Uhuru wetu hautoki kwa Kikwete au Rais yeyote; Rais hawezi kuwa "Dikteta kidogo"

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Ninaendelea kuonesha makosa ya kimantiki na kifalsafa ya hotuba ya Rais Kikwete jana. Mojawapo ya mambo ambayo aliyadai akikanusha kuwa yeye si Dikteta ni kauli hii ambayo sidhani kama watu waliielewa uzito wake. Rais alidai kitu kingine ambacho nacho pia hana!

Juzi Bungeni msemaji wa kambi ya upinzani, katika mjadala wa Muswada wa Kuunda Tume ya Kukusanya Maoni alisema Rais ni dikteta. Ama kweli “akutukanae hakuchagulii tusi” kama ulivyo msemo wa Kiswahili. Hivi mimi kweli ni dikteta? Kwa jambo lipi? Hivi ndugu zangu Rais dikteta anatoa uhuru mkubwa kama uliopo sasa wa vyombo vya habari na wa watu kutoa maoni yao? Kama mimi ningekuwa dikteta kweli nina hakika hata yeye asingethubutu kusema hivyo na kama angethubutu basi mpaka sasa asingekuwa anatembea kwa uhuru.

Mimi ninachofahamu ni kuwa nasemwa kwa kuwapa watu, vyama vya siasa na vyombo vya habari uhuru mkubwa mno ambao watu wanaona unatumika vibaya kusema maneno yasiyokuwa na staha au hata matusi, fitina na kupandikiza chuki katika jamii. Labda, nijaribu kuwa dikteta kidogo watu waone tofauti yake. Naamini kungekuwa na malalamiko makubwa zaidi ya haya.

Rais amedai vitu ambavyo vinahitaji kukataliwa mara moja kwa sababu tukivukubali tu tunampa nguvu ambazo hana.

1. Rais ndiye anayetoa uhuru wa kutembea, vyombo vya habari na hata kuwa (the freedom to be)
2. Rais ndiye anayetoa uhuru kwa watu, vyama vya siasa tena "mkubwa mno"
3. Anaweza kuingilia kati uhuru huo kwa kuwa "dikteta" kidogo.

Ndugu zangu, Uhuru wa Watanzania hautoki kwa Rais - awe Kikwete au yeyote mwingine. Katiba yetu inasema hivi kuhusu uhuru wetu: (Ibara ya 12:1)

Binadamu wote huzaliwa huru, na wote ni sawa.

Maneno hayo yanaweza kuonekana ni shallow au hollow lakini ni makubwa sana. Yanatueleza kwamba kila Mtu (mimi, wewe, mtoto, mzee, kijana, msomi, mjinga, kichaa, mwenye akili sana, mlevi, mzinzi hata shoga!) huzaliwa 'HURU NA SAWA'! Kwa maneno mengine uhuru wetu hautokani na rais au chama cha siasa unatokana na kuzaliwa kwetu kama BINADAMU. Ndio maana tunasema "binadamu wote huzaliwa huru na wote ni sawa".

Kwa hiyo, hoja ya kuwa uhuru wetu unatoka kwa rais au kwamba RAis anafikiria kuwa sisi tuko huru kwa sababu kaamua kutugea uhuru haina msingi, ni ya kukataliwa na kwa mara nyingine haina msingi wa Kikatiba (lacks constitutional basis whatoever).

NI kutoka katika kutambua kuwa sote tunazaliwa huru ndipo Katiba sasa inatambua uhuru huo na kuuhakikisha (the constitution recognizes and guarantee that freedom). Kumbe wananchi wanazaliwa wakiwa huru na kwa kutumia katiba yao wanajihakikishia uhuru huo - Rais hatoi wala kuhakikisha uhuru huo bali anasimamia kuwa uhuru huo hauondolewo - iwe na maadui wa ndani au wa nje - na hii ina maanisha hata na yeye mwenyewe!

Je ni uhuru gani tunazaliwa nao ambao hauwezi kuondolewa kiholela kama Rais alivyoashiria? Nitataja tu kama Katiba inavyoanisha sasa:

Uhuru wa kuwa hai (rais hawezi kuja na kumwambia polisi 'mpige huru risasi' halafu mtu akapigwa risasi kwa vile 'rais kasema'). Ili kuhakikisha hili Katiba imeweka wazi kuwa "itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kukamatwa, kufungwa, kufungiwa, kuwekwa kizuizini, kuhamishwa kwa nguvu au kunyang'anywa uhuru wake". Kwa maneno mengine ni kuwa kauli ya Rais anaweza kuwa dikteta kidogo na kuzuia uhuru wawatu haina msingi ni ya kuikataa kwani hana madaraka wala uwezo huo (nililisema hili siku ile aliposema Bungeni kuwa angeweza kuagiza Dr. Slaa akamatwe na akakamatwa)!

Uhuru wa mawazo na maoni - kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta,
kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa
mawasiliano yake kutoingiliwa kati.
Kwa maneno mengine ni kuwa hakuna mtu anayeweza kumlazimisha mtu mwingine kufikiri au kuwa na maoni anayoyataka yeye! Kiila mtu anahaki ya kufikiri na kujenga maoni ayapendayo yeye bila kulazimishwa. Hii ina maana kuwa uhuru huu hautoki kwa Rais. Rais hawezi kutuambia kuwa sote tunatakiwa kufikiria hivi au vile na tukifikiri tofauti basi ni makosa!

Uhuru wa imani
- Katiba inatambua kuwa kila mtu ana uhuru wa kuamini au kutoamini dini yoyote. Na katiba yetu inaenda mbali zaidi na kusema kuwa mtu anayo haki ya kubadilisha imani yake. Kwa maneno mengine mtoto aliyezaliwa katika familia ya kikristu akiamua kuwa Muislamu serikali au mtu yeyote hawezi kwenda na kumlazimisha abadili. Wanaweza kumshawishi au kumuonesha makosa lakini mwisho wa siku uamuzi ni wake. Na mtu akiamua kutoamini Mungu au akiamini minazi hakuna mtu wa kumlazimisha kuwa abadili imani! Rais hawezi kulazimisha watu waamini vyovyote apendavyo yeye.

Hiyo ni mifano michache tu. Kwa ufupi ni kuwa kauli ya Rais kuwa yeye ndiye anatoa uhuru na kuwa anaweza kuuondoa uhuru huo wa kuwa "dikteta kidogo" haina msingi. Uhuru wetu hautoki kwa Rais. Period.
 
Hivi niambieni haikuwa busara kwamba tungerekebisha baadhi ya vifungu vya sasa kwenye katiba tunayoitumia ili kupuguza madaraka yake na kuongeza vipengele vinavyofanya serikali na dola iwe juu ya wananchi ,kwa kweli kulikuwa na maeneo mengi kwenye hotuba yake ambayo yametupa kiulizo ,manake huelewi alikuwa anatueleza kama taifa maamuzi yake au na yeye alikuwa anaendeleza mipasho lakini kwa lugha ya chini
 
Ninaendelea kuonesha makosa ya kimantiki na kifalsafa ya hotuba ya Rais Kikwete jana. Mojawapo ya mambo ambayo aliyadai akikanusha kuwa yeye si Dikteta ni kauli hii ambayo sidhani kama watu waliielewa uzito wake. Rais alidai kitu kingine ambacho nacho pia hana!

Rais amedai vitu ambavyo vinahitaji kukataliwa mara moja kwa sababu tukivukubali tu tunampa nguvu ambazo hana.

1. Rais ndiye anayetoa uhuru wa kutembea, vyombo vya habari na hata kuwa (the freedom to be)
2. Rais ndiye anayetoa uhuru kwa watu, vyama vya siasa tena "mkubwa mno"
3. Anaweza kuingilia kati uhuru huo kwa kuwa "dikteta" kidogo.

Ndugu zangu, Uhuru wa Watanzania hautoki kwa Rais - awe Kikwete au yeyote mwingine. Katiba yetu inasema hivi kuhusu uhuru wetu: (Ibara ya 12:1)

Maneno hayo yanaweza kuonekana ni shallow au hollow lakini ni makubwa sana. Yanatueleza kwamba kila Mtu (mimi, wewe, mtoto, mzee, kijana, msomi, mjinga, kichaa, mwenye akili sana, mlevi, mzinzi hata shoga!) huzaliwa 'HURU NA SAWA'! Kwa maneno mengine uhuru wetu hautokani na rais au chama cha siasa unatokana na kuzaliwa kwetu kama BINADAMU. Ndio maana tunasema "binadamu wote huzaliwa huru na wote ni sawa".

Kwa hiyo, hoja ya kuwa uhuru wetu unatoka kwa rais au kwamba RAis anafikiria kuwa sisi tuko huru kwa sababu kaamua kutugea uhuru haina msingi, ni ya kukataliwa na kwa mara nyingine haina msingi wa Kikatiba (lacks constitutional basis whatoever).

NI kutoka katika kutambua kuwa sote tunazaliwa huru ndipo Katiba sasa inatambua uhuru huo na kuuhakikisha (the constitution recognizes and guarantee that freedom). Kumbe wananchi wanazaliwa wakiwa huru na kwa kutumia katiba yao wanajihakikishia uhuru huo - Rais hatoi wala kuhakikisha uhuru huo bali anasimamia kuwa uhuru huo hauondolewo - iwe na maadui wa ndani au wa nje - na hii ina maanisha hata na yeye mwenyewe!

Je ni uhuru gani tunazaliwa nao ambao hauwezi kuondolewa kiholela kama Rais alivyoashiria? Nitataja tu kama Katiba inavyoanisha sasa:

Uhuru wa kuwa hai (rais hawezi kuja na kumwambia polisi 'mpige huru risasi' halafu mtu akapigwa risasi kwa vile 'rais kasema'). Ili kuhakikisha hili Katiba imeweka wazi kuwa "itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kukamatwa, kufungwa, kufungiwa, kuwekwa kizuizini, kuhamishwa kwa nguvu au kunyang'anywa uhuru wake". Kwa maneno mengine ni kuwa kauli ya Rais anaweza kuwa dikteta kidogo na kuzuia uhuru wawatu haina msingi ni ya kuikataa kwani hana madaraka wala uwezo huo (nililisema hili siku ile aliposema Bungeni kuwa angeweza kuagiza Dr. Slaa akamatwe na akakamatwa)!

Uhuru wa mawazo na maoni - kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta,
kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa
mawasiliano yake kutoingiliwa kati.
Kwa maneno mengine ni kuwa hakuna mtu anayeweza kumlazimisha mtu mwingine kufikiri au kuwa na maoni anayoyataka yeye! Kiila mtu anahaki ya kufikiri na kujenga maoni ayapendayo yeye bila kulazimishwa. Hii ina maana kuwa uhuru huu hautoki kwa Rais. Rais hawezi kutuambia kuwa sote tunatakiwa kufikiria hivi au vile na tukifikiri tofauti basi ni makosa!

Uhuru wa imani
- Katiba inatambua kuwa kila mtu ana uhuru wa kuamini au kutoamini dini yoyote. Na katiba yetu inaenda mbali zaidi na kusema kuwa mtu anayo haki ya kubadilisha imani yake. Kwa maneno mengine mtoto aliyezaliwa katika familia ya kikristu akiamua kuwa Muislamu serikali au mtu yeyote hawezi kwenda na kumlazimisha abadili. Wanaweza kumshawishi au kumuonesha makosa lakini mwisho wa siku uamuzi ni wake. Na mtu akiamua kutoamini Mungu au akiamini minazi hakuna mtu wa kumlazimisha kuwa abadili imani! Rais hawezi kulazimisha watu waamini vyovyote apendavyo yeye.

Hiyo ni mifano michache tu. Kwa ufupi ni kuwa kauli ya Rais kuwa yeye ndiye anatoa uhuru na kuwa anaweza kuuondoa uhuru huo wa kuwa "dikteta kidogo" haina msingi. Uhuru wetu hautoki kwa Rais. Period.
Ile hotuba ya jana kwa kweli ndiyo maana alienda kuongea na hao "wazee wa Dar" halafu eti kuna wanoadai ni ya kitaifa?

Zile zilkuwa porojo kwa kiasi kikubwa,kama tu za kwenye ghahawa.

Inaonyesha wazi kabisa kuwa viongozi walioko madarakani hawafanani na sisi hata kidogo.

Sometime huwa najiuliza,hivi iilkuwaje hawa ndiyo wanatutawala?
 
Ile hotuba ya jana kwweli ndiyo maana alienda kuongea na hao "wazee wa Dar" halafu eti kuna wanoasdai ni ya kitaifa?

Zile zilkuwa porojo kwa kiasi kikubwa.

Inaonyesha wazi kabisa kuwa viongozi walioko madarakani hawafanani na sisi hata kidogo.

Mkuu jmushi1, mie nilitabiri hapa jana kabla hata msanii hajazungumza baada ya kufuatilia hotuba zake za nyuma kwamba hakutakuwa na lolote la maana katika hotuba hiyo zaidi ya blah blah ambazo hazina kichwa wala miguu. Na utabiri wangu ukawa kweli. Yaani unasikia hata uvivu kumsikiliza akiendeleza usanii wake halafu huku wakithubutu kuita Serikali yake eti ni "Serikali Sikivu" Sijui ni lini walianza kuwa wasikivu.
 
Asante tena MM, endelea na kazi nzuri Mh.

Nakiri mi wala sikuwa na muda wala utashi wa kumsikliza. Eti hivi huyu jamaa kweli ni Rais?

Nampinga Kikwete na kupinga kwa nguvu zote maneno uliyonukuu hapo juu. Samahani wadau inabidi niwe makini hapa, it's too provocative.
 
Mkuu MMJ jamaa alikurupuka hat speech ilikuwa ya kukurupuka jambo la kujiuliza Je! ilikuwa ni hotuba yake ya mwisho wa mwezi? kama ndio, Je? ya Mwezi October na sept alitoa? kama Ndio, Je? ilikidhi misingi ya kuwa na hotuba ya kila mwezi? kama ndio, Je taifa linakabiliwa na mambo mawili tu 1. uchumi 2. katiba kama ndio, Je? mambo yaliyotokea punde kabla ya hotuba yake hayakuwa na maana kwa wazee ( wanachama wa CCM) kama issue ya MBEYA, ARUSHA na TABORA? kama ndio kwa nini hotuba zote za mwiza wa mwezi huwa anaongelea mambo yaliojiri ama yatayojili punde? kama ndiyo. vipi siku ile anaongea nao (wazee) na kusema hahitaji kura za wafanyakazi? ALIKURUPUKA
 
Wanabodi, Aliyoyazungumza jana ni ya kwake na ndiyo yanayotoka moyoni mwake, haya ni mambo ya I.Q, kwa waliomsikiliza in between the lines, wanaelewa nazungumzia nini!. Ndio maana kuna wengine wanafanya Ph.D na kui earn na wengine wanasubiri za kupewa, na kupigiwa tarumbeta za shangwe na mapambio, Dr fulani, mpaka kwenye taarifa za habari amepewa title hiyo ya Dr!.Kwa hili la kuitwa Dr silaumu kwa sababu sheria yetu inaruhusu, ndio maana tuna Dr. Kifimbo, Dr. Nguzukululu Jilala (RIP) na , maprofessor kibao, akiwemo Prof. Maji Marefu etc, lakini mtu unapotunukiwa doctorate ya heshima, angalau, ufananie kwa maneno na matendo!.Nimeambiwa UDSM enzi zile, wate wanaongia walikuwa lazima wagraduate, kulikuwa hakuna DISCO, hivyo vilaza wote walikuwa wakipoozwa kwa PASS ya GPA ya 2.0! ili angalauwatoke, na haya ndiyo matokeo!.
 
kwa kweli nyinyi wafusi wa Rais aliyeshindwa uchuguzi wa mwaka jana mnaota ndoto mbaya mkithani maneno yenu dhidi ya mtu binafsi yatatuondoa hapa tulipo na kusonga mbele.
 
watanzania tulipoacha kujenga hoja na kutumbukia kwenye mijadala ya kuwalenga watu ndio tukaanza kukwama kusonga mbele. Hali hii imetuathiri hadi kwenye mijadala ya kimataifa kwani hatuna kawaida ya kuongelea issue tunaongelea watu. muda mwingi tunautumia na kupoteza katika kukosoa
 
Hiyo ni mifano michache tu. Kwa ufupi ni kuwa kauli ya Rais kuwa yeye ndiye anatoa uhuru na kuwa anaweza kuuondoa uhuru huo wa kuwa "dikteta kidogo" haina msingi. Uhuru wetu hautoki kwa Rais. Period.

hii hotuba ya jk imemtia aibu sana................pale anaposema ya kuwa hata muundo wa muungano, bunge na mihimili mingine hatuwezi kujadili kama huo siyo udikteta nini?
 
Rais hafanyi kazi peke yake kwa hiyo kumlenga yeye binafsi muda unapotea sana. tungejikosoa na kusahihisha makosa yetu wote kwa mtu mmoja mmoja pengine tungepunguza athari za mtu tunayedhani katufikisha hapa tulipo lakini tunalala kwa kuhesabu makosa ya JK na kuchambua kwa kina. Muda huo huo tungeutumia kuchambua kwa kina sehemu yetu ya kazi makosa anayofanya JK kama kweli yapo yasingekuwa na impact kubwa kwetu lakini nasisi tumejiingiza kwenye makosa hayo hayo ya kushinda kutwa tukisutana kwa miaka 4 ijayo ya utaokuwa uongozi wa JK
 
tumewazoea kwani kuna siku mliwahi kusifu hotuba

Mzee wa dar Pipijojo najua ulikuwepo Please angalia my signature! hivi alikuwa amejipanga? mbona kipindi hiki atakuwa anakurupuka kila mara... kwa mwendo huu tutamsifia 1+1=5 ama kweli alikuwa anaongea na wazee wa bagamoyo. full waganga
 
Kikwete ameshindwa kazi! Anafikia kiwango sasa anaanza kutisha watanzania kwa kofia yake ya Urais.Akumbuke kuwa ana miaka minne tu atakuwa Raia wa kawaida kama walivyo wengine....Awe makini,Dunia sasa inabadilika yaliyomkuta Aroyo yasije yakamkuta nae!
 
Wanabodi,
Aliyoyazungumza jana ni ya kwale na ndiyo yanayotoka moyoni mwake, haya ni mambo ya I.Q, kwa waliomsikiliza in between the lines, wanaelewa nazungumzia nini!.
Ndio maana kuna wengine wanafanya Ph.D na kui earn na wengine wanasubiri za kupewa, na kupigiwa tarumbeta za shangwe na mapambio, Dr fulani, mpaka kwenye taarifa za habari amepewa title hiyo ya Dr!.

Kwa hili la kuitwa Dr silaumu kwa sababu sheria yetu inaruhusu, ndio maana tuna Dr. Kifimbo, Dr. Nguzukululu Jilala (RIP) na ,aprofessor kibao, akiwemo Prof. Maji Marefu etc, lakini mtu unapotunukiwa doctorate ya heshima, angalau. ufananie kwa maneno na matendo!.

Nimeambiwa UDSM enzi zile, wate wanaongia walikuwa lazima wagraduate, kulikuwa hakuna DISCO, hivyo vilaza wote walikuwa wakipoozwa kwa PASS ya GPA ya 2.0! ili angalauwatoke, na haya ndiyo matokeo!.

Huwezi kuwa kilaza ukawa rais wa nchi yeyote Duniani

Lazima uwe na uwezo wa ku-manuva na kufanya kile ambacho wengine hawakiwezi..(IQ)

Tatizo lako unafikiri IQ ni kufaulu kwa A darasani tu....far from it..

Kwa hiyo hoja yako ni muflis na wanaofikiri kama wewe nao ni muflis..

"soma kitabu cha Tony Blair the Journey" gordon brown alikuwa na IQ kubwa sana kupita tony lakini U-PM ulimshinda sana..

huu upupu ulioandika hapa unakupunguzia heshima
 
Wakati mwingine ananipashida najiuliza alikuwa anawaza nini mpaka kutamka hayo,lakini ukiludi nyuma ukajiuliza YAMEKWISHA TOKEA NA HAKUNA JINSI NDIO HIVYO TUNATATIZO LA KITAIFA NA WENGI NDIO HAO,TULIONAO HUKO JUU.

Manake wakati mwingine tuwalaumu wanasaikolojia na madaktari wetu kwa kuwa wahoga na waficha ukweli kuwa tunatatizo la msingi ambalo lilihitaji msaada wao kuweka mambo sawa na kutoa mbinu za kuepuka haya.
 
Uhuru wa uhuru wa maoni unatokana na katiba lakini Rais dikteta anaweza ku-tamper na katiba na kuwaondolea watu uhuru wao, ndicho alichokuwa anamaanisha JK. Alikuwa na pointi katika hilo na wala hujamkosoa chochote hapo. Kwani wewe MMM unataka kusema nchi zenye madikteta hazina katiba nzuri? Usitake kukosoa kitu kisichokosolewa hapo ila badala yake mwambie Mbowe ajibu kwanini alimsifia JK bungeni halafu baadaye anaanza kumgeuka kuwa hana haki ya kuunda tume ya katiba.
 
nimejaribu kutafuta furaha kwa njia ya kukosoa wengine bado sijapata. nimejiuliza mchango wangu kwa taifa langu bado sijaona. njia pekee nimeona niendelee kumwandama JK kwani ndio njia iletayo maendeleo
 
Back
Top Bottom