Ubumuntu
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 14,316
- 10,782
Strabag ambae ndio anaejenga hiyo barabara sio aliedesign hiyo barabara, yeye anapewa michoro ambayo inaonyesha nini anatakiwa afanye kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Alidesign hiyo barabara ni SMEC International, hawa ni kutoka Australia, na ndio wanaoisimamia hiyo barabara. Swala la mitaro ya ubungo design ya mwanzo haikuwa sahihi, kwanza ilikua ni hatar kwa usalama wa watumia barabara watembea kwa miguu na hata waendesha vyombo vya moto,maana ilikua ni mikubwa sana na iko wazi. Pili hakuku na haja ya kujenga mtaro mkubwa vile kufuata barabara toka mbali wakati karibu tu kuna ule mto ambao unaweza punguza maji. Tatu, hakukua na haja ya mtaro mkubwa vile maana hakuna catchment area ya ukubwa ule, maji yanagawanywa vizur na mtaro mdogo tu wa sasa unatosha!
Chifu, hakika wewe ndiyo mhandisi.
Ile mitaro ya awali ni kweli ilikuwa ni hatari kwa usalama wa waendesha magari na watembea kwa miguu.
Halafu pia inapokuwa wazi ni rahisi kwa waswahili kuigeuza mitaro kama madampo ya takataka, hivyo inaponyesha mvua, taka hizo ndizo uziba mitaro hiyo.
Kwa upande mwingine, ujenzi wa sasa (wa kuifunika mitaro) ndiyo utaratibu wa kimataifa. Hivi Ulaya unaweza kukuta mitaro kama hiyo ya Morogoro road? Ha wapi!! Mitaro yote kama sehemu ya sewage systems za kubeba flash and storm waters, uwa imefunikwa.
Hivyo hawa STRABAG wako sawa kwa kile wanachofanya.