Ujio wa Nchimbi Kinana amepata amani ya moyo

FbUser

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
431
626
Na Bollen Ngetti

KWANZA niwape pole wanaondelea kukumbwa na madhila ya mvua jijini Dar es salaam. Hali ni mbaya sana katika baadhi ya maeneo . Nyumba zinasombwa, watu wanakufa, mali zinateketea. Ni wakati mgumu lakini tushirikiane kujiokoa pale tunapoweza lakini pia kujifunza kwa yatokanayo.

NAAM! Hatimaye CCM kimempata Katibu Mkuu wa chama kufuatia kujiuzulu kwa Daniel Chongolo aliyeundiwa zengwe la kubumba (tunajua yote nyuma ya ukuta mweupe). Huyu ni kachero Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi mtunzi wa wimbo "tuna Imani na Lowassa...2015". Huyu ni jembe kweli kweli Kwa siasa za kimkakati. Sina shaka hata kidogo na kaka yangu Nchimbi. Ni chaguo sahihi kwa wakati sahihi.

Mguu wa kwanza wa Mwamba huyu ameanza kwa kutoa maelekezo kwa viongozi wenzake, "msiwafokee watendaji wa Serikali hadharani" (naweza kukosolewa).

Kwa kauli hii na msimamo huu KM haungi mkono utendaji wa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Paul Makonda wa kuwaita hadharani watendaji wa Serikali kwa njia ya simu akiigiza utawala wa Marehemu John Pombe Magufuli ambaye alijisikia raha kudhalilisha watendaji hadharani asiamini katika vikao.

Msimamo huu wa KM Chimbi ndio imani ya Makamu Mwenyekiti Bara Kamarada Mzee Kinana asiyeamini katika siasa za kibabe. Na kwa mantiki hii ni dhahiri Nchimbi na Kinana watakiendesha CCM katika misingi yake asilia.

Kinachotia shaka ni kuona huku KM akitoa msimamo huo kama mtendaji Mkuu wa chama kwa upande mwingine Makonda yeye anapuyanga kivyake akiendelea kuwapigia simu watendaji na kuwapa maelekezo akijificha nyuma ya "maelekezo ya chama si yangu" lakini akijua si kazi yake.

Moja ya kazi ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi ni kuongozana na Katibu Mkuu na ni yeye ndiye anatakiwa kumkaribisha KM jukwaani na si vinginevyo. Kazi ambayo Nape alifanya vizuri sana chini ya Kinana. Hii ya Makonda unajiuliza nani ni KM na nani ni Mwenezi.

Bila ya shaka yoyote tunaamini Nchimbi atabadili hali hii ya Makonda kuwadhalilisha watendaji wa Serikali akiwemo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyepewa siku 60 kumaliza migogoro yote ya ardhi nchini. Sasa zimebaki siku 29 sijui Majaliwa atafanywa nini maana migogoro ya ardhi ndio kwanza inarindima (binafsi nikiwa na mgogoro wa ardhi).

Hongera sana kachero Dkt. Nchimbi. Piga kazi lakini kwa kusahau siasa za kale 2015. Usikubali kuingia kwenye mitego ya Makonda na waumini wa siasa za enzi za giza utazama kama watangulizi wako. Mimi nimekaa paleeee....na kahawa yangu. Kazi Iendelee!

Nawatakia Dominika njema!

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom