UKAWA yasambaratika wilaya ya Kwimba

mandago shululu

Senior Member
Mar 24, 2013
124
34
Nianze kwa kuomba radhi kwa kichwa cha habari kwani maelezo yangu yatakuwa kinyume.

Katika kuwekeana misingi imara ya ukawa na mikakati bora ya ushindi ndani ya UKAWA ikiwa ni ndani ya mwezi mmoja tu baada ya UKAWA kushika kasi Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Mh Freman Mbowe mzee wa kubadilisha gia akiwa angani (naipenda sana hii) alisikika kwenye vikao vya Ukawa akisema kwamba naomba kumnukuu. "Kwa yeyote yule atakayekiuka taratibu za ukawa tutamshughulikia ipasavyo" mwisho wa kunukuu.

Juzi mgawanyo wa majimbo ulikamilika kwa makubaliano na majimbo yote yakatangazwa kwa vyama vyote vinavyounda Ukawa yaani Chadema ,NCCR Mageuzi,C U F na N L D,Vilevile jana orodha ya majina ya wagombea wote wa Chadema yalitangazwa kulingana na mgawanyo wa majimbo.Katika mgawanyo wa majimbo mkoa wa Mwanza wenye majimbo tisa Chadema ilipata majimbo saba na C U F ilipata majimbo mawili ambayo ni Kwimba na Sumve kwa mantiki hiyo basi hata katika orodha ya majina ya wagombea ubunge wa chadema waliotangazwa jana majimbo yote mawili ya Kwimba na Sumve hayakuwa na wagomea kwani tayari C U F walishapewa.

Kulingana na mgawanyo huo wa majimbo baadhi ya wagombea wa Chadema walidharau mgawanyo huo na kujichukulia maamuzi kama ifuatavyo.

Mwenyekiti wa Chadema wilaya yaKwimba ndugu Babila Shilogela Nganga ambaye alikuwa mtiania ubunge jimbo la kwimba vilevile aliyekuwa mshindi wa tatu kwa kupata kura 40,mnamo Tarehe 14/08/2015 siku ya Ijumaa alifanya kikao na Kaimu katibu wa Chadema Wilaya ya Kwimba ndugu Said Abdallah (wawili tu ofsini) wakateuana kwamba wewe Mwenyekiti ambaye ni mshindi wa tatu ndio uwe umeteuliwa na chama kupeperusha Bendera ya Chadema jimbo la kwimba,Baada ya hapo kaimu katibu akajikunja kumwandikia barua huyo mshindi wa tatu mwenye kura 40 ya kumtambuliwa kuwa ndiye aliyeteuliwa na chama,baada ya hapo Ndugu Shilogera akaenda kw Mkurugenzi kuchukua fomu.Vilevile ikumbukwe kwamba matokeo ya jimbo la kwimba ya kura za maoni yalikuwa kama ifuatavyo kwa tatu bora.

  1. Juliaus Ntiga Otto- kura 122
  2. John Thobias Nzwalile {Mwana wa Nzwalile,Katibu Chadema (M) Mwanza}-kura 60
  3. Babila Shilogera Nganga (Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kwimba) kura 40

Leo Tarehe 19/08/2015 mwenyekiti wa Wilaya akapiga simu kwa mshindi namba moja wa jimbo la Sumve ndugu Ng'holo Malimi aliyepata kura 132 akimwambia kwamba aje achukue fomu ya kugombea ubunge kwani jina lake limeshachaguliwa naye akatii maagizo ya katibu wa wilaya amekuja na akachukua fomu kwa tiketi ya Chadema.

Wakati yakifanyika hayo ndugu Mchele ambaye ni mgombea Ubunge kwa tiketi ya C.U.F alishachukua fomu wiki iliyopita kwa jimbo la Sumve,vilevile aliyekuwa mshindi namba moja kwa jimbo la kwimba upande wa chadema Ndugu Julius Ntiga baada ya kuona kwamba jimbo la kwimba limeenda C U F ilimbidi aongee na viongozi wa C U F ili waweze kuelewana kama anweza akagombea yeye ili achukue kadi ya C U F n a hatimaye akachukue fomu ya kugombea,baada ya mazungumzo ya muda mrefu wakawameelewana ndipo akachukua fomuleo asubuhi.

Ukiangalia mgawanyo wa majimbo na kanuni za UKAWA tayari jimbo la kwimba halijafata hizo kanuni wala makubaliano yoyote yale kwani kila chama kitapeperusha bendera kama kwamba majimbo hayo hayakupatiwa mwafaka kitu ambacho si kweli.

Hivyo basi Mwenyekiti wa Wilaya Ndugu Babila Shilogera (0756281883) na Kaimu katibu wa wilaya ndugu Saidi Abdallah (0758423673) wamekiuka taratibu za ukawa. "Kwa yeyote yule atakayekiuka taratibu za ukawa tutamshughulikia ipasavyo" Mh Mbowe ( Mwenyekiti wa Chadema Taifa). Tunaomba iwe hivyo.

Huku wananchi hawajaelewa juu ya hali hii,wanauliza kwamba Hivi UKAWA umeshavunjika,majibu yangu juu ya swali lao ni kwamba,UKAWA bado iko imara na msitegemee siku moja itavunjika ilianza na Mungu na itamaliza na Mungu.

Kulingana na maelezo hayo pia nami nauliza maswali kwa viongozi wakuu wa UKAWA
  1. Hali hii ya Jimbo la Kwimba na Sumve mnaielewa?
  2. Mgawanyo wa majimbo mlioutoa juzi majimbo ya kwimba na Sumve yalipewa chama gani?
  3. Kama jibu la swali la pili ni C U F,nini msimamo wa viongozi wakuu wa UKAWA kwa hawa waliokiuka makubaliano ya ukawa na wakajiamulia wenyewe kujiteua kuwa wagombea?

Binafsi sijapendezwa sana na kitendo hikicha kukiuka makubaliano ya viongozi wakuu
naomba kutoa hoja,nadhani majibu mwafaka yatapatikana.
Mandago
Katibu Chadema wilaya ya Kwimba
0765183733/0782270412 kwa ufafanuzi zaidi
 
Nadhani hiyo ndo ilikuwa maana ya msemo wa Mbowe kubadilsha gia angani, hata hao pia wamebadilisha gia angani. Make hata Lowasa naye kabadilisha gia angani kwani wapi Dr.Slaa na Prof. Lipumba hata jimbo la Bunda Esther Bulaya naye kabdilsha gia angani dhidi ya mshindi Bw. masuruli-hiyo ndo UKAWA hata kabla hawajapewa nchi wanaanza kupigiana sanaa, je wakikabidhiwa? Ina maana kila mtu atakuwa na muhuri nyumbani kwake kwa ajili ya kubadilishia gia angani. Ila nimeipenda sana hiyo!
 
Viongozi wa ukawa wapo busy majimboni kuchukuwa na kurudisha fomu kuwania nafasi za ubunge na udiwani. Hilo ni jambo dogo kulitatua lisikupe pressure kamanda, tusubiri warejeshe fomu zao majimboni then hatua zichukuliwe. Ukawa ni mpango wa Mungu Hakuna wa kuuvuruga sasa.
 
Back
Top Bottom