Ukatili huu!!

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,578
8,600
Jamani wewe unapopita mahali ukakuta watu wanampiga kibaka aliyekwapua simu wanamfanyia ukatil huu wewekama mwa JF unafanya nini??


attachment.php
 

Attachments

  • ukatili.jpg
    ukatili.jpg
    75.8 KB · Views: 478
wawakumbatie wawabusu jaman si kuwapiga
then unampa chai anakunywa unamsindikiza kwake
 
Wazee mie nitakuwa different kidogo maana yamenitokea haya mambo 2009 nilipokuwa likizo homeland Bongo,jamani nilikuwa na gf wangu niko beach huko Kigamboni,tukiwa tumekaa jioni hivi kigiza kikianza walitokea jamaa 6 hivi wakawa poa tu ila mie nilishtukia deal nikamwambia bibie tuondoke ghafla walitoa visu na mapanga utadhani mie na mihela sana,wakanisearch kila mahali hadi walitaka kumbaka msichana wa watu,thank God nilikuwa ngangari ingawa walinijeruhi sana,Shukru mungu nilimpiga mmoja mwenye panga so nikalichukua wakakimbia zao ila walipora kila kitu...we acha tu...nikiona walahi ndo kwanza nanunua mafuta ya taa wachome kabisa.
 
Utauona ni ukatili kama hujawahi kufikwa na mabo haya.Utaona kuwa ni shangwe na matumaini kama ushafikwa au kuonja ladha ya kuibiwa.usiombe kabisa ukutane na wananchi wenye hasira!!!!!
 
Duniani kuna mambo huyu bwana kama alipona atakuwa na roho ka ya paka. Ujue pipo are stressed na mambo mengi so ikitokea kama hii basi kila mtu anamaliza stress yake!
 
i wish the same spirit ya ushirikiano huu wa kuua wezi ungetumika kuondoa uongozi wa kifisadi, kimabavu na ukiukwaji wa haki za binadamu hapo tarehe 31 oct. huwa wanaitwa wananchi wenye hasira but hizi hasira ni za vibaka tuuu, na haiihitaji degree kugundua kwamba vibaka wanaongezeka kwa sababu ya mfumo mbovu wa siasa na serikali isivojari makundi husika. HAKUNA MTOTO ANAYEZALIWA GENETICALLY MWIZI AU CHANGUDOA HATA KAMA BABA YAKE NI JAMBAZI. Thanks....
 
huu ni ujinga na kutostaarabika

jamii ilioendelea inajua thamani ya uhai na ina heshimu haki ya kuishi

tujitahidini kuelemisha watu wetu kuhusu thamani ya uhai na kufata sheria

kila kosa lina adhabu yake lkn sio kifo
 
Watu wanachukua sheria mkononi bse hawana imani na police.
Police wangekuwa seriuos na hao watu khali isingekuwa ivyo
 
Kuna siku moja nilikua napita mitaa ya kariakoo, basi kijana mmoja alikwapua simu ya dada fulani (simjui jina). Huyo dada alipiga mayowe! Watu wakatokea....mwizi akachomoa kisu....oh masikini weeeeeeeeeeeeee......alipigwa na jiwe kichogoni...akadondoka chini.....wakati anagaagaa....jamaa mwingine alibeba jiwe kubwa sana akamdondoshea kichwani......kichwa kilipasuka na ubongo ulitoka.....siku hiyo nilijuta kwanini niliona kitendo kile. na nilisikitika sana!
 
Mtu kupoteza uhai kwa simu yako kweli?

hii ni sign wa umasikini wa fikra...uhai ni kitu kingine..nchi haina sheria au sheria hazieleweki?

mfumo mmbaya wa CCM unapelekea haya yote..nchi inahitaji mabadiliko sehemu nyingi sana ila zoezi la kwanza ni kuwabadilisha wananchi kifikra na kuwapa mbinu ya kujikwamua na hali ya umasikini unaochangia kutokuwa na fikira za busara
 
Utauona ni ukatili kama hujawahi kufikwa na mabo haya.Utaona kuwa ni shangwe na matumaini kama ushafikwa au kuonja ladha ya kuibiwa.usiombe kabisa ukutane na wananchi wenye hasira!!!!!

Hasira za wananchi haipashwi kuwa warrant ya watu kuua wenzao ovyo ovyo namna hii. Kesho mtu akikuchukia na akakupigia kelele za mwizi, na kwa mazingira tuliyoyatengeneza ya kusifia wananchi wenye hasira, watu watakuja na mawe wakuue bila hata kuuliza umeiba kitu gani!!! Siamini hata kidogo kwa comments zitokazo kwa baadhi ya watu humu wakati huo huo wanasema wanataka utawala wa sheria. Utawala wa sheria uanzie hapa kwa vibaka kufikishwa polisi then mahakamani lakini sio kwa kuwaua. Hivi kweli mtu anapashwa apoteze uhai wake kwa sababu tu amekwapua simu? Adhabu hii inawasitahili wezi wa Fedha za EPA sio hawa vibaka wenye njaa wanaotafuta jinsi ya kupitisha siku.

Tiba
 
Nakubaliana kuwa huu ni ukatili mkubwa sana. Ijapokuwa kuna watu tumeshaibiwa sana hata vitu ambavyo tumevipata kwa taabu ila adhabu ya kutoa roho ya mwanadamu mwenzetu kwa kosa la kuiba hailingani kabisa na kosa alilofanya. Muhimu ni watawala wetu kuwa na mikakati madhubuti ya kutuongoza katika kukabiliana na umaskini na kutoa elimu kwa vijana sio kuwaacha wanazurura vijiweni bila kazi yeyote. Hivi sheria za nchi yetu zinamlindaje mtu kama huyu? Hata siku moja roho ya mwanadamu hatuwez kuihalalisha itoke kwa kuiba simu. Hii haikubaliki.
 
Back
Top Bottom