'ombe, hajuna kwenye unafuu sana, hata huku Kaskazini, na kwa baadae nyama itakuja kuliwa na wenye uwezo tu, wengine tutangoja siku za sikukuu.
 
mi ninavyoona ufugaji wa nguruwe ni kama mali akiba
ukianza na malisho yao+madawa(chanjo) unakuja kumuuza kwa bei
ambayo haijapishana sana na gharama ulizotumia katika ufugaji wake
I concur with you. Nishafuga nguruwe kwa miaka 2 nilichanganya santula na highbreed kama PT, duroc na DuPi. Nilichofanya ni kama nilikuwa natunza excess money yangu niliyokuwa napata kazini, let say kila mwezi Kuna laki 5 nainywea pombe basi nikawa nalishia nguruwe nakuja irudisha baadae nikipata shida nauza nguruwe. Sasa maamuzi yangu ni nn?
Naanza kufanya Miradi 2 kwa mpigo, mosi ng'ombe wa maziwa na nguruwe nipo kwenye ujenzi wa mabanda.
 
Ufugaji wa nguruwe unalipa sana, hasa ukipata mbegu nzuri. Maana nguruwe ukimtunza vizuri, akiwa na umri wa kuanzia miezi 8. Siyo chini ya 250,000. Hiyo inategemeana na maeneo uliyopo.
Nikitaka m25 natakiwa niwe na nguruwe 100 ambao nimewatunza kwa miez 8, gharama ya matunzo?
 
Mimi no.19, Bata, lakini kwanza mpaka nifanye upembuzi yakinifu hahah kuona kama market ipo ama vipi, Bata ni rahisi hawasumbui sana magonjwa
 
Ukichagua namba 1&2 kisha ukachanganya na 14, huji kuishiwa pesa, nafanya mimi nafuga ngombe,nalima kiazi, na ovacado, nauza
 
Back
Top Bottom