Ukatili huu!!

"Asiye na dhambi awe wa kwanza kurusha jiwe!"

Hivi kweli, kwa wakati huu, enzi hizi, zama hizi, kuna mtu MSAFI duniani? Leo nimeambiwa kwamba hata Mapadri wanawatongoza wanawake. Nimeambiwa na mtu ambaye ni Mkatoliki.

Mimi niliuliza: Wanawatongozaje?

Yeye akajibu: Wanawatongoza tu, kama wanaume wengine!

Nikajibu: Makubwa!

Sasa sisi tunatekeleza Sharia, kumwua mtu ambaye HAJAHUKUMIWA kifo, kwa kuwa tu "amedaiwa" kuwa mwizi au kibaka. Watu wangapi wameshapoteza maisha yao kwa kupigiwa ukunga "Mwizi huyoooo.... mwizi huyooooo..... kamataaaaa.... pigaaaa.... uaaaaa!", na baadaye yule ambaye alipiga ukunga, baada ya mauaji kufanyika, anakwenda pale na kumkuta mtu ambaye HAMTAMBUI wala hajawahi kumwona, na kama ndiye aliyemhusu kuwa "mwizi", basi siye! Anaanza kujutia, anamwomba Mungu amsamehe, lakini kwa dhambi hiyo.... Mwe!

Nakumbuka, kama sikosei, mwaka jana, mtoto wa mchezaji maarufu wa soka, Mtwa Kihwele, aliuwawa wakati akidamka kutoka nyumbani kwake alfajiri, akielekea kwenye biashara zake Kariakoo. Kijana huyo alikuwa na mazoea ya kuwahi dukani kwake kisha kuendelea na shughuli zake nyingine. Alipofika kwenye nyumba fulani iliyopo mitaa ambayo ni karibu na nyumbani kwake, Ilala, mwenye nyumba ambaye alikuwa akitizama dirishani akamwona akipita, akadhani kwamba ni mwizi. Akaanza kupiga kelele. Ilikuwa alfajiri, kati ya saa 10 na 11, hivyo watu wengi walikuwa bado hawajaamka. Kelele zikawatoa usingizini, wakaanza kumpiga kijana wa watu hadi kumwua, BILA HATA YA KUULIZA KULIKONI!

Hii ndiyo imekuwa hulka yetu kwa sasa.

Ndio, mimi nimewahi kuathirika na vitendo vya wizi. Mwaka jana, mwezi wa pili, tuliingiliwa nyumbani, walivunja grill ya dirisha, wakaingia ndani, wakakomba vitu vingi sana. In fact, walinifilisi, kwani vitendea kazi vyangu vyote viliondoka. Si tu kwamba nilipoteza "data" zangu zote kwenye external hard disk mbili ziliokuwa mezani, bali pia, iliondoka computer aina ya Apple iMac, laptop, home theatre, printer, na kadhalika.

Hakuna aliyepatikana, kwani wizi ulifanyika kwa ustadi mkubwa, kiasi kwamba wote tuliokuwa ndani ya nyumba hatukusikia lolote.

Nina uchungu wa kuibiwa, lakini KAMWE siwezi kuchukua hatua ya kumpiga jiwe na kushiriki mauaji ya mtu ANAYEDHANIWA tu kuwa mwizi au kibaka. Kabla ya kufanya hivyo, lazima nijiulize:

1. Nina ushahidi usiopingika kwamba mtu huyo kweli ni mwizi au kibaka?

2. Je, nina mamlaka gani ya kisheria kumhukumu mtu adhabu ya kifo?

3. Je, kama ikigundulika kwamba mtu huyo hakuhusika na madai hayo, nitakuwa mgeni wa nani mbele ya Mungu?


Kumbukeni, enyi wanadamu: Haki ya kutoa maisha ya binadam ni ya Mungu pekee, kwani yeye ndiye anayeumba, na yeye ndiye anayetwaa! Sisi HATUNA HAKI ya kufanya kazi ya Mungu, HATA SIKU MOJA!

Kumbukeni Amri Kumi za Mwenyezi Mungu. Kumbukeni, msije kujikuta kuwa WAPANGAJI WA KUDUMU wa Jahanam, siku ya Kiama, siku ya Hukumu ya Mwisho!

-> Mwana wa Haki

P.S. Mimi si mchungaji, imamu, sheikh au kasisi... lakini ninampenda, ninamtii na ninamwogopa Mwenyezi Mungu. Kila nitendalo - hata kama najua ni kosa - lazima nimweke yeye mbele kwanza. Mtangulizeni Mungu katika kila jambo lenu, kwa Amani na Upendo, Mtafanikiwa!
 
Washenzi hawa, hamna lolote zaidi ya kuonea Wanyonge.

Kama mna ubavu si mkamtwange Rostam Azziz au Lowassa?

Kuna mama Mkapa pale anadunda na Wahindi kibao wakiwa na pesa za EPA.

Mramba na kundi lake wapo tu. Chenge ndiyo kwanza anagonga dada zenu na mnamchekea.

Mnakuja kupiga mawe Kibaka aliyelala njaa jana. Hamna maana kabisa. Si usiku mtoke mpambane na Majambazi?

Au mkisikia cha moto Mnazifyata? Kunguru Dume nyie.......

Si ajabu kama si akina Lowassa na CCM kumpe njaa kijana, asingeliiba. Mnaadhibu siye. Mnakata Majani na si Mzizi.

Hawa watu ningekuwa na uwezo ningewafilisi kabisa. Majangili wakubwa wa uchumi wa nchi yetu. Halafu Kikwete anawapigia kampeni, jamani hivi WaTZ nani katuloga mpaka tumpe kura yetu Kikwete? Yaani kwa lugha nyepesi anatuambia kuwa ataendeleza wizi wa mali za nchi yetu na wimbi la umaskini kuendelea kushamiri. Tuamke usingizini tuseme hapana kwa Kikwete.
 
i think mtu kama lowasa ndo alitakiwa awe pale chini,masikini ya mungu ukute aliiba kuku tu!
 
Back
Top Bottom