Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,987
- 20,273
Nafikiri tumshauri Rais Samia afanye uamuzi mgumu kunusuru uchumi wa nchi kwa mgogoro huu wa mafuta nchini.
Tarehe 27/28 July 2023 nchi za Afrika 49 kati ya 54 zinazotambuliwa na Umoja wa Mataifa zilishiriki Mkutano wa Afrika na Urusi mjini St. Petersburg nchini Urusi na mambo Makuu mawili ambayo Rais wa Urusi Vladmir Putin alitangazia dunia na kuahidi kwa Nchi za Afrika ni;
1. Biashara zote kati ya Mataifa ya Afrika na Urusi zitafanyika kwakutumia Sarafu za Mataifa husika na sarafu ya Urusi ya Ruble.
2. Putin alitangaza kuyapatia Mataifa ya Afrika Mafuta na Gesi kwa Bei rahisi (nusu bei na kusafirishiwa bure).
3. Kuyapatia Chakula na Nafaka BURE mataifa yote yenye Uhaba wa chakula hii ilijumuisha Kuanzia kusafirishiwa bure hadi katika nchi husika na kwakuanza, Urusi iliainisha Tani 50,000 za nafaka kutolewa bure kwa nchi 6 za awali wiki inayoanza jumatatu ya keshokutwa.
Tukio lingine kubwa ni kusamehewa madeni yote kwa nchi za Afrika. Hii inamaana madeni ya Tanzania kwa Urusi hasa yale ya Kipindi cha Vita na Uganda maarufu kama maneni ya EPA ambayo CCM iliwahi kuiba pesa zile na kufanyia uchaguzi kipindi cha 2005-2015. Pia madeni ya ununuzi wa Silaha za Kijeshi katika majeshi yetu na vyombo vingine vya Usalama.
Tanzia ni miongoni mwa nchi zilizoshiriki kikamilifu mkutano huo, na hata baada ya mkutano kuisha, Tanzania ilipewa upendeleo wa kipekee kwa kualikwa na Rais Putin kushiriki sherehe za maadhimisho ya majeshi ya majini nchini Urusi, ambapo Waziri Mkuu aliongozana na Putin katika manowari ya Kijeshi wakizuru na kukagua vikosi vyabaharini kikamilifu.
HOJA: Rais Samia tumia fursa hii ya kuwa Tanzania ni nchi isoyofungamana na Upande Wowote, Wafanyabishara waagize mafuta moja kwa moja Urusi kwakutumia Sarafu ya Tanzania. Tuache kuogopa mashinikizo ya kimagharibi ambayo yanazidi kuumiza taifa letu. Sisi ni nchi isoyofungamana na Upande Wowote. Tuitumie haki hii kama tulivyothubutu kushiriki mkutano huu ili tuokoe watu wetu.
Matunda ya kushiriki Mkutano ule na kupata fursa ile, ni kuzitumia fursa hizi, biashara ya mafuta hatufungwi na sheria yoyote ya Kimataifa zaidi ya matumizi ya Dola tu ndio yanayotufunga, tunaweza kununua popote. Fursa ya kununua kwa kutumia Shilingi yetu imepatikana kutoka MOSCOW, tunataka nani atuamulie jambo hili?
Moscow inavikwazo vya Kimataifa, je, fursa ya Urusi waliyoitoa ya kutuletea wao wenyewe mafuta hadi bandaniri Dar es Salaam kwanini tusiitumie?
Kama sio hivyo kwanini tusipate kwa njia mbadala mfano, Nchi za OPEC zinauza mafuta, na Urusi ni mkuu wa OPEC, kwanini tusinunue mafuta ya Urusi kupitia Dubai, Oman, Saudia nk kwa mwamvuli wa OPEC transit?
Hivi nani anatakiwa kutusimamia kucheza game hizi ndogo kabisa kama sio sisi wenyewe?