Ujuzi wa lugha ya Kichina watoa fursa za ajira kwa vijana wa Sudan Kusini

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
Tangu kuanzishwa kwa mradi wa kujifunza lugha na utamaduni wa China mwezi Julai, 2021, vijana wengi wa Sudan Kusini waliojiandikisha katika madarasa ya lugha wamegundua umuhimu wa lugha ya Kichina.

Mayiik Deng, mwenye umri wa miaka 25, ni mmoja wa wanafunzi wa mwanzo wanaoshiriki muhula wa tano wa mradi huo katika Kituo cha Kujifunza Lugha ya Kichina katika Shule ya Sekondari ya Kutwa ya Juba. Ameliambia Shirika la Habari la China Xinhua kuwa, anaweza kuzungumza vizuri luha ya Kichina kutokana na kuhudhuria madarasa yote. Anasema kujifunza Kichina kutasaidia kuboresha uhusiano wa watu na uhusiano wa pande mbili kati ya Sudan Kusini na China.

Mayiik anasema Wachina wana ujuzi mkubwa, na anaamini kuwa, kupitia mabadilishano ya kitamaduni na lugha, wataweza kujifunza mengi kutoka kwao. Ameongeza kuwa, kuna fursa nyingi sana za ajira kutoka kampuni za China katika karibu kila sehemu ya Sudan Kusini kwa ajili ya vijana wanaoweza kuzungumza Kichina.

Kituo cha Mafunzo ya Lugha ya Kichina kimepokea mamia ya wanafunzi na wageni tangu kilipoanzishwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya nchini Sudan Kusini.

Mradi wa lugha ya Kichina na mabadilishano ya utamaduni chini ya awamu ya pili ya Mradi wa Ushirikiano wa Kiufundi unaofadhiliwa na China katika Elimu, unawezeshwa na wataalamu wa lugha ya Kichina na utamaduni kutoka Jumba la Uchapishaji la Elimu la Shanghai.

Mradi huo, ambao unatolewa bure, uko wazi kwa Wasudan Kusini kutoka Nyanja mbalimbali za maisha, na umevutia wanafunzi wa shule na wafanyakazi pia.

Puoch Simon Tut, mwenye umri wa miaka 40 na mfanyakazi wa Wizara ya Ulinzi na Masuala ya Maveterani, anasema kwa mwaka mmoja aliojifunza Kichina, anaona fahari kuwa na uwezo wa kuwasiliana kwa kina na kwa kujiamini kwa lugha ya Kichina. Anasema anaisubiri kwa hamu tarehe 23 mwezi Machi mwakani ambapo ataweza kupata cheti chake cha kufuzu masomo ya lugha ya Kichina. Ameongeza kuwa, atawashawishi wafanya kazi wenzake wajiunge na darasa la lugha kwa kuwa dunia inabadilika kwa kasi sana, na Wasudan Kusini hawapaswi kubaki nyuma.

Ustaz George Kenyi, mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kutwa ya Juba anasema, wakati mradi huo ulipofunguliwa kwa umma, watu wengi walijitokeza, hivyo kuwalazimu kuweka ukomo wa kupokea wanafunzi 30 baada ya miezi mitatu.

Mwalimu wa lugha na utamaduni wa Kichina Zhao Yongqiang ambaye pia ni msimamizi mkazi wa kituo hicho, anasema mabadilishano ya lugha na utamaduni sio ya upande mmoja, bali ni maingiliano ya pande mbili. Akizungumzia jinsi alivyoiona nchi ya Sudan Kusini baada ya kuwa huko kwa miezi 18, Zhao anasema Sudan Kusini ni nchi rafiki, watu wa nchi hiyo wanafanya kazi kwa bidii nan i jasiri sana.

Mpaka kufikia mwisho wa mwezi Novemba mwaka huu, kituo hicho kimetoa vyeti karibu 100 kwa wanafunzi walioonyesha utashi na uwezo wa kuzungumza lugha ya Kichina.
 
Back
Top Bottom