Ujumbe wa Valentine ‘Day wasababisha talaka

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,320
33,125
HAMISA HAMIDU[28] mkazi wa jijini Dar es Salaaam, amejikuta akitwanga talaka moja na mumewe kwa kile kilichosemekana ni kukosa uaminifu kwa mume wake aliyedumu nae kwa kipindi cha miaka minne toka kufungwa kwa ndoa yao
Imedaiwa kuwa, sababu ya Hamisa kutwangwa talaka ilisababishwa na simu ya mkononi ambapo alitumiwa ujumbe mfupi wa maneno unaohusiana na sikukuu hiyo ya wapendanao

Imedaiwa kuwa, ujumbe huo ulihusisha ni kutumiwa ujumbe huo na namba ambayo mume wake alikuwa haifahamu na moja kwa moja mume huyo alidaiwa kuwa mbogo kwa mke wake huyo

Imedaiwa kuwa, siku moja kabla ya sikukuu hiyo ilidaiwa mwanamke huyo alimuaga mume wake huyo kuwa atakwenda kumuona mama yake mdogo mkoani Pwani ambaye alikuwa mgonjwa ambapo tayari mume huyo alishamruhusu akamuone mgonjwa huyo

Siku ya tukio Februari 14,mwaka huu majira ya saa 1 asubuhi, kabla mume huyo hajatoka kuelekea kazini kwake ambapo imedaiwa ni mfanyakazi wa serikalini, simu ya mkononi ya mke wake huyo ilikuwa ikiita ambapo muhusika alikuwa bafuni akijitayarisha na safari yake ya kueleka mkoani Pwani

Imedaiwa mume huyo hakupokea simu hiyo na aliiacha iite na aliporudi alimtaka mke wake aangalie simu hiyo ili ajue nani alikuwa akimpigia simu hiyo na aliweza kumjibu mumewe hakumtambua mtu huyo kwa kuwa ni namba ngeni kwake

Baada ya dakika kadhaa namba ileile ilitumika kumtumia ujumbe mfupi wa maneno uliosema” Hallo dear mbona hupokei simu, Happy Valentine Day…..I love Uuu,msalimie huyo, usisahau muda” ulimaliza ujumbe huo”

Ndipo hapo varangati kwa wanandoa hao likaanza na mume wa huyo alianza kutokwa n jasho la jazba na kupandwa na hasira kali na kumtaka afafanue vizuri hiyo namba ilikuwa ya nani, na mwanamke huyo akaanza kutetemeka na bila kujua aanzie wapi kujibu swali hilo”

Kwa kuwa hakuwa na jibu la haraka alichangamshwa na ngumi moja na ndipo alipoanza kumjibu mume wake kuwa huenda alikuwa ni mdogo wake binamu aliyeahidiana nae kwenda nae Kwa mgonjwa huenda hakutumia namba yake

“Labda atakuwa Asha ametumia namba si yake ngoja tumpigie mume wangu labda atakuwa yeye, alijibu Hamisa huku akibujikwa na machozi

Hata hivyo mume huyo alijikuta akibadilisha shati lake alilolivaa kwenda nalo kazini na walijaribu kumpigia huyo Asha lakini namba yake ambayo alikuwa akiitumia ilikuwa ikiiita na ndipo mume huyo alimuomba samahani shemeji yake huyo kwa kuua soo asijue ishu hiyo

Mume huyo alianzisha kibano kwa mke wake huyo na kasha kuobndoka na asimyu ya mke wake kazini na alipotoka kazini alipeleka ushahidi huo wa ujumbe kwa wazee ili wauone wasije wakamlaumu na maamuzi atakayoyachukua

Siku hiyo usiku wakaitwa na wazee kila mmmoja kaitakiwa kutoa maelelezo yake lakini Hamisa alionekana kuwa na huzuni na kudai hakumfahamu mtu huyo, japo mtu huyo kila alipojkuwa akitafutwa kwenye namba hiyo ilikuwa haipatikani

Kitu ambacho hakikuaminiwa na watu wengi mume huyo alipotoa maamuzi ya kumpa talaka mke ake kwa kuwa alionyesha sio mwaminifu na siku hiyo huenda alikuwa anakwenda kukutana na mwanaume wa nje kitendo ambacho mume huyo kilidaiwa kumtia uchungu

“ Kwa kweli mimi nikigundua mke wangu anatoka nje ya ndoa wkangu ni sumu sana siwezi kuvumilia, ninavyojitahidi kukutunza halafu unataka kutoka nje ya ndoa siwezi naomba mnisamehe wazee wangu mimi nampa talaka moja mke wangu naona ndio nitapata nafuuu kwenye roho yangu ameniudhi sana” alilama

Jana Hamisam mjaira ya usiku wa saa mbili alikabidhwia talaka yake moja huku akiiipokea kwa mahcungu sana na ali9jaribu kumuomba msamaha lakini haukukubalika

chanzo.
Ujumbe wa Valentine
 
Mmmmmh!tatizo watanzania wengi wanachukulia hii valentine vibaya,
Siku ya wapendano haimaanishi ndio siku ya kufanya ngono jaman lol!
Pole zake ngoja akatafakari vizuri akiwa kwao.
 
kha mtu unapewa kila kitu lakini bado hautulii, pole yake. ila talaka moja si anaweza tena kurudi kwa mumewe baada ya muda?
 
Jamaa alikuwa na haraka sana. Angetulia kwanza, aone issue nzima!
 
huyo mume anabahati sana-inaonyesha alikuwa akiliwa mali yake tangu muda tu
 
Back
Top Bottom