Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,669
- 4,919
Mchezo wa kabumbu, ujulikanao kama Mpira wa miguu, kwa kimombo Soccer au Football. Ni miongoni mwa michezo pendwa Duniani, na ni mchezo unaoshika nafasi ya kwanza duniani kwa kutizamwa na kufatilia. Kwa hapa Tanzania mpira wa miguu umekuwa una vipindi maalumu vya uchambuzi kwenye Radio na TV ukilinganisha na michezo mingine kama Mchezo wa ngumi, mpira wa kikapu na kadharika.
Kumekuwa na mijadala mingi kuhusu uhalali na uharamu wa mchezo wa mpira wa miguu kwenye Dini ya kiislamu. Wengi wakisema ni mchezo haramu, na hauruhusiwi katika Dini. Lakini cha kushangaza waarabu wenyewe ambao ndio Dini imetoka kwao ni wafuasi namba moja wa mchezo huo ambao hivi karibuni tumeona wamepindua meza kwa kuamua kusajilii miamba ya soka kutoka sehemu mbalimbali za ulaya na mabara mengine hili kuvutia Soka la uarabuni. Vivyo hivyo tumeona Mchezaji mpira "Christiano Ronaldo" akiwa kwenye basi mmoja katika jiji huko Nchini Iran 🇮🇷 ambayo ni nchi inayoongozwa kwa misingi ya kiislamu, lakini tuliona Ronaldo akikimbiliwa kama Masiha au Mwokozi, na watu wa Iran. Hata hapa tunaona watu walioshika Dini mfano haji Manara kila Mwaka anaenda kuhijj Macca na sehemu takatifu za urabuni na kuhubiri Dini lakini pia ni muumini mzuri wa mpira wa miguu.
Na Nchini pia tunaona Masheikh wengi wakiwa misikitini wanahubiri mpira ni haramu lakini wao ndio namba moja wanaokwenda kutizama soka, mfano nilienda Jijini Mwanza wilaya ya Sengerema, kuna msikiti hupo mjini alafu kwenye njia ya kuingilia msikitini kuna vibanda viwili vya kahawa vyenye TV ambavyo watu wakitoka kuswali upumzika hapo kunywa kahawa na mazungumzo ya hapa na pale, ila vibanda hivi ufurika siku za mechi ya Simba na Yanga na mechi nyingine za kuvutia, na wanaokaa hapa wengi wao ni waislamu ambao wanataka kuingia msikitini au wanaotoka kuswali msikitini.
Kwa anayefahamu, tunaomba maelezo pia kama ikiwezekana na vifungu vya Quran kwamba mpira ni haramu... Maana wengine wanasema vitu ambavyo havikufanywa na mtume vingi ni haramu, na mwingine akauliza mtume alihubiri kwa kutumia kifaa gani, sasa kwa nini hawa masheikh wanatumia Microphone. Na kadharika sasa tunaomba ufafanuzi kuhusu mpira wa miguu juu ya uharamu wake.
View: https://www.instagram.com/reel/Cv5i1zWrLAy/?igshid=MzRlODBiNWFlZA==