Uhusianao kati ya Nape na Pro. Mwandosya ni wa KIITIKADI au?

Status
Not open for further replies.
Huyu Jamaa mbona katoweka, maana mi sijaelewa nini kinaendelea hapa!

Hapa ni Nape anashambuliwa na kunyang'anywa U-bin kabisa au kuna nini jamani wana-JF? Mnataka kusema ukiweka hizo picha ndio tutamtambua babae au?

Nilisema CCM haivuki septemba hii subiri baada ya NEC-CCM kama ikivuka mtaniambia, pia nilimwambia Dr. Slaa hasisumbuliwe na kelele za Nape juu ya kikao cha muhafaka maana CCM yenye ina migogoro mpaka imeinama mgongo kwa kubeba migogoro lakini imewashinda kuimaliza. Huyu Jamaa hasipo rudi hapa kuweka hii stori yake sawa na wazi nashauri Mods wafunge hii thread maana haieleweki labda kwa wale walioandika nae.
 
Jamaa kajiunga JF jana (tarehe 29 August 2011) na kutoa madongo mazito namna hii!!! Kweli mwaka huu magamba hayavuki... Nape ndugu yangu niaje hapa!?
 
Hakika unakitu kizuri ulichotaka kutwambia ila walio wengi hawaelewi aina ya uhandishi au style uliyotumia kufikisha ujumbe.Kwa ujumla ujumbe wako kwa watu makini wamekuelewa unataka kusema nini?Ila umeonyesha tu kuwa umeside upande gani japo kuwa umesema mambo ya kweli ambayo yako upande wa pili wa shilingi.Kibaya kuwa huyu uliyeside kwake kwa mujibu wa kuelewa kwako na ufafanuzi wako ni kuwa uwakilishi wako wa ujumbe ungesimama kusema ya upande wake pia kama ulivyozunguza ya upande wa pili.

Huku jamvini huyo ulieside kwake uwa HAUZIKI HATA KIDOGO,ni kana kwamba angejua siasa za Tanzania na mwendendo wake pamoja na kuwa alishafika ngazi kubwa angejiepusha akajishughurisha na biashara zake kama swaiba wake,kulikoni manake wakimchoka watamsambaratisha hata kidogo alichpaswa kubaki nacho watakomba.

Kila mcheza uchafu anafikilia na kujiona anauwezo wa kuyafanya yale ya ndoto zake yatimie,wanatabia moja utumia kukupima upeo wako kama kukushauri mzee wewe bado unakubalika,akizisikiza sauti hizo za wapambe hakika vitanda vitakuwa vingi kila mmoja kwa wakati wake.

Na kwakuwa kila mmoja ana mabilioni yake,kinachofanyika ni kuzitawanya ili kila mmoja kwa kutokuwa na ufahamu anafikilia kuwa Rais wa Tanzania lakini hatimae wataishi kumalizana kwa kuviziana kwenye chupa za maji ya salama.

Ugomvi wa panzi furaha ya kunguru,wote wanaongaika urais wa Tanzania kwa kujipenyeza kwa michezo michafu hakika wasahau.Japo wanaamini wana uwezo tunawasubiria.

Ila huyo mdau wa upande wako,sio mbaya wakati mwiingine akatafuta wazee walioko mitaani hawaulize kama kweli anaweza kuipata nafasi hiyo inawezekana hata mama Tanzania alishakasilishwa na unganganizi wake usio kuwa na chembe ya busara.

Kati yao wote wanaoangaikia urais hakuna hata mmoja wao atake kuwa Rais wa Tanzania,hata Rais mwenyewe itamuia vigumu kuliona ilo atampa nafasi kama yeye alivyoipewa bila kutegemea.

Nikushukuru sana ndugu yangu na nimependezwa sana na RED na naomba iwe hivyo na naamini Rais atatoka kwa Watanzania na si katika Makundi na nikujulisha wazi huyo unayesema labda nimeside kwake siku moja ningefurahi sana nikutane naye uso kwa uso na nimweleze (japo naamini anajua) Watanzania wanafikiri nini juu yake nami nipate kujua yale aliyo nayo. Hivyo kama kwa kutaja jina la mtu imeleta maana tofauti au uandishi nao umekuwa wa utata nakubali KOSA kwa moyo mkunjufu kabisa na marakebisho mengine yeyote ila ntarudia tena Katibu si mtu wa kutupiana maneno au kumtusi Dr. Slaa, Edward na viongozi wengine eidha waliopo Serikali au Wastaafu atafute namna nyigine kukijenga chama.
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Jamaa kajiunga JF jana (tarehe 29 August 2011) na kutoa madongo mazito namna hii!!! Kweli mwaka huu magamba hayavuki... Nape ndugu yangu niaje hapa!?

Kujiunga jana au hata leo jioni hakumaanishi kwamba hufahamu au hujawahi kujua yaliyopo au yanayojiri nchini au duniani.
 
Huyu Jamaa mbona katoweka, maana mi sijaelewa nini kinaendelea hapa!

Hapa ni Nape anashambuliwa na kunyang'anywa U-bin kabisa au kuna nini jamani wana-JF? Mnataka kusema ukiweka hizo picha ndio tutamtambua babae au?

Nilisema CCM haivuki septemba hii subiri baada ya NEC-CCM kama ikivuka mtaniambia, pia nilimwambia Dr. Slaa hasisumbuliwe na kelele za Nape juu ya kikao cha muhafaka maana CCM yenye ina migogoro mpaka imeinama mgongo kwa kubeba migogoro lakini imewashinda kuimaliza. Huyu Jamaa hasipo rudi hapa kuweka hii stori yake sawa na wazi nashauri Mods wafunge hii thread maana haieleweki labda kwa wale walioandika nae.

Hakuna anaye mshambulia Nape wala kutaka kumnyang'anya Ubin wake ila kama lisemwalo halipo basi laweza kuja nimshukuru KABEMBE, na LUKINDO wameshanipa reference and I'll accord with....
 
you have talked a lot but you have said nothing....come again and tell what you wanted to say.
<br />
<br />
alitaka Kusema kuwa Nape anajipakazia, anadanganya, anasema uongo kuwa late Moses Nnauye ni babake.
Mke wa Nnauye aliwahi kumkana Nape kuwa si mmoja wa watoto wa mzee yule.
Kifupi Nape ni Mnyakyusa wa Rungwe mkoani Mbeya.
 
Kweli wewe ni nguvumali nakushukuru sana mzee kwa kunisaidia hilo na kwa kunipa reference ya muhusika kabisa manake siku zote waungwana husema ajuaye baba wa mtoto ni mama...... Meksi Monsier....... Dieu vous benise.....
 
Wana JF,
NIMESOMA KWA KITUO MAELEZO YA MTOA MADA NA KWAKWELI SIKUSHANGAA KWASABABU HOJA HII HAIJAANZA KUSEMWA JANA....WAFUATILIAJI WA MAMBO WATAKUMBUKA HOJA HII ILIANZA KUSEMWA MWAKA 2003 NILIPOAMUA KUKATAA KUWEKWA KWENYE BOX NISIGOMBEE UENYEKITI WA VIJANA TAIFA... WAKATI ULE ILIKOSA MASHIKO NA KUISHIA KUANDIKWA NA BAADHI YA MAGAZETI NA IKAPOTEA... LAKINI HAPA NIKIRI KUWA WALIOANZISHA HOJA HII WAKATI ULE NDIO BAADHI YAO WANAOJARIBU KUITUMIA LEO NA SABABU KUBWA NI ZILEZILE, ZA KUKATAA KUTUMIKIA WATU BINAFSI BADALA YAKE KUIWEKA NCHI MBELE NA KUWA MWAMINIFU KWA TAASISI BADALA YA MTU....
KINACHOJARIBU KUFANYWA HAPA NA MTOA MADA NI MAKUBALIANO YA KIKAO CHAO KILICHOFANYIKA MOROGORO MARA TU BAADA YA KUMALIZIKA KWA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA ILIYOFANYA MAAMUZI YA KU- REFORM CHAMA. KATIKA KIKAO HICHO KULIJADILIWA WAJUMBE WOTE WAPYA WA SEKRETARIETE PAMOJA NA MAMBO MENGINE ULIPITISHWA UAMUZI WA KUTUMIA HOJA YA UHUSIANO ULIO" tungwa" KATI YA NAPE NA MWANDOSYA KUJARIBU KUMCHAFUA NAPE... NA HII ILIAMULIWA BAADA YA KURIDHIKA KUWA " NAPE ANACHAFUA KITUMBUA KWA MSIMAMO WAKE MKALI JUU YA MATUMIZI MABAYA YA RASILIMALI ZA UMMA"......(ufisadi)....

SWALA LA MIMI (kuwatukana viongozi/wazee)... MPAKA LEO HAJATOKA MTU HADHARANI ASEME KWA USHAHIDI KUWA NILIYOYASEMA NA KUYASIMAMIA BAADA YA VIKAO VYA CHAMA DODOMA HAYAKUAMULIWA KWENYE KIKAO. ISITOSHE MPAKA SASA TUMESHA KUTANA MARA MBILI KIKAO CHA KAMATI KUU AMBACHO KWA MUJIBU WA KATIBA YA CCM NDICHO KINACHOANGALIA NA KUSIMAMIA MWENENDO WA UTEKELEZAJI WA MAAMUZI YA CHAMA, VIKAO VYOTE VIWILI KWA KAULI MOJA VIMEPONGEZA UTEKELEZAJI WA MAAMUZI YA CHAMA, SASA HOJA YA KUFANYA MAMBO YANGU INATOKA WAPI KAMA SIO SARAKASI ZA WANAOTAKIWA KUWAJIBIKA KUJARIBU KUUHADAA UMMA???
HAYA YANAYOSEMWA MATUSI NI YAPI,?? HIVI LEO KUSEMA HATUUNGI MKONO UFISADI INAGEUKA KUWA MATUSI? TUNATAKA KUPELEKA WAPI NCHI YETU? NAPE AKIULIZA JUU YA MATUMIZI MABAYA YA RASILIMALI YA UMMA INAGEUKA KUWA NI KUWAKOSEA HESHIMA WAHUSIKA( hapa mfano kuhoji kutolipa kodi kwa Dr. Slaa na wenzake) ...MBONA YEYE AKIHOJI MATUMIZI YA RASILIMALI ZA NCHI HATA AKIMTAJA RAIS AU YEYOTE INACHUKULIWA NI USHUJAA NA UZALENDO SIO MATUSI KAMA AMBAVYO MNATAKA WATU WAAMINI HAPA????
AKISEMA NAPE MATUSI,KUKOSA ADABU NA KUTOJUA NAFASI YAKE, AKISEMA MWINGINE NI USHUJAA NA UZALENDO... NENDA LEO MASASI KAULIZE NAPE ALIFANYAJE KAZI ZAKE, UTAPATA MAJIBU, NATHUBUTU KUSEMA NIMEWATUMIKIA WANA MASASI KWA NGUVU ZANGU ZOTE, MOYO WANGU WOTE NA AKILI YANGU YOTE.... NA NDO MAANA LEO WANAKUMBUKA KAZI NILIYOIFANYA BILA KUJALI ITIKADI ZAO...
MENGINE HAYA YA SIJUI KWENDA TRIPOL NA KWINGINE SIJUI KUCHUKUA PESA NI UONGO USIOKUWA HATA NA RANGI COZ SIJAWAHI KUFIKA TRIPOL MAISHA YANGU YOTE SASA UONGO MWINGINE....
NAOMBA NISISITIZE......UTARATIBU WA KUJARIBU KUJISAFISHA KWA KUJARIBU KUCHAFUA WENGINE HAKUWEZI KUWAFANYA WENGINE WASAFI NA KUHALALISHA MATUMIZI MABAYA NA MABOVU YA RASILIMALI ZA UMMA..
NIOMBE YEYOTE MWENYE USHAHIDI WA NAPE KUTUMIWA KUMSEMEA MTU BINAFSI AUWEKE HAPA NAMI NITAWAJIBIKA KWA HILO, KWANI SIJAWAHI KUTUMIA, NA SITATUMIWA NA MTU BINAFSI KWA FAIDA BINAFSI, NCHI KWANZA MENGINE, MENGINE BAADAE
 
Tuna mambo mengi ya muhimu kuyashughulikia sasa kama umeme, mafuta n.k. Haya ya urais tuyaweke kiporo...
 
Mosi, binafsi nikushukuru sana Mhe. Katibu sana sana na kwa moyo wangu wa dhati kabisa kabisa kwa ufafanuzi huo. Lakini pili kama ulivyokiri haya si ya leo wala ya jana nami niseme tu kwamba haya vile vile hayawezi kubatilisha nafasi uliyo nayo ila kama nilivyotangulia kusema awali nilitaka kujiridhisha binafsi manake uongozi wa nchi hii unavyokwenda nasi tunapata shaka manake kama kweli huyo anayesemwa kuwa ni baba ako kama akiwa Raisi binafis sitazamii wewe kubaki kuwa Katibu (haya tunayaona wazi).

Lakini tatu hicho kikao ulichosema cha Morogoro sijajua ni cha nini na nani vile vile hivyo kwangu hiyo si hoja. Umesema umepongezwa na vikao husika vya chama ni sawa na ni haki vile vile upongezwe nacho ila ifikie mahali watanzania nao wakupongeze kama ulivyosema watu wa Masasi manake nchi hii ina vyama vingi sasa kupongezwa na chama kimoja bado haijakaa vizuri. Hivyo naamini kwa kusimamia Chama chako vizuri kama wafanyavyo baadhi ya Wabunge wa Chama chako sisi Watanzania hatutasita kukupongeza vile vile.

Nikubaliane na wewe moja kwa moja kwamba ni kweli kabisa hujawahi fika Tripoli manake hata mtoa mada hakusema ni wewe bali ni mmoja wa Mawaziri hivyo hili nalo lilihitaji marekebisho manake naamini wewe si Waziri. Lakini kwa upande wa Dr. Slaa umesema yeye anahoji Rasilimali za nchi (emphasis added) na pili umesema akimtaja Rais, nadhani si lengo la mada hii kujadili faida za vyama vingi na kazi zake ila tambua kuhoji juu ya Rasilimali za nchi hayo ndiyo mambo tunayohitaji. Masasi nitazungumza nao na pongezi zako nitaziwakilisha vile vile.

Na mwisho nimependa sana Slogan yako ya Taifa kwanza........... very impressing na hili ndiyo tunu kwangu na hata Taifa ila katika hili nimekuwa nikipita katika Afisi mbali mbali za CCM na kuona baadhi ya maandiko mathalan "Chama kwanza mtu baadae" sasa nadhani ukiwa kama Katibu msimamo wako ufike mpaka huko manake hili la Chama kwanza nao ni utata....... Nirudie kukushukuru sana...
 
Nape nakukubali uko vizuri na unapigania sana kukipa uhai chama chako kinachoelekea
kaburini. Lakini mnakosea sana kimkakati. Magamba yamewazunguka mpaka haujui yupi
yuko kambi gani. Na hii yote ni ile tabia ya kusitasita kimaamuzi mliyonayo CCM.

Tatizo wenyewe mnafuga magonjwa ndani ya chama. Na bado, propaganda
chafu zitaibuka kila siku midhali mnalea magonjwa. Hivi katika wanachama millioni 5,
hamuoni aibu mnashikiwa ransom na kikundi cha watu wasiozidi 1,000?

Ufisadi ni kama kansa. haijalishi iko kidoleni au kwenye mguu, usipokata kiungo
husika hatimaye nawewe utakufa siku si zako. Tatizo hili kundi la watu 1,000 wote hao
watatakiwa walipwe fadhila pindi mtu wao akikaa ikulu. Sasa tunajenga nchi au tunabomoa?

Kama mmeamua kuwavua uongozi watuhumiwa ufisadi basi kwa kauli moja wavueni,
kama mmeamua mnalea ugonjwa basi kaeni kimya musubiri mauti yawakute. Mtabadili kauli
mbiu mtakavyo lakini wananchi wamechoka na ghiliba wanataka real actions.

Hizi blabla zenu kila siku ndio maana watu wanashindwa kujenga nchi wanabaki wanajadili
mambo hayohayo, miaka 5 mizima, ufisadi, ufisadi, hatua madhubuti hakuna. Kazi hazifanyiki
kero za mgao wa umeme, mara mafuta, huku mafisadi wakizidi kuchekelea tu mtaani.

Watu mmeshika dola halafu mnawagwaya mafisadi, hivi mnatoa ujumbe gani kwa raia?
Kila siku danadana, na kikao cha septemba mkipiga danadana mujue ndo kwisha, mmejizika!
 
Usipende sana Madesa penda kusoma na vitabu vile vile mzee..... anyway your wish is granted manake nimeshajua wewe ni mtu wa namna gani.

usitoke nje.sisemi usiandike barua ndefu.andika barua ndefu,lakini achana na mafumbo ili wote tukuelewe.nadhani ndiyo lengo la jf ikiwa ni pamoja na kupashana habari na kuelimishana,siyo kufumbiana mafumbo kama kwenye nyimbo za kina khadija kopa
peace out
 
Mkuu nnauye jr, hiyo ya morogoro imekaa njema sana ukiiongezea nyama. Naona mnajuana sana na mmeamua kutupatia tusiyoyajua. Asante na twende kazi sasaaaa.
 
Hapa labda ukajipange na uje kivingine maana hapa umechemka, umetumia maneno mengi na kujaribu kuzunguka mbuyu ili hali ulichotaka kukizungumzia ni kimoja, hayo makundi yenu kwenye chama cha magamba sisi hayatuhusu na hatupo tayari kutoa msaada wowote kwa sababu mlipoyaanzisha hamkutushirikisha iweje leo unakuja na stori za ajabu tena kwa kujaribu kutufumba ila kwa kuwa sisi ni great thinkers hatuna shaka yoyote labda hao magamba wenzio waambie wakusaidie, sorry kwa hili
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom