Ugonjwa wa Malaria

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,348
33,186
Vaccine---Health.jpg




Malaria ni nini? Malaria ni ugonjwa wa kuambukizana unaoletwa na chembe chembe zinazoitwa plasmodium.Chembe chembe hizi huingia ndani ya mwili wa binadamu baada ya kuumwa na mbu wa kike kwa jina Anopheles. Mbu mwenye chembe chembe za plasmodium anapomuuma mtu,humuingizia baadhi ya mate yenye viini vya kuambukizana kwenye kidonda hivyo kusabaza Malaria. Viini hivi husafiri hadi kwenye maini ambapo hukaa hadi vifikie ukomavu. Viini hivi baadaye huingia na mtu kama huyu akiumwa na mbu,mbu huyu hubeba chembe chembe hizi na anaweza kumuambukiza mtu atakaye muuma.
2_other_children_small.JPG

Kuna aina 4 za Malaria: P. vivax, P. malariae, P. ovale na P. falciparum. Zimepewa majina kulingana na aina ya plasmodium inayozisababisha. Aina 3 za kwanza sio hatari lakini Falciparumni hatari sana na hata inaweza kusababisha kifo. Hii ni kwa sababu ikishaingia tu mwilini huzaana kwa wingi ndani ya damu.. Hii ni kwa sababu chembe chembe nyekundu za damu(ambazo husambaza oksijeni mwilini)zilizoadhirika huwa nzito na haziwezi kuingia kwenye kapilari. Hii husababisha kufa kwa sehemu ya ubongo,maini,mapafu,figo na matumbo kwa sababu ya ukosefu wa oksijeni. Hali hii inaweza kusababisha kifo kama haita tibiwa haraka.

Malaria hutambulika vipi?

Baridi,kuuma kwa misuli na kichwa zinaweza kuwa dalili za magonjwa mengi mengine. Njia ya pekee unayoweza kudhihirisha kama una Malaria ni kuenda hiospitalini kupimwa damu. Watu wengi wanaotoka sehemu zilizoadhirika na Malaria pindi wanapoona dalili hizi huenda kwenye maduka ya kuuza madawa kununua dawa za kupambana na Malaria. Huu sio ushauri mzuri. Ni muhimu kupimwa damu ili aina ya plasmodium inayosababisha maradhi yako itambulike na upewe matibabu yanayostahili.

Nani yuko kwenye hatari ya kuambukizwa Malaria?

Watoto wachanga,watoto na akina mama waja wazito wako kwenye hatarikubwa ya kushambuliwa hata kufa kutokana na Malaria. Watoto wachanga na watoto wako kwenye hatari kwa sababu wameambukizwa mara chache nahawajajenga

kinga dhidi ya chembechembe hiziVamizi la Malaria kwa wanawake wajawazito kalikwa sababu kinga yao dhidi ya maradhi huwa chini wakati wa uja uzito. Malaria huongeza tishio kwa mtoto ambaye hajazaliwa kama kuzaliwa kabla ya wakati

kutimia, uaviaji wa mimba, maambukizi ya sehemu za siri, uzani mdogo wa mtoto anapozaliwa, kupoteza uja uzito na pia ugonjwa huu unaweza kumsababishia mama kifo.


Naweza jilinda vipi dhidi ya Malaria?

  1. Msafiri: Kama unasafiri hadi kwenye eneo linalolotambulika kwa Malaria,mtembelee daktari wako ili akupe dawa mahsusi ya kupambana na Malaria ya eneo unalotembelea.Hakikisha umefuata maelezo vizuri.
  2. Wenyeji wa maeneo yalioadhirika na Malaria: Mbu wa aina ya anopheles hupenda kuuma watu nyakati za macheo na machweo kwa hivyo ni bora kujikinga nyakati hizi.Wakati wa machweo unaweza keti ndani ya nyumba iliyoekewa dawa na usiku unaweza kulala neti iliyotibiwa.
  3. Haribu sehemu mbu wanapozaliana: Kipindi cha mwisho katika ukuaji wa mbu hufanyika majini.Mbu wa aina ya anopheles hupendelea maji yasiyo ya chumvi.Ni muhimu kuharibu ama kunyunyuzia na dawa sehemu zote ambazo mbu wanaweza kutaga mayai.Unafaa kutoa chupa,ndoo ama chochote ambacho kinaweza kusimamisha maji,bacillus thuringiensis(Bti) dawa asili ya kuua wadudu kutoka BioVision inaweza kutumiwa kuua mbu wachanga bila kuharibu maji.
  4. Watoto na mama waja wazito lazima wakingwe na Malaria: Nchini Kenya,wanawake waja wazito wana haki ya kupata matibabu 2 ya bure na neti zilizotibiwa. Chukua moja kutoka katiki kliniki yako.
  5. Neti zilizotibiwa: Kila mtu anapaswa kupata neti iliyotibiwa.Kuna aina mbili ya neti hizi nchini Kenya ambazo zinauwa mbu pindi tu wadudu hawa wanapozigusa.Kuna zile zinazopaswa kutibiwa kila baada ya miezi 6nba PowerTabs na zile zinazodumukwa miaka 3 hadi 5 baada ya kutibiwa

Ni zipi dalili za Malaria?

Dalili za Malaria ni kama zile za Flu; homa, baridi na kuuma kwa misuli na kichwa. Watu wengine hupatwa na kichefuchefu, kutapika na kuharisha. Vipindi vya baridi, homa na kutokwa na jasho hujirudia kila siku moja, mbili au tatu. Watu wenye aina ya P. falciparum wanaweza kupata Malaria ya ubongo ambayo husababisha kuishiwa na fahamu ama kuchanganyikiwa kiakili.

Tiba ya Malaria

Tiba ya Malaria inategemea mambo kadhaa:
  • Hali ya mgonjwa (mtoto, mama mja mzito, mtu mzima, ni kali ama sio kali)
  • Nguvu ya dawa dhidi ya ambukizo la viini vya plasmodium.
  • Eneo la kijiografia ambalo mtu aliambukizwa. Kwa mfano, P.falciparuminayopatikana katika nchi za Mashariki ya kati inaweza kutibiwa na dawa ya chloroquine, lakini inayopatikana Africa, katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara haitibiki kwa chloroquine.
  • Aina ya plasmodium inayodhuru mgonjwa. Malaria yasiyo makali hutibiwa na dawa za kumeza ilhali wagonjwa wenye P. falciparum kali hulazwa hospitalini na kupewa sindano ya maji.
Kwa bahati mbaya aina fulani za plasmodium zimeleta upinzani dhidi ya dawa ya chloroquine.








 
Asante sana Mzizi mkavu ningependa kuongezea hapo kwenye dawa mbali na Dawa za hospital kama quinine kwa malaria sugu(p.falciparum) ALU and Sp kwa malaria yakawaida etc . Kuna Dawa mbadala ya kienyeji ambayo wengi hawaijui ambayo hutibu na kuondoa malari ndani ya siku tano, Mbegu za mpapai zikaushiwe ndani bila kukutana na mwanga wa jua, baada ya kukauka zipondwepondwe na kuzisaga harafu zichujwe kwa chujuo ili kupata unga wake, chukua kijiko kidogo jaza weka kwenye kikombe cha maji ya moto changanganya kunywa mara mbili kwa siku ukitumia na panando ndani yasiku tano malaria kwisha
 
Naam mzizi mkavu, Habari za siku 2/3 hivi je mimi uwa ninatatizo kubwa la kiafya, lila mara ninapo jielekeza maabara kuchukuluwa dam kwa kipimo cha malaria iwe ya mshipa ao ya kidole uwa sipatikaikani maleria ila ninapo tumia dawa tu napona aijui ni kwanini? Waweza kunisaidia kitu chochote hapo yani napenda kufaham kuwa nihali ya kawaida? Mana tumeambiwa tusi tumie dawa bila vipimo!!!
 
Naam mzizi mkavu, Habari za siku 2/3 hivi je mimi uwa ninatatizo kubwa la kiafya, lila mara ninapo jielekeza maabara kuchukuluwa dam kwa kipimo cha malaria iwe ya mshipa ao ya kidole uwa sipatikaikani maleria ila ninapo tumia dawa tu napona aijui ni kwanini? Waweza kunisaidia kitu chochote hapo yani napenda kufaham kuwa nihali ya kawaida? Mana tumeambiwa tusi tumie dawa bila vipimo!!!
Usile dose yeyote bila kuwa
Prescribed by the doctor hii itakufanya upunguze kinga Yako ya mwili, Fanya vipimo maradhi Yako mengi sio kila homa ni malaria..
 
Back
Top Bottom