MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,976
Wakati nchi za dunia ya kwanza/zilizoendelea zikipigana vikumbo kuhusu masuala ya kutawala kiuchumi, nchi za dunia ya tatu/zinazoendelea zinasubiri matokeo hayo ili kujua ukubwa wa athari kiuchumi katika nchi hizo.
Kinachoendelea katika nchi za Amerika ya Kaskazini kuhusu makubaliano ya NAFTA (The North American Free Trade Agreement) kinagusa kwa karibu uchumi wa nchi za Amerika ya Kusini ambao umejumuisha nchi nyingi za dunia ya tatu/zinazoendelea.
Vile vile kinachoendelea katika nchi za Ulaya kuhusu BREXIT (British exit) kinagusa kwa karibu uchumi wa nchi za Afrika ambao umejumuisha nchi nyingi za dunia ya tatu/zinazoendelea.
Kuna methali inayosema, ''wapiganapo tembo nyasi huumia. Hii ina maana kuwa zipiganapo nchi zinazoongoza kiuchumi, nchi masikini kiuchumi huumia.
Mkwara wa Marekani kwa Mexico ambayo nchi nyingi za Amerika ya Kusini zilikuwa zinaitegemea katika mapambano na Marekani kuhusu NAFTA kulifanya nchi hiyo kukubali masharti ya Marekani ambayo yanaziumiza kiuchumi nchi za Amerika kusini. Kwa maana nyingine, nchi za Amerika ya Kusini zilidhani Mexico ina nguvu mbele ya Marekani wakati kiuhalisia hakuwa nazo.
Yanayoendelea kwenye suala la BREXIT huko Ulaya ambapo Uingereza inapambana katika meza ya makubaliano ya kiuchumi, kisiasa na kijamii na Nchi zingine za Umoja wa Ulaya kinaonyesha kuwa ile nguvu ambayo nchi nyingi za Afrika zilidhani Uingereza inazo kumbe haina.
Tanzania tumekataa kuingia Mkataba wa EPA (Economic Partnership Agreements) na Nchi za Umoja wa Ulaya kwa kuitegemea Uingereza tukidhani ina nguvu za kiuchumi na kiushawishi lakini kinachoendelea kinaonyesha Uingereza haina nguvu ya kiushawishi, kiuchumi na kijamii mbele ya Nchi zingine za Umoja wa Ulaya.
Nchi za Umoja wa Ulaya kwa sasa zinaipiga mkwara Uingereza kama ilivyofanya Marekani kwa Mexico ili kuilazimisha Uingereza kuingia makubaliano ambayo kwa kiwango kikubwa yananufaisha nchi zitakazobaki kwenye Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU). Waingereza kwa sasa hasa wananchi wa kawaida wanajuta kwa nini waliamua kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya baada ya kugundua nchi yao haina uwezo wa ushawishi na nguvu nje ya Umoja wa Ulaya. wanawalaumu wanasiasa wao kwa kuwadanganya kuhusu nguvu na uwezo wa Uingereza kwenye Umoja wa Ulaya. Kuna kampeni inaendelea ili kumshinikiza Waziri Mkuu ajiuzulu.
Baada ya kumalizana na Uingereza, nchi za Umoja wa Ulaya zitaigeukia Tanzania kwenye suala la EPA kwa sababu Tanzania ndio kizingiti kikuu kwenye haya makubaliano kwa nchi za Afrika Mashariki.
Yanayoendelea kwa sasa kati ya Tanzania na Jumuiya ya Ulaya ni mvua za rasharasha tu, bado mvua za masika kuanza kunyesha.
Kama Uingereza imeweza kupigwa mkwara na kuanza kulia kulia, Tanzania ambayo iliitegemea Uingereza kuwa kama ngao yake itaweza vipi kupambana na Umoja wa Ulaya?
Je, tunakoelekea kuhusu suala la EPA, viongozi wetu wakuu pamoja na bunge watageuka jiwe kama ule mfano wa ruthu kwenye Maandiko ya Biblia ili wakiepuke kikombe cha ghadhabu za Umoja wa Ulaya?
Kwa wasiojua kuhusu EPA gonga hii LINK>>>Tanzania Yachomoa Kusaini Mkataba wa EPA - JamiiForums
Nakumbuka Mwl Nyerere alipokataa kugeuka jiwe baada ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na pia Benki ya Dunia (WB) kumtaka kushusha thamani ya Shilingi pamoja na kufanya marekebisho kwenye mashirika mengi ya umma, ambayo yalionekana yakijiendesha vibaya tulijikuta kama taifa kwenye hali mbaya sana kiuchumi kiasi kwamba alilazimika ‘’kung’atuka’’ ili kutunza heshima yake!