Ujumbe Kwa Tanapa - Utalii

Pinto ameshaanza ingia mitini, nasikia ata DISCO kule Leicester ameshafunga
 
Haya mambo bwana..watu wanafanya wakifikiri wako mbali na hawataweza kamwe kuonekana!! Shame
 
Jamani mbona huyu jamaa anapata lawama ambazo sio zake.Kwani yeye hakwenda tanzania na kulazimisha kupewa Tender, ameomba tender na amepewa.Swala la kujiuliza nani alimpa Tender na kwa kigezo gani? kwani yeye sio serikali.Serikali ya Tanzania inawajibika moja kwa moja kwa hili.

When the blind rules the blinder that is what happen
 
Jamani mbona huyu jamaa anapata lawama ambazo sio zake.Kwani yeye hakwenda tanzania na kulazimisha kupewa Tender, ameomba tender na amepewa.Swala la kujiuliza nani alimpa Tender na kwa kigezo gani? kwani yeye sio serikali.Serikali ya Tanzania inawajibika moja kwa moja kwa hili.

Tatizo sio kuomba tenda,ila kama juma pinto aliomba,hiyo tenda ilitangazwa wapi,maana kama aliomba bila kutangazwa that means kuna lobying and there was no fair competition.na kama aliomba alishindanishwa na nani
 
Wakulu wa JF;

Nimesikia kutoka katika sources mbili tofauti na katika vipindi viwili tofauti kwamba MNENE wa TANAPA alikutwa na PCCB (Arusha) akiwa na kiasi kukubwa cha pesa zinazofikia TZS 6 Billions. Ila mpaka sasa hii issue "Bado ipo ipo tu . . . . "

Wenye DATAZ tunaomba mtuhabarishe zaidi.
 
Si kweli na mbona hutaji jina lake ? Huyo anayatarajiwa kuondolewa hapo kati kati ya mwezi huu au nani
 
Mkuu Alien alikutwa na lundo la noti zinazo fikia billion 6 au? Maana ni vigumu mtu kuwa na kiasi hicho cha pesa nyumbani kwake. Au ina kuaje kuaje mkuu?
 
Mkuu Alien alikutwa na lundo la noti zinazo fikia billion 6 au? Maana ni vigumu mtu kuwa na kiasi hicho cha pesa nyumbani kwake. Au ina kuaje kuaje mkuu?


Mkuu;

Hizo ndo info nataka nijue kama una ukweli wowote.

Kama 3 months ago nilisikia toka source A lakini nikapuuzia. Few weeks tena nikasikia toka Source B. Nasikia kuna safe kwa huyu Mkulu.

Ila sijui kama zilizopatikana ni $$$ au TZS. Nilipojaribu kuwadadisi zaidi kila moja wapo anadai naye alisikia Tetesi vile vile . . .

Nchi hii ya tetesi sana. Mzee V.G. Cent naye alianza hivi hivi. Haki ya Mbongo!
 
Lisemalo lipo..hata Usalama wa Taifa sijui kweli kama tena wanatulinda hujuma za uchumi kama huu!


Kama ni kweli na PCCB hawakumshughulikia then ina maana ni YALE YALE.

Katika nchi yetu, kila kitu kinawezekana. RA ameshaprove hivyo.
 
Mkulu wa Tanapa si Bigurube, yule mzee ni mlokole bwana

http://www.uhuruinfo.co.tz/page.php?soma=page0,0,1,mz&id=7878

TANAPA kwafukuta

* Wafanyakazi wasambaza waraka wenye malalamiko
* Uongozi wadai hayo ni majungu yasiyo na ukweli

NA MWANDISHI WETU

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limekumbwa na mgogoro wa kiutendaji na hasa kuhusiana na maslahi, imeelezwa.

Wakati madai hayo yakitolewa, uongozi wa TANAPA unasema hayo ni majungu na ambayo hayana ukjweli wowote.

Habari kutoka ndani ya TANAPA zilidai kuwa mgogoro mkubwa wa kiutendaji umeibuka ndani ya shirika hilo na kuhusisha ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na upendeleo mambo yaliyosababisha kuwepo kwa mgawanyiko.

MZALENDO imeelezwa kuwa mmoja wa viongozi wa TANAPA (jina linahifadhiwa) amekuwa akitumia mtindo wa kugawa wafanyakazi na kuwatawala na kuwapa baadhi yao upendeleo jambo ambalo linalalamikiwa na wengi wao.

Ilielezwa kuwa baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo wamekuwa wakipewa upendeleo na hata kupandishwa vyeo kutokana na kuwa karibu na uongozi, licha ya kuwa hawana sifa za kushika nyadhifa walizopewa.

Baadhi ya wanaotajwa kupata upendeleo huo ni ofisa (jina tunalo) aliyepewa cheo cha umeneja na kuwa wengine ni wale wanaopewa vyeo kwa kuundwa nafasi ambazo hazikuwepo.

Wafanyakazi wa TANAPA pia wanalalamika kuwepo kwa ‘kijana’ anayelindwa na uongozi na ambaye amewekwa kwa ajili ya kuwahudumia wajumbe wa Bodi na kuwa ndiye amefanywa kuwa ofisa manunuzi ya shirika.

Walidai kuwa ofisa huyo ndiye anafanya manunuzi ya magari ya shirika na vipuri na pia kusimamia matengenezo na uwekaji wa mafuta. Ofisa huyo mara kadhaa amekuwa mfanyakazi bora.

Wengine wanaodaiwa kupewa upendeleo ni wakuu wa baadhi ya hifadhi ambao inadaiwa hawana sifa, lakini ndiyo kila mara wanasafiri kwenda nje.

Madai mengine ambayo MZALENDO imeyapata ni kuhusu kuwepo kwa upendeleo kwenye sera ya mafunzo ambapo wanaosomeshwa ni wale waliopata daraja la kwanza na pili tu, hata hivyo wengine licha ya kutokuwa na sifa hizo wamekuwa wakipelekwa shuleni.

Wafanyakazi hao pia wanalalamika kutopewa nyongeza ya mishahara ambayo bajeti yake ilitengwa tangu mwaka 2008 na sasa ni zaidiya mwaka hawajalipwa fedha hizo.

Wakati hali hiyo ikijitokeza, habari zilisema mmoja wa maofisa hao amekuwa akitumia magari ya kukodi kwa ajili ya kujenga barabara na kuwa magari hayo ni yake binafsi

MZALENDO ilielezwa kuwa magari hayo yamekuwa yakilipwa kiasi cha sh. 250,000 kwa siku huku dereva na msaidizi wake wakipewa sh. 20,000 kwa siku. Wafanyakazi hao pia wanalalamika kupigwa marufuku kwa vikao vya chama cha wafanyakazi vya CHODAWU.

Alipoulizwa kuhusiana na suala hilo, Meneja Uhusiano wa TANAPA, Pascal Shelutete, alisema madai hayo yote hayana ukweli na kuwa ni majungu.

“Zote ni tuhuma ambazo hazina ukweli wowote na ndiyo maana hakuna hatua zilizochukuliwa na mamlaka nyingi za usimamizi,” alisema Shelutete.

Aliongeza kuwa kuna baadhi ya wafanyakazi wamekuwa wakipita na kutoa taarifa za uongo kwa lengo la kuwayumbisha viongozi na kuwa mambo ndani ya TANAPA yapo shwari.

 
Source: Home

Maliasili `kwawaka moto`



Mambo sasa si shwari ndani ya ya Wizara ya Maliasili na Utalii na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa), baada ya kuwepo taarifa kuwa yatafanyika mabadiliko makubwa ya uongozi ndani ya vyombo hivyo viwili, kufutatia sakata la tuhuma za ufisadi lililoikumba wizara hiyo.

Sambamba na hilo, habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili, zinaeleza kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), tayari imeshaingia kazini kuwachunguza kwa kina maafisa wote wa wizara na Tanapa, ambao wanatuhumiwa kujihusisha na vitendo vya ufisadi na uhujumu wa maliasili za taifa.

Kama hiyo haitoshi, Waziri wa Maliasili na Utalii, amewaita ofisini kwake na kuweka ‘kiti moto’ maofisa wote wa wizara yake wanaohusishwa na tuhuma mbalimbali za ufisadi ili kujua ukweli wao.

Hatua hiyo imekuja siku chache tu, baada ya gazeti hili kwa wiki kadhaa kuandika kwa kina habari za ufisadi unaofanyika ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii na jinsi maliasili za taifa zinavyoibwa na kutoroshwa nje ya nchi kwa kasi kubwa, kwa msaada wa baadhi ya maofisa wa wizara na Tanapa.

Habari za kiuchunguzi kutoka ndani ya wizara hiyo na Tanapa, zinaeleza kuwa vitendo vya ufisadi na uhujumu wa maliasili za taifa vimekithiri kiasi cha kumshtua Waziri mwenye dhamana ya Maliasi na Utalii, Shamsa Mwangunga, ambaye ameapa kuvivalia njuga kuhakikisha anakomesha vitendo hivyo, vinavyoligharimu taifa hasara kubwa.

Mwangunga, wiki mbili zilizopita alifanya ziara ya siku sita kwenye mbuga mbalimbali za wanyama nchini na kushtushwa na ujangili wa kutisha uliopo kwenye Hifadhi za Taifa pamoja na malalamiko ya wafanyakazi.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu wiki mbili zilizopita mara baada ya kumaliza ziara yake hiyo, Waziri huyo wa Maliasili na Utalii, alisema amegundua mambo ya kutisha, ikiwemo kukithiri kwa vitendo vya ujangili na wanyama hai kusafirishwa nje ya nchi kinyume cha taratibu.

“Katika ziara hii nimegundua mambo ya kutisha, ikiwa ni pamoja na wanyama kuuawa ovyo na ngozi pamoja na nyama kusafirishwa nje ya nchi hata wengine kusafirishwa hai”, alisema waziri huyo.

Aliwataja wanyama wanaouawa zaidi na majangili ni aina ya Tembo, Pundamilia na Twiga, kwa ajili ya ngozi na nyama ya kula, ambavyo husafirishwa nje ya nchi kwa lengo la kuuzwa.

Wakati hayo yakiendelea, wakurugenzi wawili wanaoongoza vitengo nyeti ninavyohusika na wanyamapori, (majina yanahifadhiwa), wanatajwa kuwa wahusika wakuu wanaoongoza vitendo vya ujangili kwenye mbuga za taifa na utoroshaji wa nyara za serikali nje ya nchi.

Wakurugenzi hao wanadaiwa kuwasaidia wafanyabiashara wanaomiliki makundi ya majangili kuwinda wanyama pori kwa njia zisizo halali, kwa kupatiwa mgao wa fedha kutokana na faida inayopatikana kutokana na mauzo hayo.

Habari za uhakika kutoka vyanzo mbalimbali vya habari vilivyomo ndani ya sekta ya maliasili, zinaeleza kuwa kwa kushiriki uhalifu huo viongozi hao wamejikusanyia utajiri wa kutisha ikiwemo kumiliki majumba ya kifahari ndani na nje ya nchi.

Inadaiwa kuwa baadhi ya maofisa hao wana uhusiano wa karibu na vikundi vya majangili wanaouwa wanyama katika kiwango cha kutisha na makampuni ya uwindaji wanyapori ya ndani na nje yanayojihususha na uwindaji haramu.

Baadhi ya askari wanyamapori wanaofanyakazi katika hifadhi za taifa, wiki hii walilieleza gazeti hili, kuwa vitendo vya ujangili katika hifadhi hizo vimefikia kiwango cha kutisha na kutahadharisha kuwa endapo hatua za haraka hazitachukuliwa kudhibiti hali hiyo, huenda baadhi ya wanyama kama Pundamilia, Twiga wakaanza kupungua kwa kasi kama ilivyo kwa tembo na vifaru wanauawa kwa wingi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusiana na vitendo vya ujangili katika hifadhi za taifa, Mwangunga, alisema vitendo hivyo katika siku za hivi karibuni vimeongezeka kwa kasi.

Hata hiyo, alisema askari wanaolinda wanyamapori kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, wanafanyakazi nzuri ya kukabiliana na vitendo hivyo, na kwamba watu kadhaa wanaojihusisha na vitendo hivyo wamekwisha kamatwa kwenye maeneo mbalimbali nchini, baadhi yao kesi zikiwa mahakamani.

Jana Mwangunga, alisema amekuwa akipata taarifa za siri za mara kwa mara toka kwa watu mbalimbali zikiwataja baadhi ya maafisa wa wizara yake kuwa wanahusika na uhujumu wa maliasili za taifa.

“Nimekuwa nikipata taarifa za siri zikiwataja baadhi ya maafisa wa wizara yangu kuwa wanahusika kwenye vitendo hivi, kwa kuanzia nimewaita maafisa wote wanaotajwa na kuwauliza mmojammoja wana maslahi gani kwenye malaisili za taifa, wote wamekana, lakini hatuja ishia hapo bado tunawachunguza kupitia njia nyingine” alisema.

Wakati uchunguzi dhidi ya maofisa wa wizara na Tanapa ukiwa umeanza, habari zinaeleza kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa, Gerald Bigurube, ameomba kustaafu miaka miwili kabla ya muda wake kumalizika, kwa kile alichoeleza kuwa anataka kushughulikia mambo yake binafsi.

Kwa mujibu wa habari kutoka ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Bigurube, tayari ameomba kustaafu Juni 30 mwezi ujao na Rais Jakaya Kikwete amemwambia ruksa.

Alipoulizwa kuhusu taarifa hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga, ingawa hakukubali wala kukataa, lakini alijibu kwa mkato, "Mtu anayetaka kustaafu kwa hiari kabla ya muda wa utumishi siwezi kumkatalia".

Habari za uchunguzi kutoka ndani ya wizara hiyo zinasema kuwa huenda hatua hiyo ya Bigurube ikaathiri uchunguzi huo, kwani ni mtu muhimu anayetakiwa kuhojiwa kutokana na kuliongoza shirika hilo kwa muda mrefu.

“Hata kama akikubaliwa kustaafu tunaomba naye ahojiwe kwani anajua mambo mengi yaliyokuwa yakiendelea ndani ya Tanapa” alisema mfanyakazi mmoja wa Tanapa wakati akizungumza na gazeti hili bila ya kufafanua zaidi.

Sambamba na hilo, pia kumekuwa na malalamiko kuwa Bodi ya shirika hilo inayoongozwa na Modestus Lilugulu, ni dhaifu katika kutoa maamuzi na kushindwa kuchukuwa hatua hata pale maamuzi yake yanapopuuzwa, hali ambayo inamfanya waziri husika aanze kuingalia kwa jicho la wasiwasi na habari zisizothibitishwa zinasema huenda akaivunja wakati wowote.

Mmoja wa wafanyakazi hao amedai kuwa hali hiyo ndiyo chanzo cha wafanyakazi ndani ya shirika hilo kulalamika kwani shida zao zimekuwa hazitekelezwi pamoja na maslahi kupuuzwa, hakuna vitendea kazi, malazi duni na hawana uhakika na makato yao kwenye Mfuko wa Mashirika ya Umma (PPF) na mambo mengine.

Wajumbe bodi ya Tanapa ni pamoja na Bigurube (Mkurugenzi Mkuu Tanapa), Erasmus Tarimo (Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori), Lazaro Nyalando (Mbunge- Singida Kaskazini), Ramadhani Maneno (Mbunge- Chalinze), Riziki Lulida (Viti Maalum mkoa wa Lindi), Dk.Marcelina Chijoliga (Mhadhiri Chuo Kikuu), Philip Muhandagani (mfanyabiashara) na Mariam Wilmo.

Wiki moja iliyopita, Waziri Mwanguka alifanya ziara ya siku sita katika hifadhi za taifa, lengo kuu likiwa ni kusikiliza kero mbalimbali za wafanyakazi.

Katika ziara hiyo ambayo pia aliambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa, Bigurube, Mkurugenzi wa Wanyamapori Tarimo na maofisa wengine, Waziri alipata malalamiko mbalimbali toka kwa wanyakazi wa hifadhi hizo ambazo ni pamoja na Tarangire, Ngorongoro, Serengeti, Manyara na hata Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.

Baadhi ya kero alizoambiwa waziri ni pamoja na maslahi duni hasa kwa askari wanaopambana na majangili maporini, vitendea kazi haba, kutokuwepio malazi ya kudumu na kukosekana huduma nzuri za matibabu.

Wizara ya Maliasili na Utalii pia inakabiliwa na tuhuma ya baadhi ya maafisa wake kutafuna shilingi bilioni 2.4 zilizotolewa kama msaada na serikali ya Norway kupitia Mpango wa Usimamizi wa Rasilimali (MNRP) katika kipindi cha miaka 12.

Tathmini iliyofanywa na mshauri huru imefichua kwamba katika kipindi cha mwaka 1994 hadi 2006 ambacho MNRP imekuwa ikifanyakazi katika sekta za uvuvi, wanyamapori na misitu zilizoko chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, fedha hizo zilizotolewa kama msaada kwa miradi mbalimbali katika sekta hizo zilitafunwa kwa njia za rushwa na ubadhirifu.
 
Back
Top Bottom