UKAWA vs CCM katika urais, piga Kura hapa

UKAWA VS CCM KATIKA URAIS

  • UKAWA

    Votes: 757 85.2%
  • CCM

    Votes: 118 13.3%
  • NONE OF THE ABOVE

    Votes: 13 1.5%

  • Total voters
    888
Status
Not open for further replies.
Habari wakuu..
Natumai mu wazima..uzi huu ni maalum kwa hawa washabiki wa ukawa...unajua tatizo kubwa ukawa ina mashabiki vijana hasa wa mitaani na pia wanaoshinda mitandaoni....hembu ongeeni fact yani kutwa kucha ni kumsifia lowassa lakini ukiulizwa lipi zuri alilofanya huna lakujibu ila kuongea tuuh bwana mmebarikiwa...sikatai lowassa ni kiongozi mzuri tuu sana anafaa sana kuongoza lakini hafit hata kidogo kuwa rais wa nchi hii...Ana uchu wa madaraka uliopitiliza....hembu niambieni sababu kubwa ilomfanya lowassa kuhama from ccm to chadema...kweli kukatwa tuuh ndo kumsababishe akisaliti chama kilichomlea?? kwani ikulu kuna nn kinachokimbiliwa kiasi hcho mpaka watu kutaka kutoana roho??? Kwa mara nyingine tena em mfikirieni huyu mgombea wenu na sera zake....
Ametoa maji ziwa victoria na kuyasambaza kahama na maeneo mengine mengi ambapo awali yalikuwa kama jangwa.

Amejenga chuo kikuu cha UDOM

Amejenga shule za kata yaani hizo idea zilikuwa zake kama Lowassa na sio za kikwete ndani ya miaka 2 tu ya uPM

Pia kamata gazeti lako la KULIKONI la jana August 7 ujipatie utafiti uliofanyika na taasisi ya masuala ya kijamii kwenye mikoa zaidi ya nane Lowassa atapigiwa kura na wanaccm 60% mbali na UKAWA.

Hapo jifikirie.
 
Habari wakuu..
Natumai mu wazima..uzi huu ni maalum kwa hawa washabiki wa ukawa...unajua tatizo kubwa ukawa ina mashabiki vijana hasa wa mitaani na pia wanaoshinda mitandaoni....hembu ongeeni fact yani kutwa kucha ni kumsifia lowassa lakini ukiulizwa lipi zuri alilofanya huna lakujibu ila kuongea tuuh bwana mmebarikiwa...sikatai lowassa ni kiongozi mzuri tuu sana anafaa sana kuongoza lakini hafit hata kidogo kuwa rais wa nchi hii...Ana uchu wa madaraka uliopitiliza....hembu niambieni sababu kubwa ilomfanya lowassa kuhama from ccm to chadema...kweli kukatwa tuuh ndo kumsababishe akisaliti chama kilichomlea?? kwani ikulu kuna nn kinachokimbiliwa kiasi hcho mpaka watu kutaka kutoana roho??? Kwa mara nyingine tena em mfikirieni huyu mgombea wenu na sera zake....

Tofauti ya EL,MWANDOSYA,NCHIMBI,KIMBISA,KINGUNGE etc ni kwamba yeye amehama,wao wamebaki wakiwa na 'dukuduku' lao.
 
UKAWA. mods nijazie hilo jibu kwenye poll maana simu yangu ya mchina imegoma kunipa option ya kuvote. Lowassa atosha!
 
Uuuuwwwiiiiii jamani naichukia sisiem haya majitu ni kuyakimbiza na nondo kabisaa
 
Wanajamvi!
Tuko katika kipindi ambacho mijadala mikubwa katika maeneo mengi hapa nchini ni suala la uchaguzi mkuu na hasa katika nafasi ya urais. Inavyooneka ni kwamba mmoja kati ya Lowasa au Magufuli atashinda nafasi hii kubwa ya uongozi hapa nchini. Hii ni kutokana na mijadala na mivutano ya wengi iko juu ya hawa watu wawili.

Magufuli amekuwa akitajwa na wengi kwamba ni mchapa kazi lakini pia ni mtu anayesimamia sera na sheria lakini anatoka katika chama ambacho kwa miaka mingi kinatuhumiwa kwenye suala la ufisadi na kushindwa kuwa na vipaumbele katika suala la maendeleo ya taifa letu na mahitaji ya wakati huo. Kwa hiyo kuna watu wanaoona kuwa sasa hivi kipaumbele kiwe ni kuitoa CCM madarakani bila kujali mgombea wao ni mtu wa aina gani.

Lowasa pia amekuwa akitajwa na watu wengi kuwa ni mchapa kazi na mtu mwenye maamuzi magumu (sijayajua haya maamuzi magumu ni yapi, huenda ni kujiuzuru uwaziri mkuu ndo maamuzi yenyewe magumu). Kwa upande mwingine Lowasa amekuwa akitajwa mara nyingi sana kwa suala la ufisadi (sijui kama ushahidi upo au haupo) na hata matumizi makubwa ya pesa katika harakati za kuusaka urais. Huyu ndiye mgombea wa urais aliyesimamishwa na Chadema na hata UKAWA nzima imekubaliana. Chadema na UKAWA nzima siku zote wamekuwa msitari wa mbele kupiga vita ufisadi na kumtaja Lowasa kama Fisadi hali inayowafanya baadhi ya watu washindwe kuiamini tena chadema katika yale wanayoyasema siku zote hasa pale wanapojitokeza leo na kusema "Lowasa siyo fisadi".

Mimi ni mmoja wa watu waliobaki njia panda ya kufanya maamuzi ya "nimpigie nani kura ya urais". Naomba tujadili kwa pamoja bila ushabiki kwa masilahi ya taifa letu, kizazi chetu na kizazi kijacho; Ni lipi bora, kumchagua Lowasa na tuhuma zake zote akiwa Chama kinachopiga vita ufisadi au kumchagua magufuli ambaye hana tuhuma za ufisadi (kama anazo hazijulikani sana) lakini anatoka chama kinachotuhumiwa kwa ufisadi?
 
wadau wa jukwaa hili, napenda mtoe michango yenu katika mpambano huu wa wagombea hawa wawili wa urais, John Magufuli kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) niliyemuita JM na Edward Lowassa wa Ukawa niliyemuita ED mpenda urais ili kupitia kura za yupi anafaa kuwa rais zitawasaidia Watanzania kumchagua rais anayefaa kuliongoza taifa letu hapo Oktoba 25 mwaka huu.
Viongozi hao kila mmoja ana sifa zake lakini yupo ambaye anamzidi mwenzake. Kwa kuanza, mimi kwa asilimia mia moja kura yangu ya ndiyo itakwenda kwa Magufuli kwa sababu hana kashfa kama alivyo Lowassa ambaye kwa asilimia kubwa ana kashfa za ufisadi ikiwa ni pamoja na kuwaletea usanii Watanzania enzi akiwa waziri mkuu aliposema kwamba angetuletea mvua za kutengeneza. Huo ulikuwa ni usanii wa hali ya juu. Haya uwanja upo wazi.
 
Lowassa afya mgogoro, kashfa za ufisadi toka kwa Dr. Slaa hatujasahu. Pia amejidhihiri kuwa ni mwenye uchu wa madaraka na mpenda urais kwa gharama yoyote ile. Akiwa raisi ataiuza nchi yetu na pesa anazotumia kuutafuta urais ni dhahiri wakuogopwa kama ukoma.
 
Lowassa afya mgogoro, kashfa za ufisadi toka kwa Dr. Slaa hatujasahu. Pia amejidhihiri kuwa ni mwenye uchu wa madaraka na mpenda urais kwa gharama yoyote ile. Akiwa raisi ataiuza nchi yetu na pesa anazotumia kuutafuta urais ni dhahiri wakuogopwa kama ukoma.

Wewe umepima ?. Usihukumu . yakaja kukukuta ya john Kombe. Yule muimbaji wetu toka mchinga
 
Lowassa kawanunua matahila ikiwa yanatambua ni moja ya watu janga la taifa
 
wanajamvi!
Tuko katika kipindi ambacho mijadala mikubwa katika maeneo mengi hapa nchini ni suala la uchaguzi mkuu na hasa katika nafasi ya urais. Inavyooneka ni kwamba mmoja kati ya lowasa au magufuli atashinda nafasi hii kubwa ya uongozi hapa nchini. Hii ni kutokana na mijadala na mivutano ya wengi iko juu ya hawa watu wawili.

Magufuli amekuwa akitajwa na wengi kwamba ni mchapa kazi lakini pia ni mtu anayesimamia sera na sheria lakini anatoka katika chama ambacho kwa miaka mingi kinatuhumiwa kwenye suala la ufisadi na kushindwa kuwa na vipaumbele katika suala la maendeleo ya taifa letu na mahitaji ya wakati huo. Kwa hiyo kuna watu wanaoona kuwa sasa hivi kipaumbele kiwe ni kuitoa ccm madarakani bila kujali mgombea wao ni mtu wa aina gani.

Lowasa pia amekuwa akitajwa na watu wengi kuwa ni mchapa kazi na mtu mwenye maamuzi magumu (sijayajua haya maamuzi magumu ni yapi, huenda ni kujiuzuru uwaziri mkuu ndo maamuzi yenyewe magumu). Kwa upande mwingine lowasa amekuwa akitajwa mara nyingi sana kwa suala la ufisadi (sijui kama ushahidi upo au haupo) na hata matumizi makubwa ya pesa katika harakati za kuusaka urais. Huyu ndiye mgombea wa urais aliyesimamishwa na chadema na hata ukawa nzima imekubaliana. Chadema na ukawa nzima siku zote wamekuwa msitari wa mbele kupiga vita ufisadi na kumtaja lowasa kama fisadi hali inayowafanya baadhi ya watu washindwe kuiamini tena chadema katika yale wanayoyasema siku zote hasa pale wanapojitokeza leo na kusema "lowasa siyo fisadi".

Mimi ni mmoja wa watu waliobaki njia panda ya kufanya maamuzi ya "nimpigie nani kura ya urais". Naomba tujadili kwa pamoja bila ushabiki kwa masilahi ya taifa letu, kizazi chetu na kizazi kijacho; ni lipi bora, kumchagua lowasa na tuhuma zake zote akiwa chama kinachopiga vita ufisadi au kumchagua magufuli ambaye hana tuhuma za ufisadi (kama anazo hazijulikani sana) lakini anatoka chama kinachotuhumiwa kwa ufisadi?
hoja yako inanuka mavis!!!!!gamba wewe. Ukawa ushindi lazima!!!nchi ilikwisha uzwa na ccm sasa tunaikomboa!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom