UKAWA wazuiwa kufanya mkutano Jangwani na Uwanja wa Taifa

KUHUSU MKUTANO WA UKAWA JANGWANI,
Kuna barua inazunguka mitandaoni inadaiwa kuwa ni ya Mkurugenzi wa manispaa ya Ilala akidai kuzuia UKAWA kuzindulia kampeni zake uwanja wa Jangwani kwa sababu kuna shughuli nyingine (ambayo hakuitaja).

Ili kuweka kumbukumbu vizuri, naomba niwasisitize kuwa Mkutano wa uzinduzi wa kampeni za UKAWA, utafanyika Jangwani jumamosi ya tarehe 29 kama ilivyopangwa.
Ratiba ya mikutano ya kampeni inatolewa na Tume, na kwa mujibu wa ratiba hiyo, Tume imeipa kibali Chadema kufanya mkutano kwa uwanja wa Jangwani siku hiyo.
Ikumbukwe Tume ya Uchaguzi ndiyo yenye mamlaka ya viwanja vyote na maeneo ya wazi nchini kwa kipindi hiki cha uchaguzi.

Dar ina maeneo makubwa ya wazi 18 ambayo yote yamekabidhiwa kwa Tume ya uchaguzi kwa kipindi chote cha kampeni hadi siku ya uchaguzi. Hivyo basi Tume ndiyo msimamizi wa maeneo hayo kwa sasa, na sio halmashauri ya Manispaa wala jiji.

Kwa hiyo nichukue fursa hii kuwaondoa hofu kuwa hakutakuwa na shughuli yoyote ndani ya viwanja vya Jangwani siku ya jumamosi August 29, isipokuwa mkutano wa UKAWA tu.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala haina mamlaka ya kutoa kibali kwa matumizi ya uwanja huo katika nyakati hizi za kampeni, mamlaka hayo kwa sasa yapo chini ya Tume ya uchaguzi tu. (kwa mujibu wa sheria ya Uchaguzi namba 7 ya mwaka 2010).

Hili ni kwa viwanja vyote nchini vilivyoorodheshwa kwa matumizi ya kampeni.
Halmashauri za Manispaa, miji, wilaya na majiji zitarudishiwa mamlaka za kuendesha viwanja hivyo baada ya uchaguzi kumalizika, yani October 26 na kuendelea.
Hivyo basi kitendo cha Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuandika barua ya kuzuia uwanja wa Jangwani kutumiwa na UKAWA wakati akijua hana mamlaka ya kufanya hivyo ni kitendo cha kulaaniwa na kupuuzwa na watu wote wenye akili timamu.

Pia Mkurugenzi huyo anapaswa kuchukuliwa hatua kwa kupuuza Sheria ya Uchaguzi namba 07 ya mwaka 2010.
Hizi ni dalili za wazi za CCM kutumia vyombo vya umma kuhujumu uchaguzi. Hofu ya kushindwa imewageuza CCM na ma-agent wake kuwa vichaa. Wanatapatapa, Wanaweweseka. Wanatumia kila mbinu kuhujumu.

Wanaogopa nini tukitumia Uwanja wa Jangwani? Wanahofia kuwa mshindi wa Urais atajulikana maana mafuriko yatakuwa mara 10 ya ule mkutano wao. Wanahofia tutawafunika, kwa hiyo ili watanzania wasijue nguvu ya UKAWA inabidi wakatae matumizi ya uwanja huo.
Kwanini tusiwe na Fair Competition? Kwanini tusifanye siasa za kistaarabu? Wao walifanya mkutano Jangwani tukatulia, watuache na sisi tufanye. Halafu tutapima nani alipata watu wengi. Mbona wanatapatapa?

Wao waliandamana siku ya mkutano wao, tukakaa kimya. Wakazidisha muda wa mkutano, tukakaa kimya. Wakampiga marufuku mgombea wetu kupanda daladala, tukakaa kimya. Wakatuzuia kutumia uwanja wa taifa kufanya uzinduzi wa kampeni tukakaa kimya, sasa wanataka kutuzuia hata Jangwani? Hatuwezi kuvumilia udhalimu huu.

Uwanja hatukuomba Manispaa, tuliwasilisha ratiba yetu Tume ya Uchaguzi na wakaturuhusu. Ofisi ya manispaa walipewa tu taarifa ya "kuwanotify" kuwa tutatumia uwanja huo.
Sasa ni ajabu mtu unampa "notification" afu anakurupuka na kuandika barua ya kukataa.

Anakataa nini sasa? Yani ni sawa na kununua gari halafu unamnoyify rafiki yako kuwa umenunua gari halafu anakataa usinunue. Anakataaje na umeshanunua? Huu ni ujuha wa kiwango cha PhD.

Kwa kuwa ratiba yetu ipo tume na imeshapitishwa, tungeweza kufanya mkutano Jangwani bila kuwajulisha ofisi ya Manispaa ya Ilala. Lakini kwa uungwana tukaamua tuwajulishe kuwa tutakua Jangwani siku hiyo, cha ajabu eti wanakataa. Sasa wanakataa nini?

Narudia tena 29/8/2015, Chadema/UKAWA, itazindua kampeni zake katika viwanja vya Jangwani, Hivyo puuzeni taarifa za makada wa CCM kutoka Manispaa ya Ilala wanaojifanya kuweka matumizi mbadala ya uwanja huo.
Kama huyo Mkurugenzi anataka kumcheza mwanae ngoma, atafute eneo jingine sio uwanja wa Jangwani, maana uwanja huo tunao kibali cha kuutumia.
Tukutane Jangwani Wapumbavu na Malofa wenzangu 29/8/2015!

KUHUSU MKUTANO WA UKAWA JANGWANI,Kuna barua inazunguka mitandaoni inadaiwa kuwa ni ya Mkurugenzi wa manispaa ya Ilala akidai kuzuia UKAWA kuzindulia kampeni zake uwanja wa Jangwani kwa sababu kuna shughuli nyingine (ambayo hakuitaja).

Ili kuweka kumbukumbu vizuri, naomba niwasisitize kuwa Mkutano wa uzinduzi wa kampeni za UKAWA, utafanyika Jangwani jumamosi ya tarehe 29 kama ilivyopangwa.
Ratiba ya mikutano ya kampeni inatolewa na Tume, na kwa mujibu wa ratiba hiyo, Tume imeipa kibali Chadema kufanya mkutano kwa uwanja wa Jangwani siku hiyo.

Ikumbukwe Tume ya Uchaguzi ndiyo yenye mamlaka ya viwanja vyote na maeneo ya wazi nchini kwa kipindi hiki cha uchaguzi.
Dar ina maeneo makubwa ya wazi 18 ambayo yote yamekabidhiwa kwa Tume ya uchaguzi kwa kipindi chote cha kampeni hadi siku ya uchaguzi. Hivyo basi Tume ndiyo msimamizi wa maeneo hayo kwa sasa, na sio halmashauri ya Manispaa wala jiji.

Kwa hiyo nichukue fursa hii kuwaondoa hofu kuwa hakutakuwa na shughuli yoyote ndani ya viwanja vya Jangwani siku ya jumamosi August 29, isipokuwa mkutano wa UKAWA tu.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala haina mamlaka ya kutoa kibali kwa matumizi ya uwanja huo katika nyakati hizi za kampeni, mamlaka hayo kwa sasa yapo chini ya Tume ya uchaguzi tu. (kwa mujibu wa sheria ya Uchaguzi namba 7 ya mwaka 2010).

Hili ni kwa viwanja vyote nchini vilivyoorodheshwa kwa matumizi ya kampeni.
Halmashauri za Manispaa, miji, wilaya na majiji zitarudishiwa mamlaka za kuendesha viwanja hivyo baada ya uchaguzi kumalizika, yani October 26 na kuendelea.

Hivyo basi kitendo cha Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuandika barua ya kuzuia uwanja wa Jangwani kutumiwa na UKAWA wakati akijua hana mamlaka ya kufanya hivyo ni kitendo cha kulaaniwa na kupuuzwa na watu wote wenye akili timamu.

Pia Mkurugenzi huyo anapaswa kuchukuliwa hatua kwa kupuuza Sheria ya Uchaguzi namba 07 ya mwaka 2010.
Hizi ni dalili za wazi za CCM kutumia vyombo vya umma kuhujumu uchaguzi. Hofu ya kushindwa imewageuza CCM na ma-agent wake kuwa vichaa. Wanatapatapa, Wanaweweseka. Wanatumia kila mbinu kuhujumu.

Wanaogopa nini tukitumia Uwanja wa Jangwani? Wanahofia kuwa mshindi wa Urais atajulikana maana mafuriko yatakuwa mara 10 ya ule mkutano wao. Wanahofia tutawafunika, kwa hiyo ili watanzania wasijue nguvu ya UKAWA inabidi wakatae matumizi ya uwanja huo.

Kwanini tusiwe na Fair Competition? Kwanini tusifanye siasa za kistaarabu? Waowalifanya mkutano Jangwani tukatulia, watuache na sisi tufanye. Halafu tutapima nani alipata watu wengi. Mbona wanatapatapa?

Wao waliandamana siku ya mkutano wao, tukakaa kimya. Wakazidisha muda wa mkutano, tukakaa kimya. Wakampiga marufuku mgombea wetu kupanda daladala, tukakaa kimya. Wakatuzuia kutumia uwanja wa taifa kufanya uzinduzi wa kampeni tukakaa kimya, sasa wanataka kutuzuia hata Jangwani? Hatuwezi kuvumilia udhalimu huu.

Uwanja hatukuomba Manispaa, tuliwasilisha ratiba yetu Tume ya Uchaguzi na wakaturuhusu. Ofisi ya manispaa walipewa tu taarifa ya "kuwanotify" kuwa tutatumia uwanja huo.
Sasa ni ajabu mtu unampa "notification" afu anakurupuka na kuandika barua ya kukataa.

Anakataa nini sasa? Yani ni sawa na kununua gari halafu unamnoyify rafiki yako kuwa umenunua gari halafu anakataa usinunue. Anakataaje na umeshanunua? Huu ni ujuha wa kiwango cha PhD.

Kwa kuwa ratiba yetu ipo tume na imeshapitishwa, tungeweza kufanya mkutano Jangwani bila kuwajulisha ofisi ya Manispaa ya Ilala. Lakini kwa uungwana tukaamua tuwajulishe kuwa tutakua Jangwani siku hiyo, cha ajabu eti wanakataa. Sasa wanakataa nini?

Narudia tena 29/8/2015, Chadema/UKAWA, itazindua kampeni zake katika viwanja vya Jangwani, Hivyo puuzeni taarifa za makada wa CCM kutoka Manispaa ya Ilala wanaojifanya kuweka matumizi mbadala ya uwanja huo.

Kama huyo Mkurugenzi anataka kumcheza mwanae ngoma, atafute eneo jingine sio uwanja wa Jangwani, maana uwanja huo tunao kibali cha kuutumia.

Tukutane Jangwani Wapumbavu na Malofa wenzangu 29/8/2015!

Taarifa kuwa UKAWA wamenyimwa uwanja ni za kweli na kwa taarifa zaidi fungua hii link East Africa Television (EATV) - https://m.facebook.com/eatv.tv?_rdr
 
Team hasira! Acha hizo tume itarekebisha tu mtaandamana jangwani na ulinzi mtapata . Tz ni nchi ya amani na watu wake ni polite !
 
Barua gani hata muhuri haina,,,??? Hizo mbinu za kisiasa tu,,,hamna ofisi ya serkal ambayo haina mihuri hiyo ni kwa ajiri ya malofa tu
 
Attachments

  • 1440596386602.jpg
    1440596386602.jpg
    54.5 KB · Views: 221
Ccm hawajui ngoma wanayo icheza ni hatari sana,wanaishi kwa mazoea
 
Libya siyo TanZania kuna tofauti kubwa sana kwenye kila nyanja kuanzia kitaifa mpaka kimataifa! Libya iliwekewa vikwazo vya kiuchumi na Umoja wa Mataifa nchi yetu haijawahi, Libya ilikuwa na uhusiano mbaya na nchi nyingi Duniani zikiwemo Majirani zake, TanZania ina uhusiano mzuri na nchi nyingi sana Duniani, majirani zetu wanatupenda kuanzia SADC mpaka AM na Umoja wa nchi za Kiafrika, Libya kulikuwa hakuna Uchaguzi na Gadafi alikuwa Kiongozi wa maisha, TanZania yetu tuna uchaguzi kila baada ya miaka 5 na Uraisi una kikomo na mpaka leo hii ni nchi chache zilizoweza kutii ukomo wa Uongozi kama sisi, TanZania ni kioo cha utawala Bora Afrika na tumepata sifa na medali nyingi sana, Libya haijawahi, TanZania yetu wanaoitwa wapinzani wana uhuru wa kufanya wanavyotaka ingawaje wanalewa sifa na kujisahau mpaka wanamtukana Raisi wa JMTZ pmj na Watz lkn bado wanaishi kwa Amani tu!

Hivyo yaliyotokea Libya hayana sababu ya kutokea TanZania kwa sababu tu fisadi Lowasa na Genge lake wanataka kuleta fujo TanZania, kwanza kwa taarifa yako tu Wazungu hawawezi kumsikiliza fisadi Lowasa na Genge lake hata siku moja!
Ukiwa ccm sijui akili huwa zinaruka, embu rudia nilichokiandika acha kuweweseka, hakuna mahala nimesema Tanzania ni Libya..

Nilichosema ni kwamba "hata Libya waliwahi kuishi kwa amani" kama umeshindwa kujua tafsi ndogo tu ya sentesi hii nikuweke kundi gani?

Unaposoma comment ya mtu funga ubongo wako soma kwa makini uwelewe kilichoandikwa siyo unasoma huku unawaza jinsi ya kubisha.

Kwahali hii sijui tutafika, ninachojiuliza huyu unaempazia sauti na kumuona malaika anakuja kutumikia taifa kwa namna ileile ambayo atakayo chaguliwa mgombea wa chama chochote, akiongoza vibaya maumivu tutayapa kwa usawa uleule sasa yanini kukaziana misuri as if anakuja kutumikia mtaa wenu au nyumbani kwenu pekee..
 
Katika kipindi hiki cha kampeni inatupasa kuwa watulivu sana; kwani mengi yanayosemwa huwa hayana ukweli ndani yake. Kwa taratibu tu za kawaida barua za kikazi [official letters] lazima ziwekwe muhuri husika wa ofisi [lazima ziwe sealed]. Kwa kweli inakuwa ni vigumu sana kuamini barua ya kikazi tena kutoka wilayani isiwekwe muhuri. Kwa jinsi teknolojia ilivyo sasa ni rahisi mno mtu kughushi nyaraka mbalimbali.
 
Tanzania tumeanza kuichoka amani, tunaitwa wapumbavu na malofa! Tunanyimwa uwanjwa kwa shughuli halali kisheria? Naumia sana lakini maamuzi yanakuja pole pole potelea mbali
 
Back
Top Bottom