Ugonjwa wa macho(red eyes)

delako

JF-Expert Member
Oct 6, 2012
2,743
1,492
Habari wanajf,

Kuna kitu kinanishangaza katika ugongwa huu wa macho ambao umezoeleka kama red eyes,nikiwa kama mmoja wa niliopata tatizo hili tena kwa mara ya kwanza toka nimeanza kuusikia au kuona watu wakiumwa macho.

Kinachonitatiza au swali langu kwa mwenye kujua ni kwamba,kwanini kila mtu anayeanza kuumwa macho ataanza na jicho la kushoto?

Nimefikia kuamini kuwa mgongwa anaanza kuumwa jicho la kushoto kwani mimi lilianza hivyo,mdogo wangu naye ikawa hvyo,kuna majirani kama wanne hivi nao wameanza na jicho la kushoto!Je wakuu imani yangu hii ni sahihi?

Je, kuna uchunguzi wowote wa kisayansi uliothibitika km ni kweli mgonjwa huanza kupata madhara ktk jicho la kutosha?

Nawasilisha.
 
Habari wanajf,
Kuna kitu kinanishangaza katika ugongwa huu wa macho ambao umezoeleka kama red eyes,nikiwa kama mmoja wa niliopata tatizo hili tena kwa mara ya kwanza toka nimeanza kuusikia au kuona watu wakiumwa macho.
Kinachonitatiza au swali langu kwa mwenye kujua ni kwamba,kwanini kila mtu anayeanza kuumwa macho ataanza na jicho la kushoto?Nimefikia kuamini kuwa mgongwa anaanza kuumwa jicho la kushoto kwani mimi lilianza hivyo,mdogo wangu naye ikawa hvyo,kuna majirani kama wanne hv nao wameanza na jicho la kushoto!Je wakuu imani yangu hii ni sahihi? je kuna uchunguzi wowote wa kisayansi uliothibitika km ni kweli mgonjwa huanza kupata madhara ktk jicho la kutosha?
Nawasilisha.
TIBA YA DAWA KUWA MACHO MEKUNDU

TIBA(1) Weka macho yawe safi na uyakoshe kwa maji ya waridi kila wakati. Epusha macho kutokana na joto, baridi, moshi, vumbi, macho yasitumie nguvu sana kama vile kusoma sana. Tumia dawa za kulainisha choo ikiwa hupati choo vizuri kwa sababu pia huchangia katika maumivu ya kichwa na macho.awe pia anakula karoti.
 
Habari wanajf,
Kuna kitu kinanishangaza katika ugongwa huu wa macho ambao umezoeleka kama red eyes,nikiwa kama mmoja wa niliopata tatizo hili tena kwa mara ya kwanza toka nimeanza kuusikia au kuona watu wakiumwa macho.
Kinachonitatiza au swali langu kwa mwenye kujua ni kwamba,kwanini kila mtu anayeanza kuumwa macho ataanza na jicho la kushoto?Nimefikia kuamini kuwa mgongwa anaanza kuumwa jicho la kushoto kwani mimi lilianza hivyo,mdogo wangu naye ikawa hvyo,kuna majirani kama wanne hv nao wameanza na jicho la kushoto!Je wakuu imani yangu hii ni sahihi? je kuna uchunguzi wowote wa kisayansi uliothibitika km ni kweli mgonjwa huanza kupata madhara ktk jicho la kutosha?
Nawasilisha.

Wrong hypothesis and wrong conlusion.Mimi ulinianza jicho la kulia.
 
hauna dawa maalumu. so kama unao we uwe unasafisha tu macho kila wakati. kama yanauma tumia dawa ya kudondoshea matone kutwa mara 3
 
huu ugonjwa kama unaanza kukupata basi macho huwa mazito, machoz yanatoka yenyewe, pia kuna kauvimbe jichoni ambapo mtu unahisi kama kuna mchanga jichoni
 
Red eyes inasababishwa na viral infection hususan wale adenoviruses wakishambulia conjuctiva na kusababisha mishipa midogo ya damu kupasuka na damu kuvia

Dalili zake ni macho kuwasha,kuwa kama umeingiwa mchanga,kuvimba na kuwa mekundu,alama za damu iliyovia na conjuctivitis

Mara nyingi huendana na secondary bacterial infections kwa sababu damu ni medium nzuri sana kwa ukuaji wa bacteria

Red Eyes ni self limiting,inapona yenyewe baada ya siku 3 hadi tano kwa kutegemea na kinga ya mwili ya mtu,na namna unavyoyatunza macho yako kipindi cha ugonjwa

Wakati mwingine,ili kuzuia bacteria wasishambulie huwa wanatumia antibiotics kama Gentamycin,in form of eye drop au Chloramphenical

Ukipata red eyes,safisha macho yako mara kwa mara kwa maji safi,epuka kufikicha na tumia antibiotics

Pia ukiugua red eyes,itakuacha na kinga ya kudumu hivyo hutougua tena

Wengine wataongezea taarifa na kusahihisha ikibidi!!
 
Habari ndugu!!!....kuna huu ugonjwa maarufu sana hapa jijiji dar,ugonjwa wa macho,red eyes...unaofanya macho kuwasha na kuuma na kuwa mekundu sana na kuvimba..ni nini chanzo chake na namna ya kujikinga usikupate
 
Wanafunzi DUCE wakumbwa na ugonjwa wa Macho Mekundu (Red Eyes)
Jicho-jekundu.jpg

JICHO ni moja ya kiungo muhimu katika mwili wa binadamu, ugonjwa wa macho mekundu, maarufu kama 'Red Eyes' ni moja ya magonjwa ya muda mrefu na imekuwa ni hali ya kawaida ya kila mwaka wakazi wa maeneo mbalimbali kukumbwa na ugonjwa huo hususani wanafunzi wa Vyuo Vikuu.

Maeneo ya jirani na vilipo vyuo hivyo wananchi wanakumbwa na ugonjwa huo, huku wagonjwa mbalimbali wakiripotiwa kuugua ugonjwa huo katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es salaam (DUCE).

FikraPevu imeshuhudia wengi wa wagonjwa wakiwa katika hali ya awali ya ukuaji wa ugonjwa huo na macho yao yameonekana kuwa mekundu na kuvimba kama ilivyo kawaida ya ugonjwa huo katika dalili zake za awali.

Mmoja wa wauguzi katika Zahanati ya Chuo hicho (hakupenda jina lake litajwe kwa kuwa si msemaji) alisema hadi Januari 20, 2014 idadi ya wagonjwa waliofika katika Zahanati hiyo kupatiwa matibabu ilikuwa ni wanafunzi 700 (idadi hii inaongezeka kila siku) na wengine hawaendi katika Zahanati hiyo kutibiwa (wanaenda kutibiwa nje ya Zahanati hiyo).

Baadhi ya wagonjwa walioambukizwa ugonjwa huo walionekana kuvaa miwani myeusi kusitiri macho yao mbele za watu, na kwamba ugonjwa huo ulianza tangu wiki moja iliyopita.

Amiri Juma, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni hapo amesema pamoja na serikali kujitahidi kutoa fedha za kujikimu kwa wanafunzi wa elimu ya juu zamu hii hali imekuwa tafauti kwa utoaji wa huduma hiyo kwani hali ni ngumu kwa wanafunzi wanaotegemea fedha hizo boom.

Ugonjwa wa 'Red Eyes'

Ugonjwa wa macho mekundu kwa kawaida unasababishwa na kitu kinachoitwa tabaka la juu ya jicho hali ambayo inatakiwa ilifanye jicho kuwa jeupe na linapobadilika na kuwa jekundu hapo ndipo binadamu anapotakiwa kujua kuwa tabaka jeupe linaleta chakula na hewa kwa ujumla wake. Pia vipo vimishipa kwenye macho ambavyo vinapovimba husababisha ugonjwa wa Red Eyes.

Hadi sasa chanzo halisi cha ugonjwa huo hakijajulikana kuwa unatokana na nini lakini tafiti zinaonyesha kuwa vipo viashilia vinavyoonyesha kuwa ugonjwa huo unatokana na kuwepo kwa michirizi inayokatiza kwenye jicho ambayo huathirika mfumo wa damu.

Sababu ya jicho kuvimba inatokana na vumbi, mzio/aleji na inaweza kuwa moshi, unywaji wa pombe, kuchelewa kulala na mwingine anaweza kukumbana na hali ya mishipa kujikunja hali inayopelekea mishipa kushindwa kusambaza damu kama kawaida.

Daktari Erick Matimbwi, mtaalamu wa tiba mbadala jijini Dar es Salaam, anasema sababu nyingine ya ugonjwa huo ni kuwa na ugonjwa wa Shinikizo la damu la juu na ukosefu wa vitamin A. B3 au B6 na kwamba idadi kubwa ya watu wanaweza kuambukizwa ugonjwa huo kwa wakati mmoja katika baadhi ya nchi za Afrika.

Utumiaji wa vitamin A, B, B6 na nyingine chachu zitokanazo na vitamin za mboga za majani, matunda kwa wingi vinasaidia kuweka kinga ya kuugua ugonjwa huo pamoja na kula maharage kwa wingi kwani inasababisha vitamini B.

Moja ya sababu inayotajwa kusababisha hai hiyo ni neon la kitaalamu lijulikanalo kama chavua katika anga hewa licha ya asili ya macho kuwa na uzio wa kuzuia kitu isichopata na acho kukizuia ili kisiingie ndani.

Aidha, imeelezwa kuwa ugonjwa huo unasababishwa na aina mbalimbali za bacteria. Watu wenye umri wa miaka 40 na kuendelea kwa kawaida mamcho yaop huwa mekundu kuliko vijana.

Tafiti zinaonyesha kuwa macho ya mwanadamu hayatakiwi yazidi kuwa mekundu na watu waliochini ya umri huo wanatakiwa kuwa makini wanapoona macho kuwa mekundu wazingatie kwende kwa madaktari kujua chanzo na tiba.

Mgonjwa anapohitaji tiba anatakiwa kutumia njia ya kumuona mtabibu haraka iwezekanavyo ili kujua kama jicho lina bacteria au limeathiriwa na mwanga mkali ambao pia unasababisha ugonjwa wa mamcho kuvimba na kwamba uvaaji wa miwani meusi inaweza kusababisha mikunjo ya mishipa ya damu.

Copy: Wanafunzi DUCE wakumbwa na ugonjwa wa Macho Mekundu (Red Eyes)
 
Red eyes inasababishwa na viral infection hususan wale adenoviruses wakishambulia conjuctiva na kusababisha mishipa midogo ya damu kupasuka na damu kuvia

Dalili zake ni macho kuwasha,kuwa kama umeingiwa mchanga,kuvimba na kuwa mekundu,alama za damu iliyovia na conjuctivitis

Mara nyingi huendana na secondary bacterial infections kwa sababu damu ni medium nzuri sana kwa ukuaji wa bacteria

Red Eyes ni self limiting,inapona yenyewe baada ya siku 3 hadi tano kwa kutegemea na kinga ya mwili ya mtu,na namna unavyoyatunza macho yako kipindi cha ugonjwa

Wakati mwingine,ili kuzuia bacteria wasishambulie huwa wanatumia antibiotics kama Gentamycin,in form of eye drop au Chloramphenical

Ukipata red eyes,safisha macho yako mara kwa mara kwa maji safi,epuka kufikicha na tumia antibiotics

Pia ukiugua red eyes,itakuacha na kinga ya kudumu hivyo hutougua tena

Wengine wataongezea taarifa na kusahihisha ikibidi!!
Mkuu kuhusu vidonda vya macho inakuwaje
 
Back
Top Bottom