UKAWA Wapuuzwe!

Acha ujinga wako wewe! Nchi hii ni ya Demokrasia kila mtu ana haki ya kuamini na kufuata anacho penda! Kama mnataka anzisheni radio UKAWA na TV UKAWA muwasifie akina Mbowe,Mbati,Limpumba na Maalim Seif kuanzia asubuhi hadi usku wa manane kwa kila siku
mlengo wa Kati simama hapo Kati Kati usiegemee CCM wala UKAWA chombo cha Habari kazi yake ni kubalance Habari , yaani kinachukua pande zote si kuegemea upande mmoja.
 
Tena sio Millard tu, hiyo radio Clouds yote ni wana CCM, kiongozi wao ndio alipata tenda ya kuaandaa venue ya kufanyia mkutano Mkuu wa CCM uliopita kwa hiyo nyimbo zao ni CCM. Watangazaji karibu wote wako biased sana na wanafagilia sana CCM hawa wanatumiwa hawa na ukizingatia wengi wao ni ma radio DJs sasa sijui kama wanajua ethics za utangazaji kama inavyotakiwa
 
Habari ya wakati huu wana jf?
Mtangazaji maarufu wa cloulds fm millard Ayo,anayefanya kipindi cha amplifaya j3-ijumaa kuanzia saa moja usiku leo katka kipindi chake ameonyesha kutumika na ccm dhahiri, amewapa air time kubwa uvccm Dodoma kupitia kwa msemaji wao paul makonda. Katika tamko lao, paul makonda amelekeza mashambulizi makali kwa UKAWA, hasa Tundu lisu na Prof. Lipumba.

huyu dogo huwa namfatilia sana.nyenendo zake katika kutumia vyombo vya habari kuadres issues mbalimbali hasa za kisiasa ni biased kwa upandewa ccm.anakera sana sana.pamoja na ujana wake anakosa weledi japo wa kung'amua.nimetokea kumchukia hamna mfano.
 
Hivi kama ukawa wanalipwa na Mataifa ya Nje nyie mlieko na dola mko kimya tu?
Pale LOLIONDO MMEPAKABIDHI KWA MTOTO WA SULTANI TWIGA WANAISHA, WANANCHI HAWARUHUSIWI KUFIKA, WANA UWANJA WA NDEGE AMBAO WANARUKA BILA WASIWASI LEO MMESAHAU? Wengine walihongwa suti na waarabu ila ilikuwa sawa jitafakarini la sivyo mlete USHAHIDI WA HAYO MATAIFA YANAYOWATUMIA WAPINZANI KAMA KUNA UKWELI SIO MNAISHIA KUSEMA TU MATAIFA.

Hii ni aibu kwa taifa. Cjui mfumo wa kutoa vibal vya uwindaji uki vip maana kinachofanyika pale loliondo ni aibu kwa taifa. Ila ipo siku
 
...most of you guys need to go for 'Head' checkup. Hivi mnadhani mtabaki madarakani milele? Katiba siyo ya CCM, kama mnataka kutunga ilani yenu watu wa Lumumba haina sababu ya kutumia 'National Resources' kufanya hivyo. Mmejisahau sana.
 
Kuvimbiwa kubaya sana; na hasa kuvimbiwa madaraka! Akina Jaji Warioba na Tume yake nao ni "BAPHOON"? Sidhani kama wewe ni "mkereketwa" au mzalendo kumzidi Jaji Warioba! Kumzidi Dr. Salim Ahmed Salim! Kumzidi Mzee Butiku! Kumzidi Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na Jaji Mkuu Mstaafu Augustine Ramadhan! Sidhani kama una uzalendo kuzidi Tume zote zilizopita za akina Jaji Francis Nyalali, akina Jaji Kisanga, sidhani na haitakaa iwe hivyo.

Wewe u mtoto mdogo sana dogo, tena kinda kweli kweli. Tumia hekima acha kejeli hivi vyeo vinapita, vyama vinapita, taifa linadumu. Anyway, labda kwa sababu unaamini mtatawala milele sio ajabu ukaongea uliyoyaongea. Roma iliyoogofya mataifa ilikuja na kupita itakuwa kundi lenu! Babeli iliinuka, ikastawi, na ikasahaulika itakuwa kejeli zako. Kejeli hazijengi wala haziadabishi zaidi ya kubomoa. Ni ushauri wa bure; una hiari ya kuuchukua au kuachana nao ila wakati ndio utakaoamua.

Mimim mwenyewe nilitaka nimjibu kama wewe! Nikatulia kwanza, nikarudia kusoma uzi wake. Nikarudi kuangalia title yake, nikaamua kumwacha kama alivyo!!
 
MKUU makonda nimepitia uzi wako, kisha nikapitia kwenye hadhara ya watu uliowaita wakusikilize yaani Jf members, nashindwa kuelewa kwa nini karibia wote wamejibu kwa matusi kama ulivoandika kwa matusi.
Mkuu inafaa nyie kama ccm mkae mtafakari je mnapowaruhusu watanzania waanze kuhoji kwa nini viongozi wa taifa ili mnaanza kutukana matusi ni dalili ya kutimiza miiko ya utawala au ni kuchanganikiwa au ni kejeli kwa watanzania?

Nyie mna dola, au kwa ufupi niseme tu mnao uwezo wa kuunda au kubomoa,je kwa nini muanze kutaja matusi sijui bwana za cuf, nccr ,cdm , tume zoote za akina kisanga, warioba na wasomi kuwa wanawatukimia mabwana zao ni hekima? je nyie mnawatumikia mabwana wapi?au wao wana mabwana ila nyie mna nini?

Kiukweli siasa za taifa ili ni za ovyo kabisa. Mkuu makonda, unaridhishwa na tabia za bunge lenu za kutaja matusi mfano kumuita raia mwenzio SHETANI, mara MABWANA, mara KUUKALIA, mara BUSHA, je unahisi watanzania wanasubiri kauli izi kwa hamu?

Mkuu, rais kikwete alizindua rasimu, akakabidhibiwa kwa hafla nzito ya kutumia mamilioni , ikachapishwa na taasisi ya kiserikali kwa gharama za walipa kodi, akawateua nyie mkale kodi zetu, leo hii mnasema alichopokea kwa shangwe na sifa kedekede kilikuwa kiini macho?
Juzi nilikuta cd moja mtaani watu wanasikiliza, ikawekwa kipande cha video jk anahutubia wakati anazindua tume, kikachomekwa kipengele anapokea taarifa na rasimu ya tume, wakakata wakaweka kipengele cha kuzindua bunge ambako anakana sifa zooote alizoimwagia tume...huwezi kuamini kama ni mtu mmoja aliongea matamshi ayo...yaani ya kwanza ni kinume cha ya mwanzo!

Mkuu, sina budi kukufikirisha au kukuudhi, kwa matusi uliyoleta sio ya kujenga bali matusi, ndio maana watu badala ya kukujibu wakatukana pia. mimi siwezi kukutukana ili kujibu ayo matusi ila kiujumla hamjengi taifa mnalioboma.
Niliwahi kuwaambia apo nyuma, kama hamuitaji vyama vya siasa, rais kikwete anao uwezo wa kuamuru vifutwe, turudi kwenye udikteta, ila kama mkikubali ivi vyama viwepo basi wasikilize maana ni wenzenu.binafsi natamani siku moja ivi vyama vyoote ccm, cdm , nk nk vifutwe nchi itulie...udini umeletwa na nyie wanasiasa, ukabila, ukaskazini , uchaga, mfumo kristo, uislamu, ughaidi nk nk ni nyie wanasiasa mnaleta!

Mkuu sitaweza kuendelea kuchangia kwa kuwa apa hatujengi tunabomoa...izi kauli za kuongozwa na jeshi, nk nk ni kama zile za BORA TUKOSE WOTE, hatuachii, wala hatuchukui.
MKUU, kwa ujumla awa wapinzani ni wachache alafu sio wakorofi, wanaongea sana ila vitendo vibaya hawana, nakushauri tu badala ya kuanza ligi na kujiandaa kuua watu kama ulivotangaza kuwa green guard wajiandae, msifike uko, fanya mpango mkae nao muyamalize, uku uraiani wengi hawako na nyinyi , pitia mtaani msikilize mawazo huru, ila mkitaka yale ya kusifiana tu ...mjue mnasifiwa kinafiki ila watu wako katikati na wengi upande wa kushoto.
Ni ayo kwa leo!
 
Mkuu acha kubabaisha watu wewe umeandika nini sasa ni sawa na zero kabisa makonda kaweka andiko lenye mashiko na hoja ndani yake wewe na ubavicha wako unaleta porojo.

Sikushangai kwa hiki ulichoandika hapa. Uwezo wako wa kufikiri umeishia hapo.
 
Wakumbuke hakuna cha milele, wengi walikuwepo leo wako wapi, na wakae wakijua kuna kizazi hakitakuwa na nidhamu ya woga, tutegemee nini??? Ni mtazamo tu.
 
tuanze kuwapuuza watu wa siasa kama wewe ndipo tufanye tathimini ya wanachofanya ukawa.
 
Nimepuuza huu uzi Nimeishia aya ya pili Kama mkuu hajui hata buffoon dah! Hajaangaika hata 'ku-google'.....................naisikitikia Tanzania.
 
Hivi ndugu yangu umesoma shule gani wewe?! Hujui hata chama kinachoongoza Kenya kilikuwa cha upinzani enzi ya KANU madarakani sasa je hivi vyama vilivyopo madarakani Kenya vinanufaisha nchi za nje? Acha kufikiri na kuandika kwa kuwa unataka madaraka, andika kwa kuwa unaelewa usemalo na ni sahihi. UKAWA itapuuzwa na wanaccm waliopo madarakani kimkandamkanda tu, ila wenye kujielewa hawataipuuza kamwe.
 
Hapa naona Bwana Makonda ameteleza. Katika kiingereza hakuna neno BAPHOON bali kuna neno BUFFOON. Ni bora atumie lugha anayo iweza!

A buffoon is someone whose ridiculous behavior is a source of amusement to others. People you might call a buffoon are a political rival or the guy at work who tells silly jokes at office parties.
 
View attachment 152855
Leo Nitatumia maneno makali kidogo ili tuelewane kiurahisi. Wapinzani wa Nchi hii ni "BAPHOON". Maana ya BAPHOON ni Watu au Kundi la Watu linalotumika Kwa Maslahi ya Mataifa Mengine Kuangamiza Taifa Lao. Wako Tayari Hata Kuchukua Mabomu na kulipua Nchi yao Wenyewe. Hawa ndio wanaojiita UKAWA (THE BAPHOON)

Imani namba Tano na namba nane za Chama Cha Mapinduzi kwa pamoja zinasema:
Cheo ni Dhamana, sitatumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu na Nitasema Kweli Daima Fitna kwangu Mwiko.

Kwa tafsiri ya Imani ya Chama tunakubaliana na maneno ya Mwanahistoria wa zamani wa Uingereza Lord Acton aliyewahi kusema;

“Power tends to Corrupt, and absolute power corrupts absolutely. Great men are almost always bad men”

Yakimaanisha kuwa;

“Madaraka yana tabia ya kuwaharibu walio nayo, na wenye madaraka makubwa Zaidi huharibika Zaidi kwa kuwa hata watu wema hugeuka kuwa wabaya wakishakuwa na madaraka”


Na sisi Vijana Wazalendo tunasema;

“Watu wenye Madaraka Makubwa Wakiharibiwa na hayo madaraka hulewa hayo madaraka na kuanza hata kutukana kudharau waliowapa madaraka hayo. Lakini wenye madaraka makubwa wanaojua kuwa madaraka yao ni dhamana, kwanza huwa wapore na wanyenyekevu na hubeba dhamana kubwa ambayo wao huona madaraka hayo ni Mzigo wala si zawadi.”

Wapo wanaodhani kuwa Vyama vya Upinzani vipo kwa ajili ya Maslahi ya Taifa. Wapo wanaodhani Vyama vya Upinzani ndio mkombozi wao. Na wapo wanaodhani muarobaini wa matatizo ya taifa hili ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ni vyama vya Upinzani. Ukweli halisi wamepotoka sana. Vyama vya Upinzani vipo kwa maslahi yao tu na vimekuwa ni dhaifu kiasi haviwezi kuaminiwa kupewa dhamana ya Uongozi wa Taifa hili.

Hatuna haja ya kuwaambia BAVICHA waombe radhi kwa matamshi yao yasiyo na adabu waliyoyatamka jana dhidi ya Rais wa Jamhuri na Waziri Mkuu kwa sababu tunajua wanadhani wako sahihi. Lakini tunajua wanajua hawako sahihi na wanafanya hivyo ili kuwaridhisha mabwana zao ambao wanawatumia wao kutengeneza mitaji yao kisiasa. Wao wanabaki tu kama kigenge fulani ambacho kama kikiachwa kikue na uwongo wake mwishowe kitaaminiwa na hapana shaka nchi hii ipo siku itaongozwa na Vichaa.

Tuelewe Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ndiyo Lulu pekee iliyobaki Afrika ambayo imeundwa na sisi wenyewe , kwa hiari yetu wenyewe baada ya kukomboa sehemu zake mbili kutoka katika Ukoloni. Haiwezekani tuache Muungane uchezewe tu na wachache wetu ambao kinachowasukuma ni Uroho tu wa madaraka.

Tulipoanzisha Mfumo wa Vyama vingi, tulidhamiria kuwa na vyama vyenye nguvu za dhati ambazo ama zingekuwa kubwa kuliko CCM ili kuweza kuiwajibisha serikali sawasawa nayo iwajibike moja kwa moja kwa ujenzi wa taifa. Miaka 21 baada ya kuwa na mfumo wa vyama vingi, tumekuwa na vyama legelege ambavyo havina dira wala mwelekeo badala yake vimejikita katika uchochezi na ulaghai. Hali hii inatupa wasiwasi kama kweli hivi ni vyama vya siasa ama ni vikundi tu vya harakati vinavyofanya siasa. Watanzania wako tayari kuamini Upinzani lakini si kwa miaka hii ya karibuni,ni mpaka tutakapopata vyama vyenye nia thabiti ya kuleta maendeleo ya nchi hii huku vikithibitisha kwamba vitadumisha muungano wa nchi mbili serikali mbili na kuheshimu Katiba ya Nchi.

Chama Cha Mapinduzi kinabaki Imara na Msimamo thabiti wa Kuendelea na Jamhuri Muungano wa nchi mbili na Serikali Mbili. Azimio la kutaka serikali tatu si mara ya kwanza sasa. Azimio kama hili lilikuwepo Mwaka 1993 kwa hoja Binafsi ya Wabunge 55 (G55) iliyopelekwa na Mh. Njelu Kasaka Mbunge wa Chunya. Kwa kikao Cha Bunge cha August 24-27, Bunge liliridhia mchakato wa kuanzisha serikali ya Tanganyika. Lakini kwa Uthabiti wa CCM ambao ni imara sana sasa kuliko mwaka 1993, kilisimamia mfumo wa kubaki na Muungano wa Nchi mbili na Serikali Mbili. Msimamo wa CCM wa Mwaka 1993 ni thabiti sana sasa, hatuwezi kufufua Tanganyika isipokuwa tutatumia mfumo uliopo kutatua kero za Muungano zilizopo. Changamoto kubwa zinazotukabili ni za kiuchumi kuliko zilivyo za kijamii na muungano wetu sana una nia thabiti ya kijamii kuliko uchumi.

Demokrasia imechukua njia hadi sasa hata mifumo ya demokrasia imeanza kupuuzwa. Nasema inapuuzwa kwa sababu hata Vichaa sasa wanaweza kuamka tu na kutoa matamko yasiyo na kichwa wala Miguu. BAVICHA ni Vijana wadogo sana ambao hawawezi kuamka na kutoa matamko waliyoyatoa ila kwa kutumwa na Bwana zao. Na hao Bwana zao wanafadhiliwa na Mataifa ya nje ambay hayataki kuona siku moja AFrika inaungana na kuwa taifa moja kubwa. Namna pekee ya kufanikisha uovu huo mkubwa dhidi ya Afrika, ni kuibomoa Tanzania, na wenzetu hawa wapinzani wamekubali kutumika kama vibaraka wa kudidimiza Afrika.

Hatuoni Sababu ya Kukaa Kimya, Sitanyamaza kufumbia macho Ujinga huu. Nani kawatuma BAVICHA kutoa Matamko dhidi ya Rais na Waziri Mkuu? Nani kawadanganya kuwa eti Mchakato wanaoutaka UKAWA ndio Mchakato wanaoutaka Wananchi?

Unamsikiliza Mh. Lipumba, amejawa maneno kinywani mwake ya uchochezi tu wa kidini na ubaguzi wa wazi kabisa. Hizo zote ni hila ambazo kama zisipodhibitiwa kwa kuelezwa ukweli wake kama hivi, taifa litaangamia. Tumedhamiria kupambana na hili, hatutakaa kimya Mpaka watanzania watuelewe na wawapuuze wapinzani kwa lugha zao za uchochezi.

Kwa Nini wakatake kufanyia Mkutano Zanzibar kibanda Maiti na Si Dodoma maana wote walikuwepo hapa? Hivi wapi ni Karibu, Iramba kwa Tundu Lisu au Zanzibar (Unguja Kibanda Maiti)? kuna Umbali gani Hai kwa Mbowe au Tabora kwa Lipumba au Vunjo kwa Mbatia ukilinganisha na Zanzibar? Hawa waheshimiwa wasitake kulaghai Umma, kuna ajenda wameibeba ambayo hawataki kuisema. Warudi Bungeni waje wajenge hoja maana Katiba haitapatikana Majukwaani bali kwa kukamilisha Mchakato Bungeni na ndicho CCM tutakachofanya. Tunaendelea na Bunge na tunakamilisha Mchakato hata wasiporudi.

Ikiwa wao ni vyama vya kidemokrasia na nia yao ni kujenga demokrasia, kwa nini hawataki kukaa meza ya Mazungumzo? kwa nini wakimbie mkutano halali wa kidemokrasia wasikae hapo wajenge hoja hapo badala yake wanakimbilia eti kwenye mikutano ya hadhara? Hapo kuna walakini na demokrasia wanayohubiri. Anayehubiri demokrasia lazima awe wa kwanza kukaa meza ya mazungumzo. Mumewasikia wakitoa matamko kwamba hawako tayari kukaa meza ya mazungumzo na serikali wala CCM, hawa ni washari na wanatangaza shari na kisha wanatafuta huruma ya wananchi. Hiyo siyo demokrasia ni Vurugu. Uhuru bila mipaka i vurugu na Demokrasia bila Utaratibu nayo ni vurugu.

Tunazo tetesi kuwa hivi vyama vinafadhiliwa na wasiotaka kuiona Afrika ikiungana na kuwa jumuiya moja kubwa yenye nguvu. wanatafuta ucku na Mchana kuisambaratisha Afrika na namna pekee ye kuisambaratisha Afrika ni kuisambarataisha Tanzania kwa maana Tanzania ndiyo kinara wa Umoja wa Afrika. Kutumiwa kwao na Ukibaraka wao uendelee lakini tuko imara sana kulinda Muungano wetu. Hawa ni BAPHOON.

Lugha za kichochezi za wapinzani wananchi wamezisikia. Wamemsikia Prof. Ibrahim Lipumba akiweka matabaka ya watu kwa sababu za Kidini, wamemsikia Tundu Lisu akipandikiza chuki dhidi ya Mwalimu Nyerere na waasisi wa Muungano, Mumewasikia viongozi wa CUF, NCCR Mageuzi, wakifanya juhudi za kufitinisha watanzania kwa kauli zao ovu. Ufitini wa aina yoyote, uwe wa kidini, kikanda, kikabila au haiba ya watu hauna budi kupigwa vita kubwa na kila Mtanzania mpenda amani.

Wakumbuke, Chuki wanazozijenga sasa, itafika mahali zitakomaa na zikishakomaa zitaanza kuwa mwiba mkali kwao wao wenyewe. Kwa maana wakifanikiwa kupanda mbegu ya chuki miongoni mwa watanzania kwa namna yoyote ile, hakuna namna ambayo hao waliowapandikiza chuki watawapenda wao. Chuki yao itawala wao wenyewe na itaangamiza taifa. Hatuwezi kuacha hili litokee tukiangalia kwa macho yetu.

Taifa halitajengwa na watu waoga wala waongo na wafitini. Watanzania wenzangu tujikite katika kujenga uchumi na kujiletea maendeleo kwani tukiendelea kuwasikiliza "BAPHOON" hawa na kuacha shughuli zetu za kiuchumi, ni kujipotezea fursa tulizo nazo kwa faida ya wengine. Hawa wanawasumbua nyie mwasikilize, wao shughuli zao za NIGHT CLUBS, GUEST HOUSE ZAO, BAR ZAO, CASINO ZAO, DALADALA ZAO, MAHOTEL, na BIASHARA ZAO NYINGINE zinaendelea kuwaingizia Pesa na wanachofanya ni kuwajaza matumaini ya uwongo huku wao wanajaa MAPESA. Kwa kuwa wameamua kutumika na mataifa ya nje kuhujumu nchi yao, bado wanalipwa kwa kazi yao ya UFITINI. Mapato yao hayayumbi na wala hayatayumba.

Ewe Mtanzania Mwenzangu, Shtuka, Achana na BAPHOON.

Mungu Ibariki Tanzania
Paul C. Makonda
Katibu Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM
Mjumbe Bunge Maalum la Katiba

0716696265
Paul Makonda ni kichwa sana. Hongera sana. Vijana tumekuelewa hawana lao wanafiki hawa
 
Back
Top Bottom