Mkuu unapinga sio nyoka na tornado ni nn? Au kwakua wazee wako waliita nyoka basi umeona ni myth lakini unakubali kinajiviringa kama nyoka .Hizi myth tulikuwa tunazisikia sana. Tukiwa vijana huko Morogoro hususani kipindi cha mvua za Elinino, kuna siku mvua ilipiga kubwa sana kuamka asubuhi tukakuta madaraja yameng'olewa na maji wazee wakawa wanatuambia kuna linyoka lilikuwepo katika safu za milima ya unguu kule Mvomero sasa linaenda baharini ndio limepita na kung'oa hayo madaraja kwani hupitaga na Maji.
Nadharia hii pia niliwahi isikilize kule Iringa kuwa kuna Joka(Wao hujiita litemela) watanisahihisha hukaa kwenye kichuguu karibu na chemchemi za maji na kuna kipindi hua linahama toka eneo moja kwenye eneo lingine so ukiamka asubuhi unakuta Kichuguu kimehama toka sehemu moja kwenye sehemu nyingine. Wazee wa kihehe walinieleza hilo kule Dabaga kwenye mashamba ya Chai.
Kimsingi, binafsi naamini katika ulimwengu wa Roho na haya manyoka ndio hayo wazungu wanadaiwa Levithian n.k possible waliishi duniani kabla ya uumbaji wetu.