Ujenzi udom ni epa nyingine?

kweleakwelea

JF-Expert Member
Nov 29, 2010
3,066
1,535
Kwa miaka mingi, Mfumo wa utawala wa siasa umeomanishwa na utawala wa serekali. kwa namna hii tofauti na nchi kama Ethiopia, wananchi wa Tanzania kwa kupitia serekali yao, mashirika ya umma na vyama vya ushirika wamejikuta wakilipa kodi kubwa kugharamia ufisadi na matanuzi ya wanasiasa. hii ikapelekea kushindwa kwa serekali kugharamia huduma za msingi, kuua mashirika na vyama vya washirika. era hii iliishia pale che Nkapa alipomgonga nyundo ya utosi Edward Hosea kwa kupanda ndege moja na mwenyekiti wa ushirika shinyanga wakienda kula bata sauzi. ilibidi hosea afunge faili hili la ufujaji fedha za ushirika shinyanga baada ya kuona maelezo haya ya picha almaarufu kibonzo hiki!.

ukaja ufisadi wa design mpya ambao ulimshirikisha kwa kiasi kikubwa RA akiwa mwenye dhamana ya kutunza shilingi ya chama. huyu ameruhusiwa kufanya madeal mengi tu wala sio hilo la dowans na richmond pekee. kimtizamo, huyu ndiye aliyemfurunda Magufuli na kuweka team yake ambayo inampa contract za barabara. sina uhakika lakini quality ya hizo barabara anazojenga. inaweza pia kuwa ufisadi mwingine. wapo wanaofadhili makontena ya tshirt na kuachiwa wauze mafuta kwa bei wanayotaka wao in the name of Haruna Masebu. TUNAONA jinsi masebu jinsi alivyo readily kupandisha bei ya umeme.

"Tumeamua kuruhusu ongezeko hilo na kama Tanesco wanadhani gharama zao za uendeshaji zinapanda kwa sababu ya ongezeko la gharama za mafuta ya kuzalishia umeme, wanaweza kujenga hoja na tukabadilisha bei ya mafuta pia," alisema Masebu. Masebu alisema pia wameiagiza Tanesco kuanza mabadiliko hayo ya bei ndani ya siku 30 na kuwapelekea mkataba ili kujiridhisha kama hautakuwa na madhara kwa watumiaji wa nishati hiyo - source mwananchi 25 dec 2010.

uharaka huu hautofautiani sana na ule wa ngeleja katika zoezi zima. Waasia wamependwa zaidi kwani dili zote alizoshirikishwa mswahili huwa zinabumburuka. mfano ni EPA za bank kuu na kina balali...kagoda enterprises na meremeta. hesabu za waasia ni kali zaidi.

nina wasiwasi kuwa sasa epa imehamia kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii yaani PSPF, LAPF na NSSF. sina uhakika sana ila nina mashaka makubwa. siku moja nikiwa natembelea kule juu nikapata nyepesi kuwa cafeteria moja hujengwa kwa gharama hadi ya 8 bn. kamzunguko kenyewe wala si ka kubwa kihivyo. nina wasiwasi kuwa inaweza kabisa kuwa ujenzi wa UDOM ni epa nyingine? kwa sehemu kubwa wajenzi wa chuo ni wachina. Wakati el akiwa waziri wa tamisemi alilianzisha pia kwa fujo ujenzi wa LGTI hombolo. All in all, hebu wanajf tulifwatilie hili tusijekuwa tunahangaika na dowans wenzetu wako karne mbili mbele! inawezekana zaidi ya nusu ya hizo hela za wastaafu zinarudi kwa mlango wa nyuma! OLE WAKO TANZANIA! UTAJENGWA NA WAVAA T - SHIRT UTALIWA NA WAPANDA MASHANGINGI!
 
umekosea kidogoo Mizengo Pinda ndiye alikuwa Wizara ya serikali za Mitaa! Ila all in all tukianza ukaguzi wa huo mradi utapatwa heart attack maana 30% ni nyingi mnoo...
 
yeah! el alikuwa ni primier..... he emphasised seriously and facilitated hard on the ongoing construction!
 
Back
Top Bottom