Ujumbe muhimu Sana. Soma kwa makini ili uwe philosher kama wao

deblabant

JF-Expert Member
Oct 7, 2022
901
1,334
Justice okoro, Mchungaji wa dhehebu la pentekoste, Zambia alisema;

Mimi nawapenda Wakatoliki kwa kiwango cha kutokujali maneno ya watu wanasema nini juu yao, Unaweza kukosoa kanisa lao, viongozi wao au imani yao, kadiri unavyoweza watakusikiliza hadi umalize, kisha wataenda kanisani Jumapili ijayo, kushiriki Sakramenti na kurudi nyumbani.

Wanaamini kuna miujiza lakini hawatafuti miujiza feki na bandia kutoka kanisa moja hadi kanisa lingine, au upako na baraka za uongo na wala hawahitaji kujitetea kwa mafundisho yao msingi.

Misa ni saa 1 tu, hakuna wakati wa kejeli, ushuhuda na sio lazima uvae nguo kupita kiasi ili kumvutia mtu yeyote kwasababu wanaamini Mungu anaangalia moyo uliopondeka sio mavazi.

Hawana hata vipaza sauti makanisani mwao vya kuwasumbua watu, hawafanyi mikutano ya kidini njiani wala kwenda kuinjilisha kwenye viwanja, Ukitaka kujiunga nao, inabidi uende kutafuta kanisa wewe mwenyewe, hawana muda wa kukushawishi ujiunge nao au kukubembekeza ubaki kanisani kwao.

Wala hawana muda wa kuhubiri dhidi ya madhehebu mengine. Hawana hata wakati wa kutambua wageni kwa salamu zisizo za lazima kanisani.

Kuzingatia mambo yao ndiyo kazi yao wakati wote. Hakuna wakati wa kuandaa ndoa za uwongo, miujiza feki hakuna unafiki wa kujificha wanapokunywa au kula au kuhubiri injili kwa kujeli imani za wengine.

Hakuna haja ya kibali cha padri kujua unaishije, kwasababu uhusiano ulio kati yako na Muumba wako moyoni mwako unatosha bila kupiga kelele ili kuthibitisha chochote kitu.

Kama wanadamu ambao pia ni dhaifu Wanatenda dhambi kila siku na kufanya toba ya kila siku, sala, ibada na kutafakari kila siku. Kanisa lenye nidhamu sana toka enzi za mitume, likaenea ulimwenguni kote, mama wa dini ya Ukristo na ndilo lililoandaa hata Biblia tunayoitumia sisi kwasababu kabla ya mwaka 399 hatukuwa na Biblia duniani 🙏🙏
 
kanisa ambalo kubatiza mtoto kwanza masharti yake uyazingatie afu utoe michango yote wanayotaka na zaka ya mwaka mzima kama hutaki basi na kubatiza hubatizi pita kule hawakibembelezi! ni nzuri but haijakaa sawa!
 
kanisa ambalo kubatiza mtoto kwanza masharti yake uyazingatie afu utoe michango yote wanayotaka na zaka ya mwaka mzima kama hutaki basi na kubatiza hubatizi pita kule hawakibembelezi! ni nzuri but haijakaa sawa!
Ni nzuri ila haija kaa sawa sio😂
 
Ni madhehebu ya kwanza pia yaliyo ruhusu kuwabariki mashoga.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom