Ujumbe toka Kanda ya Ziwa kwa wanaume wa Dar es salaam

nawaheshimu watu wa mtwara. siyo hawa midebwedo. mwanaume mzima unachonga nyusi, unapaka wanja,lip shine, unabana sauti,unavaa tight, hayo yote unamrembeshea mwanaume mwenzako au? acheni u.....

Jamani wamesikia ili tuone uanaume wao wajiandikishe kupiga kura na wafanye mabadiliko vinginevyo hiii thread itaendelea mpaka uchaguzi mkuu upite
 
Usicheke mkuu....mtusaidie kuwafundisha ustaarabu hawa mashujaa wanaowamaliza vikongwe na maalbino badala ya kupambana na wawekezaji wanao waachia mashimo na ufukara....wanawamaliza bibi zao walowalea tangu utotoni mpaka ukubwani maana mama zao wengi wamekimbilia kimboka na uwanja wa fisi( wahaya) kuganga njaa...
.....nilishangaa kusikia shujaa limecharanga mkewe mapanga eti kazidisha chumvi kwenye mboga....hivi kweli utasema huyu nae ni shujaa...??

Mkuu naona mmeamka kujibu mapigo... Una mtizamo gani kuhusu wapaka lipstick, lipshine, wafanya pedi na manicure n.k?
 
Kama kweli nyie mpo strong....kwanini msitumie hiyo miili yenu mikubwa kama vibanda vya mikaa kufanya kazi kwa bidii na kujiletea mafanikio badala yake mmegeukia shotikati kwa kuwaua ndugu zetu albino na kuwamaliza wazee wenu....huku mkitarajia mafanikio kwa kunywa damu za watu hasa wasio na hatia...ndio maana wengi wenu kama mmechanganyikiwa kwa kuwa mwanaume mwenye akili timamu na anayejiita shujaa hawezi akamuua mkewe eti kisa kazidisha chumvi kwenye mboga....au kachelewa kurudi kisimani wakati unafahamu watu wanategemea kisima kimoja....badala yake ungetakiwa uonyeshe ushujaa wako na maguvu yako kwa kumchimbia mkeo kisima nyumbani au kuweka bomba la majisafi..ili mkeo asichelewe kurudi tena......Mwili mkubwa akili ya sisimizi....

Tunawamisi sana hao panya labda ndo maana nguvu zinaishia huko, lakin nyie visima mnaweza chimba ule urojo uchimbe kisima? Et ubungo to mabibo hostel kanaume kanapanda gari ndo maana hata kova alisema kuwa ni ka issue kadogo ila kamekuzwa tu mkammaind ila n ukweli n ka issue kadogo vitoto tu nawe ukawah uvunguni
 
Ila mi ni mhamiaji lakini ujumbe wako pamoja na kwamba umekaa kimzaha lakini ndio ukweli.
Ile siku mi nilitoka na panga linalokata kote kote nikaona vijana wanashangaa eti 'umepata wapi upanga!' nikasema pumbafuu.
 
Mkuu huu ukweli hatukakiwi ila umejaa ukweli! Dar waoga muno ,sehemu kubwa ya
maisha yangu imekuwa dar ila meengi ulitosema nimeyaona kwa nyakati tofauti tofauti! Mwaka 2007 serikali ilitishia eti kuna popo bawa, eti watu wakatetemeka, yani uwoga wa uchawi uchawi, niliwaambiaga mtaani acheni uoga uyo popo hayupo....ikaja dengue...wanaume wanataka kulia! Serikali dar inawafanya mazezeta!! Sasa eti kuna panya barabarani!! Hao panya wanatokea ikulu au kuzimu? Mbona mtaani hatuwaoni?????? Serikali mnawafanya mazezeta wanadarisalaam!!
 
Dar ndio Tanzania.....kwann tujisumbue kupigana na wahuni wkt jeshi la polisi lipo...hatutaki kuharibu mikono na sura zetu..dar kila m2 celebrity
 
Ndugu zangu wa Dar nimechoka kuwatetea....naona mpo kimya sana.....narudi...au yanayosemwa ni kweli mbona nakanusha pekee yangu.......watoto wa kiume wenzangu mbona mko wapi.......au wakina mura wapo sahihi......???
 
Lakini hii mada ina ukweli ndani yake.....wazawa wa DAR wana asili ya ulege lege......hata huku JF kutwa nzima wanashinda SELEBRITI FORAMU....
 
Wanaume wa dar kweli mmedhihirisha ni waoga wa kutupa.

Juzi nyinyi wenyewe ndo mlikuwa vinara wa kutangaza hofu
kuwa kuna panya-road, afu ndo wenyewe mlikuwa mstari wa mbele kufunga maduka na kukimbia hovyo hovyo hata hao panya hamjawaona.


Ni aibu sana hii kwa mwanaume. Yaani badala ya kuhamasisha wanaume wenzio mjitokeze kupambana na panyaroad, nyie ndio mnahamasisha
watu wafunge biashara wakimbie! dah aibu kweli hii.


Ulegevu huu huwezi kuukuta huku Kanda ya Ziwa maana kwenye dharula kama hiyo huwa kuna vitu vifuatavyo wanaume mlipashwa kufanya.

Kupiga yowe na kukusanyika kwenda kuwafyekelea mbali hao panya road. Sasa basi ili muwe majasiri inabidi muache mambo ya kitoto kama:

1) Kunywa kahawa na kashata na joto lote lile.

2) Achaneni na kula pweza kuleni ugali wa mhogo na sangara.

3)Vitu kama ngisi, kachori na juice ya miwa vinawafanya muwe nare nare sana.

4) Ni aibu kwa mwanaume kuweka chumvi pilipili na ndimu kwenye mahindi ya kuchoma au
kuweka chumvi kwenye embe.

5)Acheni mara moja kula ubuyu mnajidharirisha mno.

6)Komeni kuangalia tamthiliya kwenye tv.

7).muache kuvaa heleni na kupaka ina na kuongea sauti za kike.

Haya ndio baadhi ya mambo yanawafanya muwe mdebwedo wa kutupa. Mkiendelea hivi ipo panyaroad panya road watakuja kuomba wawekewe maji ya kuoga na wake zenu mchana kweupe na nyie mpo.

Jiangalieni sana...
UMESAHAU .. Waache kushabikia CHAMA kizee
 
Ndugu zangu wa Dar nimechoka kuwatetea....naona mpo kimya sana.....narudi...au yanayosemwa ni kweli mbona nakanusha pekee yangu.......watoto wa kiume wenzangu mbona mko wapi.......au wakina mura wapo sahihi......???

Mkuu hakuna cha kutetea,hao kanda ya ziwa wametushika leo!Tujirekebishe siyo mpaka kuua mende unamwita house boy au mlinzi?!
 
Back
Top Bottom