Ukame, upungufu wa mvua, na njaa, Je, Serikali haikufahamu?

Ngereja

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
798
333
Tatizo la ukame na njaa ambayo ni matokea ya ukosefu wa mvua za kutosha katika baadhi ya maeneo hapa Tanzania, linatokana na athari za hali ya klimatolojia (Climate effects) hasa kupoa kwa maji ya bahari kwenye maeneo ya bahari ya Pacific, hali ambayo hujulikana kitaalamu kama La Niña. Utabiri wa kutokea kwa hali hii ulitolewa na vyombo mbalimbali vinavyofuatilia masuala ya hali ya hewa, chakula na majanga ya ukame. Taarifa hizi pia hutolewa kwa mamlaka za Serikali husika kama vile Wizara zinazohusika na masuala ya chakula, kilimo, maafa na maji.

Utabiri wa kutokea majanga haya ulitolewa tangu mwezi septemba mwaka 2010. Kituo cha utoaji tahadhari ya njaa na ukame (Famine Early Warning System Network - FEWS-NET, chenye vituo kadhaa ikiwemo Nairobi-Kenya kwa nchi za Africa Mashariki na pembe ta Africa. Kilitoa tahadhari na taarifa ambayo inapatikana hapa http://www.fews.net/docs/Publications/La_Nina_Brief_East Africa_Sept_2010_final.pdf

Suala la kujiuliza, ni kwamba, viongozi wetu akiwemo Rais, wanataka kutuambia kwamba suala hili la ukame na ukosefu wa maji limewashtukiza na hawakuwa wamejiaandaa kukabiliana nalo. Kitu ambacho si kweli, kwa kuwa hata mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) watakuwa walifahamu na walitoa taarifa kwa serikali na wizara zote zinazohusika.

Ukisoma taarifa hii, utaona kwamba maeneo yale ambayo, yanahusika kwa kiasi kikubwa kama vyanzo vya maji kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme, yanahusika. Siamini kwamba hata TANESCO hawakuwa na uelewa wa kutosha katika kutafsri taarifa hii kama walikuwa nayo.

Nato hoja.
 
Dr Idris akiwa bado MD wa Tanesco alionya serikali, kuwa nchi itakuwa kwenye giza, na kuishauri ichukue hatua za dharura kunusuru nchi na balaa hili
 
Back
Top Bottom