Ujasiriamali gani huu wa kuvunja ndoa za watu……………………!

ipo siku atashughulikiwa mwenyewe atatulia..kama si kuhama mtaa....
hata hao private investigators hawafanyi hivyo, mpaka mwenye mke/ mume amtume...
huyo anachofanya ni blackmail
 
Biashara matangazo! Anachukua initiative ya kusaka wateja. It is allowed, kosa lake ni kuanza kukusanya data kabla ya initial contract na mteja (cheatwadi). Ila ni lazima afanye baseline survey anyway kujua kama kuna potential. Hehehee, umekamatika mwaka huu dingi, niunganishe nae nimuajiri kwenye kampuni,lol
Huyu mimi simfagilii, maana anafanya kama udaku................Kama ingekuwa anafanya hivyo baada ya kuombwa, basi isingekuwa ni jambo la kushangaza.................Lakini huyu anaangalia familia ambazo kipato kipo.........hasa kama mke anafanya kazi aua ni mjasiriamali, hapo anajua kuna dili.............lakini sisi ambao wake zetu ni wauza maandazi na chapati uswazi tumesalimika..............
 
Biashara matangazo! Anachukua initiative ya kusaka wateja. It is allowed, kosa lake ni kuanza kukusanya data kabla ya initial contract na mteja (cheatwadi). Ila ni lazima afanye baseline survey anyway kujua kama kuna potential. Hehehee, umekamatika mwaka huu dingi, niunganishe nae nimuajiri kwenye kampuni,lol
Mpaka sasa simjui na hata hao wanaume ambao ndoa zao zimeingia kizungumkuti hawajamjua kidudu mtu huyo.............Mie mwenyewe amenidokeza mama Ngina baada ya kumegewa siri na shogake..............Nimemuonya katu asije akamtumia huyo shushushu kunifuatilia...........Atajuta.................LOL
 
Anafanya kazi nzuri tuu ila asiseme au kutoa data za uongo atakuwa ameharibu kazi yake. Ingefaa pia asaidie na utoa data za wake za watu wanaotembea nje ya ndoa na za wanaume wanaoharibu watoto wa shule na za wamama watu wazima wanaowalea na kutembea na watoto wa kiume bila wazazi wao kujua na kukubaliana na hali halisi. Watu wakimuogopa Mungu kwa kutenda mema huyu jamaa wala hata kuwa na ajira hii tena, ajira hii tumempa wenyewe kwa kufanya umalaya.
 
muhahahahahahahahahah dah kweli udaku cio kwa shigongo tu.yan huyo anakulika mwizi balaa.naona vidume vinakoroma humu me namwmbia aendelee bnana wanaume mmezidi khaaa kwani anayokufanyia ashura y ucmwambie mkeo akufanyie?wel done kijana endelea kumulika wezi haooo....kakata dagaa pigaaa.dah huu uzi umenifurahisha kweli mtambuzi,halafu ulivyogomba inaonyesha unaogopa kumulikwa ndo maana umempiga mkwara mama nanilii.na bado zamu yako inakija huyo kijana c wa hapo mtaani kwenu?ha ha ha mtambuzi 40 yako imefika jiandae.
 
Kwa usalama wake kwanza anatakiwa ajitengenezee kinga, ajisajiri, awe na TIN #, leseni, awe na ofisi ambapo watu watamfuata na si yeye kuanza tu uchunguzi wake unaosimamia upande mmoja, awe na wasaidizi na ahakikishe anadhibiti mianya ya rushwa kwa wasaidizi wake.

Nakubali kazi yake kama ataiboresha, Babu najua tayari ushafungua BP hapo ulipo sina dawa zaidi ya kusema waache walee bibi bibi wa mtaa wa tatu na saba yasikukute madhila.
 
Labda tumshauri awe anachunguza pande zote...........!


Yaani hapo nakubaliana na wewe mkuu kwa 120%,huyo kijana anachokifanya si kibaya ili vidume ndo wanafanya ukware usiotakiwa,ukiona wote wanaomshambulia lazima watakuwa ni wakware wa kutupa,wewe una mkeo nyumba ndogo ya nini,ninyi ndo msababishao ukimwi usiishe na mnaongeza watoto wa mitaani,Kijana anitafute na mimi nimpe tenda,Kijana ana akili sana ya ujasiriamali aanzishe kampuni na aisajili kabisa ili asaidie kurejesha maadaili ya mtanzania ambayo yamepotea
 
Huyu kijana amegeuka kuwa hatari hapa mtaani ninapoishi. Mpaka sasa kuna ndoa kama saba hivi ambazo inaonekana jahazi linaelekea kuzama kutokana na ushushushu wa huyu kijana anayedai eti amejiajiri ili kujikimu na maisha.

Anachofanya ni kumfuatilia mume wa mtu ambaye anamhisi ni mkware, akishagundua ana nyumba ndogo mahali atahakikisha anajuana na hiyo nyumba ndogo ili apate taarifa za jamaa na ikiwezekana anampiga picha huyo nyumba ndogo kisha anamfuata mke wa jamaa na kujenga naye urafiki na wakizoeana anamweleza kwamba anayo siri kubwa na anaomba ahakikishiwe usalama wake.

Akihakikishiwa usalama wake anamuuliza mke wa muhusika, kama akimpa taarifa kuwa mumewe anayo nyumba ndogo pamoja na ushahidi atamlipa kiasi gani……………Mke akikubali dili, anamwaga siri zote pamoja na picha na details nyingi tu alizokusanya ili mke aweze kumulika mwizi.

Akishakabidhi ushahidi anakunja mkwanja wake kisha anasepa na kuacha timbwili nyuma………………Wanawake hapa mtaani wanampenda kweli na wanapeana namba zake za simu. Sasa hivi huyu kijana anatengezeza mkwanja ile mbaya. Ila nimesikia wanaume wanamuwinda ili wamfanyie kitu mbaya……………………..


Yaani hapo nakubaliana na wewe mkuu kwa 120%,huyo kijana anachokifanya si kibaya ili vidume ndo wanafanya ukware usiotakiwa,ukiona wote wanaomshambulia lazima watakuwa ni wakware wa kutupa,wewe una mkeo nyumba ndogo ya nini,ninyi ndo msababishao ukimwi usiishe na mnaongeza watoto wa mitaani,Kijana anitafute na mimi nimpe tenda,Kijana ana akili sana ya ujasiriamali aanzishe kampuni na aisajili kabisa ili asaidie kurejesha maadaili ya mtanzania ambayo yamepotea
 
Kwamba itapunguza Ukware? hio ni kudanganyana HP.... Hio ndoa itavunjika.... ikiwezekana mwanaume ataoa tena na atacheat vile vile.... na kwa upande mwingine siamini kua ndoa zote ambazo anachonganisha kweli zavunjika. Ingekua anapeleleza wanawake na kupelekea waume zao sawa! Katka ndoa ambazo zipo hadi sasa ni aslimia zaidi ya 60 ambayo wake imewatokea kujua kua mume wake alichepuka/anachepuka nje ya ndoa.....

AshaDii, nilikuwa najaribu kufikiria mbali kidogo kuwa, mtu ukishajua kuwa kuna watu ambao hufuatilia tabia zako, basi ni lazima utakuwa makini na mwenendo wako na pia waweza kufikiria kuachana na ukware. I mean hofu husaidia kupunguza kufanya maovu.
 
Cantalisia uko wapi,
babako anaogopa kufotolewa akiwa kwenye mawindo yake.
kijana anasaidia watu kuimarisha ndoa zao,
kama zinaa mkafanyie hukoooooo, na foleni ya bongo
sijui itakuwaje.
 
Duuuuuuuuuuuuuu! Aisee si muwatafute tu mateja wamfanyie kitu mbaya. Usikute naye anapenda sema tu anaona aibu kutsema
 
Mkuu Mtambuzi habari ya Mapinduzi,
maisha yanakwendaje lakini,
sasa hivi najua ndoa za mtaa wenu ni
shwari kabisa, akina mama ngina hawana
wasiwasi wa ma pe nzi tena wamepata msaada.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom