Ukabila/ubaguzi wazuia wananchi waliyopokwa mashamba kwa matumizi ya jeshi kulipwa fidia monduli

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,484
7,293
Eneo la lolkisali monduli awali lilitengwa kwa matumizi ya jeshi enzi hizo waziri mkuu akiwa edward sokoine. Baada ya miaka kadha ikaonekana na serikali wananchi wanaweza kupewa eneo hilo kwa kilimo. Wapo wananchi walipewa rasmi na kupewa hati za umiliki ili kufanya kilimo kikubwa kwenye eneo hilo. Baada ya wamiliki kuwekeza na kufanya kilimo kwa miaka kadhaa serikali baada ya kuona mahitaji ya jeshi wakatwaa tena sehemu hiyo. Tangu mashamba hayo yatwaliwe tena kwa matumizi ya jeshi ni zaidi ya miaka ishirini. Wenyewe wamekua wakidai fidia miaka yote huku kwa misingi ya ukabila na ubaguzi halmashauri ya monduli wakiwa wakipiga vita wenyewe kulipwa fidia. Baadhi ya wenyeji kwa msingi wa ukabila tu wamekua wanapinga wenye hati halali za umiliki mashamba eneo hilo la lolkisali kulipwa fidia eti sio watu wa monduli. Hawajui au wanapinga kwamba mtanzania anaweza kumiliki ardhi popote nchini? Ni hawahawa wenyeji wa monduli na wilaya zingine za wamasai wamekua wakizurura na mifugo yao nchi nzima wakidai haki yao kama watanzania.
 
Back
Top Bottom