Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo updates

Bright Smart

JF-Expert Member
May 4, 2011
644
311
Wakuu naomba kujua kwa wale wenye ufahamu. Kuhusu ujenzi wa bandari ya Bagamoyo maendeleo yake yamefikia wapi.

Na pia naomba kujuzwa kuhusu maendeleo ya Bagamoyo Park project yamefikia wapi!!

Na pia vp nchi za Marekani na India zina mpango wowote wa kuzuia hizi project za Bagamoyo port na Bagamoyo park zisiendelee!!
Asanteni.
 
Kwa vile ujenzi haukuanza awamu iliyopita ikiwa madarakani, ndio basi tena.
 
Kwa sasa vipaumbele ni kuhamia Dodoma na ujenzi wa Chato and Dodoma airports. Sahau kuhusu mradi wowote ule unaoihusisha Bagamoyo.
 
Mambo yote Dodoma, hujasikia wachina wanataka kujenga barabara ya kulipia
kutoka Dar mpaka Dodoma? utasubiri sana Bandari ya Bagamoyo,
kama uliwekeza huko kwa sasa utaisoma namba vizuri.
 
Jamani Langu ni Moja tu! Kwa hapa Magomeni kota Hii ahadi ya mheshimiwa rais kujenga makazi, naomba iangaliwe vizuri kama ikiwezekana hawa watu wakaajengewe makazi maeneo kama Kigamboni au Buguruni na eneo husika likakodishwa kwa wawekezaji kwa ajili ya vitega uchumi (Shopping complex owned by Government - Land) na tutakuwa tumeongeza wigo wa Kodi na ajira!! Ikumbukwe hawa watu walikuwa wapangaji na si wamiliki wa eneo ila serekali ikawajengee eneo jingine. Always a controlled business area (Park) kama mlimani city is easy to collect Tax Hatujachelewa bado kwani nia ya Mheshimiwa rais ni njema sana!!
 
Hivi inakuaje kweli wapangaji wanajengewa nyumba na serikali,ila wale wa kule kahama waliopatwa maafa serikali imegoma kutekeleza ahadi yake?
 
Duh!! yaani majibu yote yaliyotolewa hakuna hata moja linalo jibu maswali yangu, hivi jamii forums bado ni ya Great Thinkers kama zamani!!?
 
Back
Top Bottom