Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,318
- 33,125
NI VIZURI KUJUA VITU FLANI, USUSANI KATIKA UJASIRIAMALI
Ulishaji: Kuku wa kienyeji wanaweza kulishwa
kwa kumia mahindi, mchele, na mabaki ya
ugali. Vyakula hivi ni lazima vikaushwe vizuri na
kusagwa vizuri. Ulishaji ni lazima ufanyike katika
sehemu safi au kwa kutumia vyombo
vilivyotengenezwa maalumu kwa ajilii ya kulishia
kuku.
Banda: Kuku wawe wa kienyeji au wa kisasa,
wanahitaji kuwa na banda zuri kwa ajili ya
malazi na kuwalinda. Wanahitaji chumba chenye
nafasi ya kutosha na kinachopitisha hewa ya
kutosha. Ni lazima kuwawekea fito kwa kuwa
ndege hupenda kupumzika juu ya fito. Ni lazima
banda la kuku lifungwe vizuri nyakati za usiku ili
kuzuia wanyama wanaoweza kuwadhuru kuku.
Ni lazima liwe safi wakati wote ili kuzuia
magonjwa kama vile mdondo na mengineyo.
Usitumie pumba za mbao au nguo kuukuu
kwenye viota vya kutagia kwani huchochea
kuwepo utitiri na funza wa kuku. Inashauriwa
kutumia mchanga laini.
Maji ya kunywa: Kuku wapatiwe maji safi. Ni
lazima kuangalia mara kwa mara na
kuyabadilisha maji. Kamwe usiwape kuku maji
machafu.
Chanjo: Chanjo kwa mifugo ni lazima ili kuzuia
mashambulizi ya magonjwa. Magonjwa
yaliyozoeleka ni kama vile Mdondo, Kideri, Ndui
ya kuku, na homa ya matumbo (typhoid).
Chanjo kwa kawaida hutolewa mara moja kwa
kila baada ya miezi miwili.
Uwekaji wa kumbukumbu: Kumbukumbu
zijumuishe aina ya ulishaji, namba ya uzalishaji,
muda wa mwisho wa matumizi, kiasi cha
malisho kwa kila siku, idadi ya vifo, na idadi ya
mayai yaliyozalishwa.
Mwanzoni unahitaji nini?
Wafugaji walio wengi wanauliza wanahitaji nini
katika hatua za awali ili kuweza kuanzisha mradi
wa ufugaji wa kuku. Hii itategemea aina ya kuku
uliochagua kufuga.
Ni busara kuwa na vifaa muhimu vinavyohitajika
na viwe katika hali ya usafi kabla ya kuweka
kuku bandani mwako. Kama unaanza na
vifaranga, vifuatavyo ni vifaa muhimu
vinavyohitajika kwa ajili ya vifaranga 200.
Tenga na utengeneze banda zuri lenye joto na
hewa ya kutosha wakati wote.
Vyombo vinne (4) vya kunyweshea maji, hii ni
katika wiki 2 za mwanzo na uongeze vyombo
taratibu kulingana na kuku wanavyokua.
Vyombo vinne (4) vya kulishia chakula, na
viongezeke kulingana na kuku wanavyokua.
Matandazo makavu na safi, inaweza kuwa
maranda au mabua ya ngano.
Pakiti moja au mbili za dawa ya Coccid (hii
inapatikana katika maduka yote ya kilimo). Hata
hivyo, utaratibu wa chanjo ni lazima
ukamilishwe.
Chakula kwa ajili ya vifaranga ambacho
kimezalishwa na watengenezaji wanaoaminika.
chanzo:MziziMkavu
Kazi kwenu Wafugaji wa kuku wa Kienyeji.